Nenda kwa yaliyomo

Wikipedia:Makala kwa ufutaji/Nyaraka 6

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Hii ni nyaraka ya makala Wikipedia:Makala kwa ufutaji ya mwaka 2020 na 2021.

Kwa nyaraka za zamani zaidi angalia hapa.

Ukurasa huu unaonyesha maudhui yote ya ukurasa ya miaka 2020 na 2021. Makala ambazo hazikuamuliwa zinarudia kwenye ukurasa kuu.

Makala zilizopelekwa hapa 2020

[hariri chanzo]

Makala ambazo hazikuamuliwa katika miaka ya nyuma

[hariri chanzo]

Sina uhakika juu ya hali ya hakimiliki katika Tanzania kuhusu matini ya nyimbo. Nashauri mtu ajaribu kupata kibali chake, au kutoa maelezo hapo. Kipala (majadiliano) 16:38, 7 Mei 2015 (UTC)[jibu]

Tuhamishe wikichanzo? Bado sijui mambo ya hakimilikiKipala (majadiliano)

Inawezekana ya kwamba makala hii ni kweli kuhusu mwandishi anayestahili kutajwa katika wikipedia. Lakini hakuna ushuhuda wowote, mfano kutaja jina la kitabu pamoja kampuni ya mchapishaji na mwaka wa kutolewa n.k. Pia kuna matini nyingi isiyo na maana yoyote (mfano majina ya marafiki, madai kuhusu uwezo wake akiwa mwanafunzi wa shule; maelezo ya kurudia eti alitunga "makala mbalimbali"). Haionekani kutokana na makala kama huyu ni kweli mtu aliyepata kiwango fulani ya umaarufu (aliwahi kutajwa katika gazeti au jarida au kitabu fulani?). Inaonekana zaidi kama mchango iliyoandikwa ama na mwenyewe au na rafiki ili aonekana katika intaneti. Pamoja na hayo matumizi ya HERUFI KUBWA hayalingani na utaratibu wa wikipedia. Kama hakuna masahihisho tunapaswa kufuta mchango huu. Linganisha Wikipedia:Mwongozo (Kutaja vyanzo), Wikipedia:Umaarufu. Kipala (majadiliano) 13:40, 25 Agosti 2018 (UTC)[jibu]

Narudia pendekezo ifutwe. Inaonekana kama makala ya mtu kujitangaza mwenyewe au kama makala ambako mtu anamtangaza mwenzake. Hali halisi kuna vitabu 2 vinavyoonyeshwa na mwandishi huyu na amazon inaonyesha alivichapisha mwenyewe (selfpublished) ambayo haitoshi kwa makala ya hapa. Kipala (majadiliano) 15:18, 21 Julai 2019 (UTC)[jibu]

Tatizo la makala hizi zote ni swali la ushuhuda na umaarufu. Nje ya tovuti ya wenyewe hakuna ushuhuda. Tuelewane kuhusu makala za shule. Kipala (majadiliano) 19:10, 21 Agosti 2019 (UTC)[jibu]

Baada ya majadiliano ya awali (wapi?) nadhani tulikuwa pamoja tusikubali makala za shule za kawaida, kama hakuna ushuhuda wa nje ya wenyewe, mfano shule ya kihistoria. Kwa hiyo naona ifutwe. Kipala (majadiliano) 20:01, 10 Februari 2020 (UTC)[jibu]

Kiswahili kibaya, hakuna vyanzo, haionekani kwa nini makala iwepo kwetu. Ifutwe. Kipala (majadiliano) 07:17, 18 Novemba 2019 (UTC)[jibu]

Makala haieleweki. Haionyeshi sababu yoyote kwa nini mtu huyu awe na makala, pia haionyeshi alifanya nii hasa, alikuwa na mafanikio gani. Nahisi kuna habari zaidi lakini hazionyeshwi. Tena Kiswahili chake kina dalili za tafsiri ya kompyuta. Ilhali makala nyingi zimetokea wakati wa Novemba kwa lugha za Kiafrika, inaonekana ni mchezo wa watu wanaotaka kusambaza jina hili katika wiki nyingi, ila tu imeandaliwa vibaya. Kipala (majadiliano) 06:23, 6 Desemba 2019 (UTC)[jibu]

