Pawaga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Pawaga ni tarafa iliyopo katika wilaya ya Iringa vijijini, mkoa wa Iringa. Inaundwa na kata za Ilolo Mpya, Itunundu, Mboliboli na Mlenge.

Ni sehemu ya chini kabisa katika mkoa huo, kwenye kimo cha mita 700 juu ya usawa wa bahari. Kwa sababu hiyo eneo hilo ni tofauti sana na sehemu nyingine za Nyanda za Juu za Kusini Tanzania. Kwanza kuna joto, halafu ukame.

Kwa upande wa Kaskazini imepakana na kijiji cha Makuka (kata ya Izazi), upande wa mashariki imepakana na Idodi, upande wa magharibi imepakana na Ipwasi (kata ya Mlowa) na kwa kiasi kikubwa imepakana na hifadhi ya Ruaha mpaka kusini. Kitovu cha hifadhi hiyo ni Msembe.

Zao kuu la wakazi wa Pawaga ni mpunga unaosifika kwa utamu wake. Unalimwa kwenye mto Ruaha ambao katika sehemu hiyo una muungano wa Ruaha ya Iringa na Ruaha ya Usangu, unaoandaa bwawa la Mtera ambalo linapatikana mbele kidogo kutokana na lambo lililopo mpakani mwa Mkoa wa Iringa na Mkoa wa Dodoma. Kwa kuvuka mto Ruaha unaweza kuingia mkoa wa Singida.

Pawaga ni eneo zuri kwa ufugaji kutokana na hali ya hewa ya joto.

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Iringa bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Pawaga kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.