Uhuru Kenyatta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Uhuru Kenyatta.

Uhuru Muigai Kenyatta (amezaliwa 26 Oktoba 1961) ni mwanasiasa nchini Kenya ambaye ni rais wa nne na wa sasa wa Jamhuri ya Kenya. Aliapishwa tarehe 9 Aprili, 2013. Alizaliwa kama mwana wa kwanza wa Jomo Kenyatta aliyekuwa rais wa Kenya na mke wake Ngina Muhoho aliyeitwa Mama Ngina.

Kuingia katika siasa[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kumaliza masomo alishughulika hasa biashara za familia alizorithi kutoka kwa babake. 1997 alijaribu kuingia mara ya kwazna katika siasa lakini alishindwa katika uchaguzi wa bunge.

1999 rais Daniel arap Moi aliimpa cheo cha mwenyekiti wa bodi ya utalii. Moi aliendelea kumpandisha ngazi kwa kumpa nafasi ya mbunge wa kitaifa na waziri msaidizi.

2002 akawa makamu wa mwenyekiti wa KANU.

Mgombea wa urais 2002[hariri | hariri chanzo]

Tangu Julai 2002 ilionekana wazi ya kwamba Moi alimtaka kama mgombea wa urais upande wa KANU atakayemfuata katika ikulu. Mkutano mkuu wa KANU katika mwezi wa Oktoba 2002 uliitikia mapenzi ya rais ukamtangaza Uhuru kama mgombea wa urais.

Tendo hili lilisikitisha wanasiasa wengi wasiokuwa Wakikuyu na kutegemea nafasi hii kwa ajili yao wenyewe. Waliondoka katika KANU na kuendelea katika ushirikiano wa upinzani wa NARC.

Uhuru ulishindwa katika uchaguzi wa 2002 alipata asilimia 31 za kura tu.

Kiongozi wa upinzani na wa chama[hariri | hariri chanzo]

Katika bunge jipya alikuwa kiongozi wa upinzani lakini aliona pia upinzani ndani ya chama hasa kutoka kwa Nicholas Biwott pamoja na wanasiasa kutoka Bonde la Ufa. Kwenye mkutano wa chama cha Januari 2005 Uhuru alithebitishwa kwa kura nyingi na Biwott aliunda chama cha New Kanu.

Upingamizi dhidi yake ndani ya KANU[hariri | hariri chanzo]

Katika kura maalumu ya wananchi kuhusu katiba Uhuru alishikamana na viongozi wa LDP katika kambi ya machungwa. Mipango yake ya kushiriki katika Orange Democratic Movement (ODM) yalipingwa vikali ndani ya chama kwa sababu wanaKANU pamoja rais mstaafu Moi waliogopa kupotea kwa chama cha kwanza katika historia ya Kenya.

Katika Novemba 2006 Biwott alirudia jaribio la kumpindua Uhuru kwa kuita mkutano wa Kanu mjini Mombasa bila idhini ya mwenyekiti wala kamati ya chama. Hapa alichaguliwa kuwa mweyekiti mpya. Kwa msaada wa serikali Biwott alifaulu kuandikisha kamati yake kama uongozi rasmi hivyo kumwondoa Uhuru katika nafasi ya kiongozi wa upinzani bungeni. Uhuru alipinga na mahakama kuu ikabatilisha kura ya Mombasa tar. 29 Desemba 2006 ikathbitisha azimio hili katika Juni 2007.

Kuhamia upande wa Kibaki 2007[hariri | hariri chanzo]

Juni 2007 Uhuru alionyesha wazi ya kwamba alitaka kuacha ushirikiano wa ODM kwa kutopeleka jina lake kati ya wagombea wa urais upande wa ODM. Badala yake alieleza ya kuwa atampigania rais Kibaki achaguliwe tena.

Katika uchaguzi wa 2007 Uhuru alichaguliwa tena katika kama mbunge Garundu Kusini kwenye tiketi ya KANU.

Kenyatta, Uhuru