This is not an advertisement article and is not only in African languages but also in a few European languages. The article is about a brave young man who saved the local community. He was one of the youngest secretaries of Communist Youth in the former Yugoslavia. Take it hier.Procuratorac (majadiliano) 11:32, 9 Januari 2020 (UTC)[jibu]

Makala zilizowahi kupata alama ya "futa" bila kuletwa hapa

[hariri chanzo]

(zilipatikana wakati wa kukagua orodha ya "Viungo viungavyo ukurasa huu" kwa ukurasa wa "Kigezo:Futa", tarehe 18-03-2020)

  1. Alfagems Secondary School
  2. Alien (kiumbe)
  3. Amini Cishugi
  4. Amini Cishugi
  5. DJ LYTMAS
  6. Emmaus Shule ya Biblia
  7. JamiiForums
  8. Kigezo:Ambox ‎ IBAKI, inaonekana kwa sababu inataja "Delete" ndani yake
  9. Kigezo:Ambox/hati
  10. Kisoli (ukoo)
  11. Lango:Asia
  12. Majadiliano ya mtumiaji:Pesa Day
  13. Maneno Lusasi
  14. Mbonea
  15. Mtumiaji:AliceShine
  16. Mtumiaji:Jabir Mking'imle
  17. Mtumiaji:Kipala/Archive 8 ‎
  18. Mtumiaji:Legobot/Wikidata/eowiki
  19. Mtumiaji:Mholanzi
  20. Mtumiaji:Ramad Jumanne
  21. Mtumiaji:Silverlombard
  22. Mtumiaji:Tegel
  23. Mtumiaji:Veracious/Draft
  24. Nairobi fly
  25. Orodha ya miji ya Kiswahili
  26. Faili:Elizabeth Michael2016.jpg
  27. Shinz Stanz
  28. Shule za sekondari
  29. Stopselcub
  30. Tumaini Lenye Baraka
  31. Ukaguzi wa masoko
  32. Webico
  33. Wikipedia:Istilahi za wiki/Kiingereza

Makala zilizoletwa hapa mwaka 2020

[hariri chanzo]

Alijiandikisha kitambo, aliamua leo kutangaza biashara.Tumpe siku kadhaa kwa marekebisho ,menginevyo tumfute. Kipala (majadiliano) 16:17, 6 Januari 2020 (UTC)[jibu]

Isahihishwe au kufutwa. Kipala (majadiliano) 06:58, 8 Februari 2020 (UTC)[jibu]

Itasahihishwa. Kipala (majadiliano) 06:59, 8 Februari 2020 (UTC)[jibu]

Makala haielezi inahusu nini; Kiswahili ni kibaya na tahajia ya duni. Sijui kama tovuti inyojadiliwa inastahili makala lakini hakika hii si makala inayofaa. Ifutwe. Kipala (majadiliano) 19:49, 10 Februari 2020 (UTC)[jibu]

Akaunti hii imefunguliwa na mtumiaji majadiliano ya mtumiaji:Maulidi jumanne. Ilhali kwa kawaida hatukubali akaunti ya pili ya mtumiaji yeye yule, nimeweka alama ya "futa" hadi kuona maelezo, menginevyo akaunti hii ifutwe karibuni na jina libanwe na kuhariri.Kipala (majadiliano) 07:03, 4 Machi 2020 (UTC)[jibu]

Matini yote ya makala imenakiliwa kutoka sehemu nyingine ya intaneti. Ninakuta manen yaleyale hapa www.facebook.com › sw.islamkingdom, www.pinterest.es, www.al-feqh.com na www.kenyatalk.com. Kunakili matini na kuibandika hapa ni marufuku kabisa kwenye wikipedia. Makala inatumia pia lugha ya Kihispania kutokana na kunakiliwa. Ama itasahihishwa haraka sana au kufutwa.Kipala (majadiliano) 20:18, 10 Machi 2020 (UTC)[jibu]

Matini imenakiliwa kutoka https://www.al-feqh.com/sw/swala-ya-kuomba-mvua. Ifutwe, mwandishi ni mgeni lakini hasomu au hajibu ujumbe kwenye ukurasa wake wa majadiliano. Kipala (majadiliano) 14:30, 14 Machi 2020 (UTC)[jibu]

