Wikipedia:Makala kwa ufutaji/Nyaraka 5

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Hii ni nyaraka ya makala Wikipedia:Makala kwa ufutaji ya mwaka 2019.

Kwa nyaraka za zamani zaidi angalia hapa.


Makala zilizopelekwa hapa 2019[hariri chanzo]

Makala kuhusu Hoyce Anderson ifutwe isipoboreshwa haraka. Kwa sasa haina habari yoyote isipokuwa jina na tarehe ya kuzaliwa. Tena jina la makala linatumia HERUFI KUBWA ambayo haikubaliki. Kipala (majadiliano) 07:26, 20 Oktoba 2018 (UTC)[jibu]

Imeelekezwa ukurasa sahihi. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:18, 19 Februari 2019 (UTC)[jibu]

Makala haina habari kuhusu mhusika. Kama hazipatikani heri ingefutwa. Kipala (majadiliano) 07:44, 22 Oktoba 2018 (UTC)[jibu]

Je kuna sababu gani kumpa mtu huyu makala? Hakuna ushuhuda ana umaarufu wowote. Makala za wikipedia hazifai kabisa kama marejeo. Heri makala ifutwe. Kipala (majadiliano) 13:32, 4 Desemba 2018 (UTC)[jibu]

Hakuna yaliyomo, hakuna vyanzo, na topic haina maana. Kipala (majadiliano) 09:35, 15 Desemba 2018 (UTC)[jibu]


Lugha irekebishwe au ifutwe. Tafriri ya kompyuta. Haieleweki. --Ndesanjo (majadiliano) 04:29, 2 Januari 2019 (UTC)[jibu]

Nimeacha kiini chake tu. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:25, 19 Februari 2019 (UTC)[jibu]

Kuna sentensi 1 tu , Kiswahili kibaya. Isahihishwe au kufutwa. Kipala (majadiliano) 17:29, 15 Februari 2019 (UTC)[jibu]

Nimeirekebisha. Inaweza kubaki ingawa ni fupi. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:30, 19 Februari 2019 (UTC)[jibu]

Hakuna matini hata kidogo, ni mkusanyiko wa picha za pasipoti tu. Hata jina la makala si Kiswahili kweli, inaonekana kama tafsiri ya google. Sioni sababu ya kuwa nayo. Kipala (majadiliano) 07:00, 19 Februari 2019 (UTC)[jibu]

Ni zote makala fupi sana zilizoanzshwa na mtumiaji: Bilyan7777 ambaye hajui Kiswahili. Zote hazieleweki. Zifutwe. Kipala (majadiliano) 07:08, 19 Februari 2019 (UTC)[jibu]

Advertising--94rain (majadiliano) 09:11, 23 Februari 2019 (UTC)[jibu]

Kuna kurasa nyingi za namna hiyo; shida hatuelewi lugha! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:05, 25 Februari 2019 (UTC)[jibu]

Huyu anajinadi. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:05, 25 Februari 2019 (UTC)[jibu]

Alitafsiri sentensi chache, mengine Kiingereza. Kipala (majadiliano) 21:13, 26 Februari 2019 (UTC)[jibu]

Ameshatafsiri baada ya kuonywa. Kipala (majadiliano) 21:40, 26 Februari 2019 (UTC)[jibu]

Mchangiaji mpya, nilimwomba akamilishe, menginevyo tufute haraka. Kipala (majadiliano) 09:18, 13 Aprili 2019 (UTC)[jibu]

Makala haikuwa katika muundo wa Kiwiki na wala haijaeleza dhima ya maandishi. Ukisoma mtiririko wako ni kama kitabu hivi. Lakini hajaweka viungo vya nje na wala hakuna pa kupata habari zake. Hivyo ninapendekeza ifutwe tu.--Muddyb Mwanaharakati Longa 15:24, 17 Aprili 2019 (UTC)[jibu]

Mtumiaji asiyejiandikisha alileta hapa matini ya matangazo ya kibiashara kuhusu kitabu fulani. Matini hailingani na fomati zetu. Haelezi wala mwandishi ni nani wala haelezi yaliyomo ya kitabu. Inawezekana ya kwamba kitabu hiki inaweza kustahili makala lakini matini hii haistahili kubaki kwenye wikipedia. Ifutwe. Kipala (majadiliano) 19:29, 20 Aprili 2019 (UTC)[jibu]

Shule ya msingi - hakuna umaarufu wa kutosha ili ipate makala. Inaweza kutajwa katika makala ya kata. Ilianzishwa na mchangiaji mpya aliyejaribu pia kuingiza makala juu yake mwenyewe na mmoja wa ndugu zake (ambazo nilifuta mara moja), ameingiza jina lake hapa pia. Kipala (majadiliano) 05:51, 26 Mei 2019 (UTC)[jibu]

