Majadiliano ya mtumiaji:Innocent Massawe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Twamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo - hata kuitafsiri kutoka katika Wikipedia kwa lugha nyingine. Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wa sanduku la mchanga. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike pekee kwenye ukurasa wako wa mtumiaji baada ya kufungua akaunti. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho. Ujue miiko: usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje wala matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo). Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!

Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non speaker better first communicate with one of our admins who will advise you. You find them at Wikipedia:Wakabidhi. And btw: NEVER post computer translated texts (like google-translate, mediawiki Content Translation etc.) nor copied texts/images from other webs to this site! And do not use links to commercial pages. As a newcomer we advise that you register your email which will not be visible to others but it allows to contact you, which often is helpful in case of problems.

Hongera kwa michango yako ya kusahihisha vizuri Kiswahili cha makala mbalimbali. Kuhusu shule za Tanzania, sijui kama zote zina sifa za kustahili kuwa na ukurasa katika kamusi elezo hii. Ngoja tujadiliane kabla hujaendelea na kutunga kurasa za namna hiyo. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:41, 21 Agosti 2019 (UTC)
Naomba tena usubiri jibu la Kipala tusije tukafuta kurasa zako ukawa umefanya kazi bure. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:52, 21 Agosti 2019 (UTC)
Kuhusu shule nashauri tusipokee zote. Naona hapa tufuate mashariti ya kimsingi ya umaarufu, kama vile Wikipedia:Umaarufu#Kanuni_ya_kimsingi_kuhusu_umaarufu_kwenye_Wikipedia: Mada (au mtu) inastahili makala kama masharti matatu yanatimizwa:
  • imeshajadiliwa katika jamii kwa kiwango fulani (si mara ya kwanza hapa wikipedia!)
  • katika vyanzo vinavyoweza kutegemewa (si facebook, twita, tovuti ya binafsi tu)
  • tena vyanzo visivyotungwa na wenyewe (si tovuti ya wenyewe, matangazo yao).
Maana kama hatuna ushuhuda nje ya facebook au tovuti ya wenyewe au kutajwa kwa jina tu katika orodha fulani - hatuna umaarufu wa kutosha. Nashauri usiendelee kuunda makala hizi pasipo na ushuhuda imara zaidi. Kipala (majadiliano) 18:21, 21 Agosti 2019 (UTC)
Ndugu, hongera kwa michango yako, ila usipende kufuta yaliyoandikwa tayari, bali uyaongezee. Kwa mfano katika ukurasa "Golikipa", pamoja na mengine, umefuta "jamii" upande wachini. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:25, 10 Oktoba 2019 (UTC)