Kuna dalili hii ni akaunti maradufu (linganisha Majadiliano ya mtumiaji:Hamid ibn juma iliyoanzishwa pamoja nayo), mwenyewe ajieleze au tutafuta akaunti ya mtumiaji. Kipala (majadiliano) 11:51, 15 Machi 2020 (UTC)[jibu]

Mwembamba IMEBADILISHWA

[hariri chanzo]

"Mwembamba" ni neno ambalo halitaji mwili pekee, kitu chochote kinaweza kuwa chembamba au pana. Istilahi haifai kwa makala ya wikipedia, ipelekwe https://sw.wiktionary.org na kufutwa hapa. Pia tahajia ni vibaya mno Kipala (majadiliano) 07:27, 18 Machi 2020 (UTC)[jibu]

Ifutwe, matini imenakiliwa hapa https://www.al-feqh.com/sw/utwhara-na-aina-za-maji. Kipala (majadiliano) 18:25, 20 Machi 2020 (UTC)[jibu]

Udhu IMEBORESHWA

[hariri chanzo]

Mchangiaji alinakili hapa https://www.al-feqh.com/sw/kutawadha. Nimemwonya, nilimbana kwa siku tatu, hajibu na anaendelea kuleta matini kutoka al-feqh.com. Nambana sasa wiki 1, lakini sijui kama anaitambua. Kipala (majadiliano) 11:03, 26 Machi 2020 (UTC)[jibu]

Mchangiaji amenakili matini kutoka https://www.al-feqh.com/sw/hukumu-za-swala. Nambana sasa wiki 1, lakini sijui kama anaitambua. Kipala (majadiliano) 11:06, 26 Machi 2020 (UTC)[jibu]

Mchangiaji amenakili matini kutoka https://www.al-feqh.com/sw/swala-ya-kuomba-mvua. Kipala (majadiliano) 11:14, 26 Machi 2020 (UTC)[jibu]

Makala haifuati fomati, haina ushahidi wowote kuhusu umaarufu au ukweli wa habari, hakuan jamii wala interwiki. Isahihishwe katika wiki 1 au kufutwa. Kipala (majadiliano) 17:20, 1 Aprili 2020 (UTC)[jibu]

Chanzo kimoja kimeongezwa, angalau tunajua yupo mwalimu kwenye barefoot college bila habari zaidi, lakini chanzo kingine hakielezi kitu. Habari karibu zote ni bila ushahidi, umaarufu haueleweki. Kipala (majadiliano) 19:22, 10 Aprili 2020 (UTC)[jibu]

Makala haina chanzo na marejeo na inaeleza kuhusu takwimu bila marejeo. Czeus25 Masele (majadiliano) 15:44, 5 Aprili 2020 (UTC)[jibu]

Hadi sasa tulivumilia habari za kimahali (kama vile habari kuhusu kata na pia jamii za Tanzania kama utamaduni wa makabila, lakini si juu ya ngazi ya kata) hata bila ushahidi. Maana hali halisi kwa maeneo yale karibu yote hakuna vyanzo vya kimaandishi. Upande wa wakabidhi tuliona tufanya hivyo isipokuwa kama nafasi hiyo inatumiwa kukashifu watu wengine au kukazia sifa za watu walio hai. Kwa mtazamo huu naona inaweza kubaki. Tafadhali wengine wachangieKipala (majadiliano) 17:03, 5 Aprili 2020 (UTC)[jibu]

Makala imeandikwa zaidi kama insha, si makala ya kamusi elezo. Umbo haulingani na kawaida yetu. Tena sehemu "Sayansi imechunguza viumbehai waliopo ..." imenakiliwa neno kwa neno kutoka https://napradck.blogspot.com/2017/11/binadamu-or-human.html. Makala haitoshelezi masharti ya kamusi elezo. Isahihishwe haraka au kufutwa. Kipala (majadiliano) 22:53, 5 Aprili 2020 (UTC)[jibu]

Ni kinyume: blogu ilinakili sehemu hiyo kutoka kwetu, kwa kuwa niliiandika mwenyewe kutoka kichwani. Kuhusu umbo, tutalirekebisha. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:00, 9 Aprili 2020 (UTC)[jibu]

