Wikipedia:Email

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mawasiliano kwa barua pepe kati yako mwenyewe na watumiaji wengine wa wikipedia ni chaguo unaloweza kuruhusu au la.

Mtumiaji anayetuma barua pepe ataonekana kwa jina la mtumiaji na pia kwa anwani ya email aliyoandikisha hapa wikipedia.

Wakati wa kuandika hujui anwani ya mpokeaji. Unaweza kutuma barua kwa hao pekee walioruhusu njia hii.

Kuwasha email kupitia wikipedia[hariri chanzo]

Nenda kwa "Mapendekezo" hapu juu kwenye ukurasa wako.

  • Baada ya chaguo za lugha na sahihi utaona "Hitiari za barua pepe".
  • Hapo unaweza kuruhusu "Wezesha barua pepe toka kwa watumiaji wengine" pamoja na mwengine.

Ukibofya sehemu hii mstari mpya utatokea upande wa kushoto wa ukurasa wako wa mtumiaji

  • "Email this user"

Basi wengine wanaweza kukuandikia email bila kuona anwani yako.