Injini ya ndege

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Injini ya ndege aina ya Rolls-Royce Merlin ikiwa imefungwa katika ndege ya Avro York.

Injini ya ndege ni kifaa kinachosukuma eropleni katika urukaji wake.

Kimsingi kuna aina mbili za injini zinazotumiwa

  • injini za pistoni inayoendesha parapela
  • injini za tabo zinazotoa gesi kwa kasi kubwa, ni nguvu ya msukumo inayoendesha ndege yote.
  • injini zinazounganisha tabo na parapela

Mara chache kuna majaribio ya kutumia injini za umeme au za roketi.