Makala haielezi mhusika ni mteule (maana yake??) wa aina gani, wala haielezi lile baraza la muungano (wa nini?) la vijana ni kitu gani. Pamoja na kutoeleweka (isipokuwa kwa watu wanaojua tayari "mteule wa baraza" ni nini) hakuna chanzo maana linkedin ni sawa na facebook, ni tovuti am bako kila mtu anajitangazua. Makala isahihishwe; kama la heri ifutwe. Kipala (majadiliano) 16:49, 8 Aprili 2020 (UTC)[jibu]

Makala haina fomati, wala vyanzo, wala jamii, wala interwiki. Itafutwa usiporekebisha.Kipala (majadiliano) 17:26, 8 Aprili 2020 (UTC)[jibu]

Makala haina vyanzo. Itafutwa isiporekebishwa. Czeus25 Masele (majadiliano) 04:42, 12 Aprili 2020 (UTC)[jibu]

Makala imenakiliwa moja kwa moja kutoka twita hapa au kutoka hapa, ambayo hairuhusiwi. Pendekezo lilitoka kwa mtumiaji:Riccardo Riccioni, kwa hiyo ninafuta sasa.Kipala (majadiliano) 11:58, 23 Aprili 2020 (UTC)[jibu]

TomKat IMEBADILISHWA

[hariri chanzo]

Ukurasa huu unahusu mapenzi yaliyokwishaisha kati ya wasanii wawili. Ifutwe. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:52, 7 Mei 2020 (UTC)[jibu]

Ukurasa unasema tu habari moja kwa ufupi. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:34, 11 Mei 2020 (UTC)[jibu]

Ukurasa una umbo la katiba ya chama hicho, si la kamusi elezo. Usiporekebishwa sana, ufutwe. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:15, 13 Mei 2020 (UTC)[jibu]

Makala haielezi mada yake, haifuati fomati ya kamusi elezo na haionyeshi chanzo chochote. Inaonekana ni kama matangazo ya wenyewe. Kipala (majadiliano) 05:03, 5 Juni 2020 (UTC)[jibu]

Makala inahusu mtu asiyejulikana na haifuati fomati. Ifutwe. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:37, 5 Juni 2020 (UTC)[jibu]

Makala haina vyanzo; haionekani mhusika ana umaarufu wowote. Inaonekana kama matini iliyotungwa na mhusika mwenyewe au alimwomba rafiki kutunga makala na kumpeleka wikipedia. Ifutwe. Kipala (majadiliano) 17:28, 8 Juni 2020 (UTC)[jibu]

Matini yote ni Kiingereza, hakuna vyanzo vya kuthibitisha habari. Sijafuta mara moja ili tumpe mchangiaji nafasi ya kubadilisha. Kipala (majadiliano) 06:18, 20 Juni 2020 (UTC)[jibu]

Makala haieleweki. Ifutwe. Kipala (majadiliano) 05:32, 23 Juni 2020 (UTC)[jibu]

Bweri Secondary school IMEELEKEZWA KWENDA KATA YAKE

[hariri chanzo]

Kwa kawaida shule ya sekondari haina umaarufu wa kutosha ili kustahili makala. Tena makala haina ushuhuda wowote. Kipala (majadiliano) 18:33, 24 Juni 2020 (UTC)[jibu]

Nadharia ya Kiswahili KICHWA KIMEREKEBISHWA

[hariri chanzo]

Jambo linalojadiliwa linafaa kutajwa katika makala ya "Kiswahili". Jina la makala halieleweki kirahisi, maana mchangiaji alimaanisha "nadharia kuhusu asili ya Kiswahili", ambayo ni tofauti na "Nadharia ya Kiswahili". Kwa makala ya pekee ingefaa kuonyesha vyanzo na pia kueleza hizo nadharia tofauti, ambayo haitokei katika makala hii. Kipala (majadiliano) 07:13, 10 Julai 2020 (UTC)[jibu]

Makala ina dalili ya kutungwa na mwenyewe. Jina la mwazilishaji linalingana na lemma. Hakuna vyanzo isipokuwa kurasa ambako watu wanajitangaza wenyewe. Ifutwe. Kipala (majadiliano) 08:56, 6 Agosti 2020 (UTC)[jibu]

Msisimko IMEBORESHWA

[hariri chanzo]