Sielewi kusudi la makala hii. Ni mkusanyiko wa maoni (bila kutaja chanzo - inaonekana ni maoni ya mwandishi, jambo linalokataliwa kwetu). Mengi ni kweli kwa lugha yoyote, mengine inaweza kupingwa eti si kweli. Hakuna sababu aumaelezo kwa maoni haya. Ifutwe. Kipala (majadiliano) 09:45, 27 Mei 2019 (UTC)[jibu]

Mtumiaji: Saidi lihuwi alinakili sehemu za makala Teresa wa Mtoto Yesu, hana amelezo ya ziada. Pia alitunga jina la makala lisilo kawaida kwa Teresa, maana mafundisho kuhusu "Moyo Mtakatifu wa Yesu" ni tofauti na huyu mama.Kipala (majadiliano) 14:20, 21 Julai 2019 (UTC)[jibu]

Mtumiaji: Saidi lihuwi alikopi matini ya Kishawishi na kuipakia hapa tena kama makala yake mpya. Alifanya vile kwa makala mengine. Nilimwonya. Kipala (majadiliano) 15:35, 21 Julai 2019 (UTC)[jibu]

Mtumiaji: Saidi lihuwi alikopi matini ya Mapendo ya kiuchumba na kuipakia hapa tena kama makala yake mpya. Alifanya vile kwa makala mengine. Nilimwonya.Kipala (majadiliano) 15:39, 21 Julai 2019 (UTC)[jibu]

Mada inaweza kuwa na maana. Kwa bahati mbaya maelezo si sahihi, hayaeleweki, hayaleti picha za aina mbalimbali za injini za ndege na pia yanajaa makosa ya lugha. Ama iandikwe upya au kufutwa, isibaki jinsi ilivyo.Kipala (majadiliano) 21:07, 4 Agosti 2019 (UTC)[jibu]

Basi nimeinyosha, bado inahitaji kupanushwa. Kipala (majadiliano) 10:08, 7 Agosti 2019 (UTC)[jibu]

Kama hakuna uthibitisho wa ukweli wa melezo na umaarufu wa mhusika, basi ifutwe. Kati ya blogu zinazotajwa siwezi kufungua yoyote- Kipala (majadiliano) 22:13, 16 Agosti 2019 (UTC)[jibu]


Kihariri oneshi IMEFUTWA[hariri chanzo]

Makala haieleweki. Kichwa hakina uhusiano na maudhui. Halafu hakuna daili kwamba mtu anayejadiliwa ana umaarufu wowote kwa kupokelewa katika kamusi elezo. Hakuna vyanzo wala ushuhuda wowote. Ifutwe.Kipala (majadiliano) 04:35, 6 Oktoba 2019 (UTC)[jibu]

Makala haifai. Kwanza haielezi kitu kuhusu mifumo ya kupanga wachezaji, ila inaongea kiefu kiasi kuhusu umuhimu kuwa na mfumo fulani. Pili lugha si nzuri ("sika" kwenye sentensi ya kwanza), tatu hakuna chanzo chochote, wala interwiki. Kama ingekuwa na habari ya maana ningesaidia, hivyo ifutwe tu. 10:15, 18 Oktoba 2019 (UTC)

mwanzo makala hii haikua na vyanzo kabisa ila tayari naona vimewekwa, chapisho la kwanza lilikua ni kama utangulizi wa makala hii, sidhani kama kuna uhitaji wa kuifuta ila kuongezwa kinachokosekana,
kuhusu makosa ya kiuandishi nahisi huwa yanatokea kwa mtu yoyote, ni jukumu letu sisi kama wahariri kubatilisha makosa hayo tukiyaona.--Innocent Massawe (majadiliano) 12:48, 18 Oktoba 2019 (UTC)[jibu]
Vyanzo vimeingizwa, pamoja na maelezo kuhusu mifumo kadhaa. Bado tahajia ni mbaya sana, maelezo yanaweza kuboreshwa,hakuna interwiki. Hata hivyo, inaweza kubaki paoja na ilani ya umbo. Namshauri mchangiaji kutangulia kutunga makala kwenye nafasi yake binafsi (kama: Mtumiaji:Innocent Massawe/Mfumo katika soka) halafu kuipeleka kwenye nafasi ya makala baada kumaliza kazi. Kuweka sehemu ndogo zisizoeleweka kutaleta pendekezo la kufuta. Nampongeza Innocent kwa kujibu hapa badala ya kukaa kimya tu jinsi wanavyofanya wengi walio wachangiaji wapya!IBAKI Kipala (majadiliano) 07:00, 21 Oktoba 2019 (UTC)[jibu]

Pawaga ni tarafa, si kata. Tazama ukurasa wa majadiliano kwa sababu za kuifuta. Kipala (majadiliano) 18:59, 13 Desemba 2019 (UTC