Nenda kwa yaliyomo

Kilipukaji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kilipuzi)
Tangazo la onyo mahali penye vilipukaji
Milipuko kwenye maonyesho

Kilipukaji (pia kilipuzi [1]) ni kemikali au dawa yenye sifa ya kumenyuka haraka na ghafla kwa umbo la mlipuko. Mmenyuko huo unatoa joto na gesi inayopanuka na kusababisha mshtuko.

Kilipukaji kinachojulikana zaidi ni baruti iliyotumiwa katika silaha lakini leo nafasi yake imechukuliwa na TNT hasa. Vingine hutumiwa kwa milipuko ama ya kijeshi au ya kiraia (ujenzi wa barabara, migodi, windo la mawe).

Kemia ya kilipukaji

[hariri | hariri chanzo]

Kemikali za vilipukaji zina kiasi cha oksijeni ndani yake katika muungo wa kikemia. Muungo huu ndani ya kilipukaji si imara sana kikemia na kuna uwezekano wa kusababisha mbunguo wa haraka unaotenganisha oksijeni pamoja na kuweka huri nishati ya joto. Joto wakati wa mlipuko inaweza kufikia sentigredi maelfu. Oksijeni inaingia katika kampaundi mpya ya gesi zinazopanua mara moja na kuleta mshuto kwa mazingira.

Kuna pia vilipukaji vya nguvu ndogo zaidi ambavyo ni mchanganyiko wa kemikali zinazochoma haraka pamoja na kemikali yenye oksijeni.

Kuwasha kilipukaji

[hariri | hariri chanzo]

Mlipuko husababishwa ama kwa mshtuko (pigo) au kwa joto. Baruti inahitaji moto ili ilipuke. Kuna pia vilipukaji vinayopasuka vikisikitishwa tu. Lakini hali halisi haiwezekani kutumia kemikali ambazo zinawaka mara moja baada ya mshtuko mdogo kwa sababu hizi ni hatari mno kwa mtumiaji.

Kwa hiyo vilipukaji vinavyotumiwa ama kijeshi au kiraia haviathiriwi nyepesi. Mmenyuko wa kikemia huanzishwa kwa kiwashio ambacho ni kiasi kidogo cha kemikali kali zaidi inayoungwa katika kilipukaji wakati wake. Kiwashio kinawaka ama kwa pigo au kwa joto kwa mfano kwa njia ya umeme na mlipuko wake unaanzisha mmenyuko wa kilipukaji kikuu.

  1. Kilipukaji ni msamiati wa KKK/ESD p. 271; Kilupizi wa Kamusi Kuu uk. 456