Maelezo ni mafupi na si sahihi. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:38, 7 Agosti 2020 (UTC)[jibu]

Ni kwaya ya Kanisa tu, si maarufu. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:11, 17 Agosti 2020 (UTC)[jibu]

Hakuna ushahidi wote, jina kama ni kweli si jina kamili. Ifutwe. Kipala (majadiliano) 21:24, 17 Agosti 2020 (UTC)[jibu]

Makala haifai jinsi ilivyo. Haina habari za maudhui ya kitabu bali tu maoni ya mtungaji kuhusu sababu za kupigwa marufuku kwake zamani. Haielezi kwamba baadaye ilikuwa kitabu kilchotumiwa shuleni Tanzania na Kenya. Haina vyanzo vyovyote. Isahihishwe haraka au heri kufutwa. Kipala (majadiliano) 16:31, 23 Agosti 2020 (UTC)[jibu]

Makala ama ibadilishwe au kufutwa. Habari zake si sahihi. Hii ni kampuni ya Kichina (si ya Kitanzania), tena siwezi kukuta taarifa juu yake. Vyanzo vyote ni vya wenyewe. Tovuti yao ina Kiingereza kibaya kiasi kwamba makala inadai kampuni hii "inasafirisha karibu asilimia tisini ya vifaa kote ulimwenguni" ambayo si kweli hata kidogo. Hapa iko swali la umaarufu. wanfanyakazi 2000 kwa kampuni ya kimataifa si namba kubwa kweli. Sijui kama hii ni jaribio la kutangaza kampuni au makala tu ambayo mada yke haikuchunguliwa. Kipala (majadiliano) 08:14, 2 Septemba 2020 (UTC)[jibu]

Mtumiaji:Kipala : SILENT OCEAN TANZANIA. Ni Kampuni ya kitanzania inayomilikiwa na mtanzania na ina makao yake makuu Dar es salaam, Lumumba. Ni kampuni ambayo ilianzishwa mwaka 2006 na ikiwa na jina Kilimanjaro cargo, ikiwa chini ya Usimamizi wa Home shopping center. Na tovuti ya silent ocean iko sawa huwenda umeona tovuti tofauti, lakini pia wafanyakazi 2000 nadhani ni namna ya uwandishi tu, ambapo ni lazima ifanyiwe maboresho. yote ya yote nashukuru sana kwa kujali, kuhusu makala hii na ku hoji kwa kina. molee4real (majadiliano)
Basi usahihishe ili ieleweke. HAkika haisafirishi asilima 90 wala ya bidhaa duniani wala za Tanzania, kitengo cha Tanzania haina wafanakazi 2000, bado sioni chanzo nje ya hao wenyewe. Una siku kadhaa. Kipala (majadiliano) 12:26, 8 Septemba 2020 (UTC)[jibu]
Nimekwisha fanya kama ulivyo agiza ku sahahihisha makosa, na pia nimepata dondoo chache zenye uhakika juu ya Kampuni hiyo, Ambapo dondoo hizo zimenisaidia kusahihisha taarifa kwa usahihi, nakukaribisha kwa mapitio na uhakiki wa mabidiliko hayo. molee4real (majadiliano)
Bado naona heri makala ifutwe. Nikiangalia tanbihi, hazithebitishi habari ndani ya makala. Kufuatana na chanzo 2, "Silent Ocean Limited is a clearing & Forwarding company based in Guangzhou, China". Kwa hiyo si kampuni ya Kitanzania jinsi inavyodaiwa. Inawezekana kuna tawi la kampuni ya China katika Tanzania iliyoandikishwa pale pia. Idadi ya wafanyakazi haina uthebitisho, kinyume cha maelezo ya makala. Kosa kuu ni: hakuna vyanzo visivyo vya vyenyewe. Lemma hii imeshafutwa kwenye enwiki kama spam, tazama en:User_talk:Molee4real. Hatuna data kabisa, inawezekana ni kampuni ndogo (isiyofaa kupata nafasi hapa). Kipala (majadiliano) 08:50, 14 Septemba 2020 (UTC)[jibu]
Makala imejikita sana kama maelezo ya kibiashara, hivyo naona ifutwe.Czeus25 Masele (majadiliano) 21:56, 14 Septemba 2020 (UTC)[jibu]
Bado hakuna ushahidi wa nje wakuthibitisha maana kwamba hakuna marejeo yenye mashiko, jamiiforums sio marejeo sahihi bado hivo ukurasa ufutwe Olimasy (majadiliano) 05:49, 15 Septemba 2020 (UTC)[jibu]
Imefanyika.--'Muddyb Mwanaharakati' 'Longa' 13:47, 15 Septemba 2020 (UTC)[jibu]

