Gaston Ngailo
Makala haina vyanzo vya kutosha
Makala (au sehemu ifuatayo ya makala) inatoa habari bila kuonyesha vyanzo au uthibitisho wowote.
|
Makala hii inahusu mada au mtu asiyejulikana sana. Kuna mashaka kama mada inastahili kuwa na makala katika kamusi. Onyo hili linaweza kuwekwa pia kama makala haionyeshi umaarufu, hata kama upo.
Watumiaji wanaombwa kushiriki katika majadiliano kama makala hii inafaa kubaki au la. Tazama:Wikipedia:Umaarufu
Unaweza kuondoa kigezo hiki kama majadiliano yametokea na washiriki walipatana.
'
Gaston Jackson Ngailo (alizaliwa Maposeni, Peramiho, 20 Aprili 1990) ni mjasiriamali na mfanyabiashara kutoka Tanzania.
Pia Gaston ni mkurugenzi mkuu na mwanzilishi wa kampuni ya GETVALUE, duka la vitabu vya aina anuwai kupitia mkondoni, ambalo pia hutoa huduma za uuzaji na usambazaji wa bidhaa za kidijitali mtandaoni.
Maisha ya awali
Gaston alizaliwa katika Hospitali ya Peramiho tarehe 20 Aprili 1990 majira ya saa kumi na moja jioni katika kijiji cha Maposeni. Amezaliwa katika familia ya watoto watano. Wadogo zake ni pamoja na Neema Jackson Ngailo, Jenipher Jackson Ngailo, Rehema Jackson Ngailo na Jenister Jackson Ngailo. Akaja kusoma katika shule ya msingi Kiwira iliyoko wilayani Rungwe kata ya Kiwira. Huku sekondari akisomea katika shule ya Sekondari ya Kamene iliyopo Tabata Kimanga. Sekondari elimujuu alisoma Tusiime Iliyopo Tabata Sanene.
Baadaye akaendelea na elimu ya chuo ambapo alitua katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (The Institute Of Finance Management)IFM. Akiwa hapo alipopata shahada ya usimamizi wa fedha. Pia akaenda kusomea utaalamu wa mambo ya benki na fedha katika taasisi na bodi ya Mabenki ya Tanzania (Tanzania Institute Of Bankers)TIOB.
Kazi
Pamoja na kazi ya ujasiriamali, Gaston pia ni mwandishi wa vitabu na mkufunzi wa mambo ya fedha na elimu ya uanzishaji wa biashara. Ameshaandika kitabu chake cha kwanza kiitwacho Why I Hate Being An Employee. Ambacho kipo katika lugha ya Kiingereza pekee. Pamoja na kusomea mambo ya benki, Gaston amekuwa akipendelea sana masuala ya teknolojia. Hivyo akjikuta akiamua kujisomea mwenyewe kuhusu mambo ya teknolojia.
Kwakua alikuwa hapendi kuajiriwa, pindi alipomaliza chuo tu akaamua kuanzisha taasisi yake yeye mwenyewe iitwayo GETVALUE ambayo alianza kuifanyia kazi mwaka 2013 na kuja kuirasimishwa mwaka 2017 na baadaye kufanikiwa kuzinduliwa tarehe 15 Mei 2020.
GetValue
Gaston alianza kufanyia kazi wazo la GETVALUE tangu mwaka 2013 akiwa chuo mwaka wake wa mwisho. Kwasababu alikuwa hataki kuajiriwa, alipata wazo la kuandika kitabu chake kikielezea kwanini hataki kuajiriwa. Ni mawazo yake kuwa huenda kuna watu wengine ambao hawataki kuajiriwa na hivyo kwa yeye kuandika hicho kitabu ingeweza kumsaidia kufikisha elimu, ujuzi na maarifa ya kama mtu anachukiwa kuajiriwa basi kupitia hicho kitabu atapata kujua namna ya nini cha kufanya ili aweze kuishi vizuri bila kuwa mwajiriwa.
Wakati amepata wazo la kuandika kitabu, kwakuwa alikuwa mgeni kabisa kwenye tasnia ya uandishi alilazimika kutafuta mwalimu ambaye angeweza kumfundisha namna nzuri ya kuandika kitabu na njia ya kukiuza. Hivyo alijiunga na mafunzo ya uandishi ambayo yalikuwa yanapatikana mtandaoni.
Alipomaliza kuchukua hayo mafunzo aliweza kuandika kitabu chake cha kwanza kiitwacho “Why I Hate Being An Employee”. Alipokuwa anataka kuanza kuuza kitabu chake hapo ndipo wazo la GETVALUE lilipomjia. Maana alihangaika sana kutafuta mtandao nzuri utakao mfaa kuuza kitabu chake mtandaoni lakini alikosa. Sio kwa maana hakukuwa na mitandao ya kuuza vitabu bali ni kulikuwa hakuna mtandao ambao aliona unafaa kwa yeye kuuza kitabu chake. Hivyo Gaston kwasababu hapo awali tayari alikuwa ameshajifunza kutengeneza mifumo ya kitehama alichukua maamuzi ya kujitengenezea mtandao wake binafsi ambao atatumia kuuza kitabu chake. Wakati alipomaliza kutengeneza mtandao wake akaanza kuuza kitabu chake.
Lakini kitu cha ajabu ni kwamba kila mwandishi aliyekuwa anaona anacho kifanya Gaston na mtandao wake wa kuuza kitabu chake alipenda naye kufanya vile vile. Ndipo Gaston alipogundua kuwa kumbe kuna uhitaji mkubwa sana wa mfumo kama wake. Hivyo ilipofika mwaka 2016 ndipo alipo amua kuanza rasmi kutengeneza mfumo mpya ambao sasa utawezesha sio yeye tu kuuza kitabu chake bali utawezesha hata waandishi wengine wa kitanzania na nje ya tanzania kuweza kuuza vitabu vyao ndani ya tanzania na nje ya tanzania pia.
Ilipofika mwaka 2017 kwasababu Gaston alitaka kuifanya hii kama biashara rasmi aliweza kusajiri kampuni yake kwa jina la GETVALUE ambapo alipata cheti cha usajiri wa GETVALUE tarehe 7 Desemba, 2017 na kuzinduliwa rasmi sokoni mwaka 2020. Kwasababu ya hatua ya tehama iliyokuwepo kipindi hicho na mahitaji ya GETVALUE kuwa makubwa sana Ilimchukua Gaston takribani miaka mitano kutengeneza mfumo wa GETVALUE mpaka kuhakikisha unafaa kwenda sokoni kwa ajili ya mtumiaji wa mwisho.