Dedan Kimathi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kwa maana nyingine, tazama: Dedan Kimathi (kata).
Sanamu ya Dedan Kimathi Nairobi, Kenya.

Dedan Kimathi (Thenge, tarafa ya Tetu, kaunti ya Nyeri, 31 Oktoba 1920 - 18 Februari 1957) alikuwa Mkenya aliyeongoza harakati za kundi la Mau Mau za kutwaa ardhi iliyokuwa iko mikononi mwa wakoloni toka Uingereza.

Kimathi alihukumiwa na kunyongwa kutokana na harakati zake za kuikomboa nchi ya Kenya. Serikali ya wakoloni Waingereza ilimchukua Kimathi kama gaidi, lakini wananchi wengi wa kabila la Gikuyu walimchukua kama mpigania uhuru.

Maisha ya mwanzo[hariri | hariri chanzo]

Alipofika miaka kumi na mitano, Kimathi alijiunga na shule ya msingi, Karuna-ini, ambapo aliweza kujifunza kiingereza halisi. Hii baadaye ilimsaidia kuandika kwa kiingereza kabla ya mnyanyuko na wakati wa mnyanyuko wa Mau mau. Akiwa shuleni alijiunga kwa chama cha ushauri. Alikua muumini wa dini na alibeba Bibilia kila wakati. Alifanyia kazi idara ya misitu kuokota begu za miti, ili aweze kujilipia gharama ya shule. Baadaye akajiunga na shule ya upili ya Tumutumu CSM, lakini akaacha shule kwa sababu ya kutolipa gharama ya shule.

Kimathi alifanya kazi kadhaa lakini hakupata msimamo. Mojawapo ya kazi hizo alijiunga na jeshi na kutumwa kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia mwaka wa 1941. Lakini, mwaka wa 1944, alifukuzwa jeshi kwa sababu ya makosa kadhaa. Mnamo 1946, alijiandikisha kwa chama cha Muungano wa Waafrika Wakenya. Mnamo 1949, alianza kufunza shule alikosomea, lakini wakamfukuza kazi kwa sababu ya kulaumiwa amefanya ubakaji. La kuaminika ni kwamba alipigwa kalamu kwa makosa ya uchochezi.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Kimathi aliweza kuvutia watu kwa kuonyesha bidii kwa kazi aina zote, alizoweza kufanya. Kimathi alianza siasa za upinduzi mwaka wa 1950. Alianza kuwa mfuasi wa Mau Mau, na baadaye kupanda cheo na kuweza kuwapa wajiunga wapya kiapo cha Mau Mau na kwa hivyo akawa gaidi kulingana na Waingereza. Alijiunga tena na Kikundi ya Arubaini, wakombozi wa Chama cha Kati cha Wakikuyu mwaka wa 1951. Alichaguliwa kama karani kwa chama cha KAU eneo la Ol' Kalou na eneo la Thomson Falls mwaka wa 1952. Alishikwa kwa mmda mwaka huo, lakini akatoroka kwa usaidizi wa polisi wa kijiji. Hii ilileta mwanzo wa Vita vya ukereketwa halisi. Kimathi aliunda baraza la ulinzi wa Kenya, ambayo ilitoa amri kwa wapiganaji wote msituni mwaka wa 1953.

Mwaka wa 1956, alishikwa pamoja na bibi yake mmoja, Wambui. (hadithi nyingi za Kimathi zaeleza vile alivyopigwa risasi.) Alihukumiwa kifo na mahakama, na Jaji wa sheria Chifu Kenneth O'Connor, akiwa bado kitandani katika hospitali kuu ya Nyeri. Asubuhi na mapema mnamo 18 Februari 1957 alinyogwa na serikali ya wakoloni Waingereza.

Urithi[hariri | hariri chanzo]

Kimathi alizikwa kwenye kaburi la umma mahali pasipojulikana katika gereza la Kamiti. Serikali ya Uingereza mpaka sasa inapinga maiti ya Kimathi ifukuliwe ili azikwe tena kirasmi, kwasababu wanasema alikuwa gaidi. Lakini Wakenya wengi wamchukulia kuwa Shujaa wa Taifa. Jina la Kimathi linakumbukwa nchini Kenya hasa kutokana na mitaa ya miji, majengo mengi na pia barabara ambazo zimeitwa kwa jina lake. Mchezo wa Kuigiza wa "Mzalendo Kimathi" ama kwa kiingereza The Trial of Dedan Kimathi umeandikwa na Ngugi wa Thiong'o (ndugu wa shujaa wa Mau Mau) akishirikiana na Micere Mugo na mchezo huo unaeleza kisa cha Kimathi.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]