Pendekezo la kufuta makala hii imepelekwa na mtumiaji:Praxidicae akitaja sababu: Cross-wiki spam. Makala iliwekwa na mtumiaji:Molee4real, aliyejaribu kuipeleka pia enwiki ambako lemma imefutwa. Mtumiaji Molee4real alijaribu kuepukana na mchakato wa kufuta pale enwiki alibanwa kwa sababu makala zake kuhusu yule Salah na kampuni ya Silent Ocen zilikuwa nje ya utaratibu. Alijaribu mara kadhaa kurudishwa alikiri "my mistake was to use Wikipedia for advertisement". Hapo nashangaa kidogo akileta mambo yaleyale hapa swwiki. Naona labda mtungaji hajaribu kudanganya bali anashindwa kufanya utathmini wa vyanzo na kutumia mantiki. Chanzo cha pekee kuhusu Salah na kampuni ni "millardyo" (ambayo ni dhaifu!), mengine ni bure kabisa. Millardyo alidai aliajiri Wachina 300, ilhali Molee4real alijaribu kutuambia katika makala ya kampuni kuna wafanyakazi maelfu. Kumtangaza hapa kama mwimbaji kama ametoa wimbo moja pekee?? Inawezekana hii ni mada inayofaa kwa wikipedia lakini bila vyanzo vya kuaminika, afadhali makala zote mbili zifutwe kwa sasa hadi vyanzo vya uhakika vinapatikana. Kipala (majadiliano) 08:50, 14 Septemba 2020 (UTC)[jibu]

Imefanyika.--'Muddyb Mwanaharakati' 'Longa' 13:48, 15 Septemba 2020 (UTC)[jibu]

Isipoongezwa haraka ifutwe. Haina vyanzo, haina habari , haieleweki Kipala (majadiliano) 12:22, 8 Septemba 2020 (UTC)[jibu]

Mwandishi hakutaka kupokea maelekezo, ila kurudisharudisha toleo lake. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:18, 8 Septemba 2020 (UTC)[jibu]

Mtungaji ameandika juu yake mwenyewe, amepokea onyo. Makala ifutwe. Kipala (majadiliano) 07:17, 22 Septemba 2020 (UTC)[jibu]

Aliendelea kutunga kurasa za namna hiyohiyo kujitangaza. Nimezifuta zote. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:29, 22 Septemba 2020 (UTC)[jibu]

Pendekezo la kufuta Makala hii, Makala hii liwahi kufutwa ila mwandishi amekua akirudia makosa yale yale, maelekezo mengi alishapata. Makala imekaa kibiashara na imetumia kurasa ya mitandao ya kijamii na tovuti ya kampuni. Czeus25 Masele (majadiliano) 13:50, 25 Septemba 2020 (UTC)[jibu]

Mwanamalundi IMEELEKEZWA KWENDA UKURASA HUSIKA

[hariri chanzo]

Inaonekana makala hiyo ina matini iliyonakiliwa, mfano [1] ambayo haikubaliki. Hivyo naongeza alama ya kufuta makala hiyo. Kipala (majadiliano) 19:15, 1 Oktoba 2020 (UTC)[jibu]

Makala haina vyanzo vyovyote, lugha yake haieleweki vema, na umbo lake haulingani na masharti ya makala ya kamusi elezo. Ama iandikwe upya pamoja na marejeo au ifutwe. Kipala (majadiliano) 12:59, 4 Oktoba 2020 (UTC)[jibu]

David ameleta makala kadhaa ambazo zote hazionyeshi vyanzo vyovyote, pia havilingani na masharti ya umbo. Hizo ni pamoja na Splitting Adam ‎, Rags, Betty in Newyork, Secret Superstar, Zig na Sharko, Stitches, School of Rock, Starfalls, Aidan Gallagher, PAW Patrol, Danger Force, Nicky, Ricky, Dicky and Dawn, Haunted Hathaways, Transfomers: The Last Knight, Zuchu, Becky Lynch, Sofia the first, Rango (filamu, 2011), Big Time Rush, Kung Fu Panda, Power Rangers Ninja Steel. Sijapitilia kila moja lakini idadi kubwa niliyona haziwezi kubaki kama haziongezwi vyanzo na fomati kusahihishwa. Kipala (majadiliano) 15:15, 25 Oktoba 2020 (UTC)[jibu]

Pia Pj masks. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:16, 3 Novemba 2020 (UTC)[jibu]

ːBado hakuna dalili ya kwamba atazifanyia marekebisho tusubiri muda kidogo labda. Olimasy (majadiliano) 08:59, 16 Novemba 2020 (UTC)[jibu]

Nimejaribu kupitia baadhi ya makala, napendekezwa zifutwe, hazina umaarufu huku. Czeus25 Masele (majadiliano) 08:45, 2 Juni 2021 (UTC)[jibu]
Ukiona vile, basi futa! Kipala (majadiliano) 23:05, 6 Septemba 2021 (UTC)[jibu]

Mankala IMEBORESHWA

[hariri chanzo]

Nimeongeza, si ndefu kama ya kiingereza, lakini nafikiri imetosha kwa sasa. Benson Muite (majadiliano) 17:30, 25 Oktoba 2020 (UTC)[jibu]

Asante, inafaa. Kipala (majadiliano) 07:13, 26 Oktoba 2020 (UTC)[jibu]

World Wrestling Entertainment, Air force one, Ertugrul, Kaan Urgancıoğlu, Burak Özçivit, Keith lee , :Hazina vyanzo, umbo si sanifu; mtungaji yeye yule (mtumiaji:1z beat); zisahihishwe au kufutwa. Kipala (majadiliano) 07:14, 26 Oktoba 2020 (UTC)[jibu]

Haina vyanzo, umbo si sanifu; isahihishwe au kufutwa. Kipala (majadiliano) 13:31, 26 Oktoba 2020 (UTC)[jibu]

Napendekeza ifutwe Aneth 06:50, 27 Oktoba 2020 (UTC)[jibu]

Haina maana wala vyanzo. Kipala (majadiliano) 05:06, 27 Oktoba 2020 (UTC)[jibu]

Naunga mkono ifutwe, hata uandishi sio mzuri Aneth 04:49, 27 Oktoba 2020 (UTC)[jibu]

Kama makala nyingine za siku hizi, haifuati fomati, haina vyanzo. Halafu naona dalili za tafsiri ya kompyuta (Sanduku la ofisi - boxoffice). Isiporekibishwa, ifutwe. Kipala (majadiliano) 13:30, 27 Oktoba 2020 (UTC) Makala hii imetafsiriwa kutoka makala ya Wikipedia ya Kingereza. Makala hii naendelea kuiboresha, nashauri isifutwe. Ebenezer Mlay (Ebenezer Mlay) 08:04, 30 Oktoba 2020 (UTC)[jibu]

Bado haijafanyiwa marekebisho mpaka sasa tangu kutangazwa kufutwa, bado twasubiri. Olimasy (majadiliano) 09:08, 16 Novemba 2020 (UTC)[jibu]
Naona vyanzo viko, nimenyosha lugha ya kompyuta niliyoona, ibaki. Kipala (majadiliano) 12:11, 16 Novemba 2020 (UTC)[jibu]

Naona makala ni jaribio la kusimulia hadithi ya mhusika wa filamu au kitabu fulani, lakini haieleweki. Umbo haulinganoi na kamusi elezo, hakuna marejeo - ifutwe. Kipala (majadiliano) 13:48, 8 Novemba 2020 (UTC)[jibu]

Ifutwe au kuboreshwa. Fomati haijafuatwa, haina vyanzo. Aneth 12:59 11 Novemba 2020 UTC

Haina vyanzo vyovyote. Iboreshwe. Aneth 13:02 11 Novemba 2020 UTC

Frozen 1 IMESAHIHISHWA, IBAKI

[hariri chanzo]

Inahitaji maboresho kufuata mpangilio wa makala za filamu na pia kweka vyanzo. Iboreshwe. Aneth 13:03 11 Novemba 2020 UTC

Makala hizo saba hazieleweki vizuri. Umbo halifanani na makala ya kamusi elezo, vyanzo havitajwi. Zisiporekebishwa, zifutwe. Kipala (majadiliano) 14:47, 8 Novemba 2020 (UTC)[jibu]

==> Napendekeza ifutwe kwa sababu haina vyanzo pia Aneth 1257, 11 Novemba 2020 (UTC)

Lugha mbaya, dhahiri tafsiri ya kompyuta, ifutwe au kusahihishwa. Tena mchango usiofaa kutoka mtumiaji:MrWaxwell. Kipala (majadiliano) 06:04, 11 Novemba 2020 (UTC)[jibu]

Makala haina vyanzo hata kimoja Aneth 07:52, 01 Disemba 2020 (UTC)

Nimeongeza walau viungo vya nje kutoka Wiki ya Kijerumani. Kwa Kiingereza hamna vyanzo, lakini mtu alikuwa muhimu. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:55, 22 Juni 2021 (UTC)[jibu]

Sioni maana ya makala. Maandamano ni jambo la kawaida katika nchi ya kidemokrasia. Makala haina chanzo chochote kuthibitisha chaguo la maanadamano yaliyoteua. Kipala (majadiliano) 21:45, 13 Desemba 2020 (UTC)[jibu]

Makala ni tafsiri mbaya ya kompyuta iliyoleta maudhui yasiyoeleweka. Ilhali mada ina maana, si vibaya kama mhariri anajitolea kuokoa makala. Lakini bila masahihisho heri ifutwe. Kipala (majadiliano) 10:23, 14 Desemba 2020 (UTC)[jibu]


Makala zilizoletwa hapa mwaka 2021

[hariri chanzo]

Je, ni maarufu kweli? --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:13, 3 Januari 2021 (UTC)[jibu]

Je, ni maarufu kweli? --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:13, 3 Januari 2021 (UTC)[jibu]

  • Ibaki Mtu huyu ni maarufu, Mkurugenzi uwekezaji wa kampuni ya Gsm, lakini pia ni mkuu wa uwekezaji na usajiri wa ndani ya timu ya yanga. Pia huyu ndie alijenga jengo la upasuaji la mwananyamala, na msikiti wa Kinondoni. Lakini pia ni mfanya biashara ni mmoja wa wamiliki wa wamiliki wa hotel ya White sand hotel na kupitia uhandisi ndie aliekua mwandisi mkuu wakati wa ujenzi wa uwanja wa Taifa wa mpira. Kwa hivo nin shauri makala hii ibaki na ifanyiwe marekebisho. 4realtz (majadiliano) 08:09, 4 Januari 2021 (UTC)[jibu]

Sioni msingi kubaki na kifungu hiki. Hakuna ushahidi wowote, na kwa mkusanyiko wa maoni ambayo mchangiaji alibahatika kusikia, ni ndefu mno. Tunakosa habari za kimsingi kuhusu kundi hilo, lakini matini ndefu ya udaka kuhusu kundi hili. Ifutwe. Kipala (majadiliano) 19:46, 15 Januari 2021 (UTC)[jibu]

Nadhani ukurasa wote kwa ujumla una marejeo machache sana na unahitaji marekebisho kwenye baadhi ya sehemu. Kipengele kilichopendekezwa kufutwa kina taarifa ambazo zinaweza kua sahishsi ila kinahitaji marejeo.

Aneth David (SLU) (majadiliano) 14:20, 2 Julai 2021 (UTC)[jibu]

Ukipenda kusahihisha, usahihishe. Menginevyo futa, Kipala (majadiliano) 14:55, 2 Julai 2021 (UTC)[jibu]

Makala imeletetwa bila ya kuwa na vyanzo, tunaweza kuitafutia vyanzo kwa ajili ya maboresho zaidi kabla ya kuifuta, asante.

Nimeiboresha kidogo. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 06:48, 15 Aprili 2021 (UTC)[jibu]

Nimesahihisha mwanzo lakini naona makosa yanazidi. Tafsiri ni mbaya, tahajia hata ya kichwa (lemma) si sahihi, matini bado inajaa Kiingereza kisichotafsiriwa. Ama mmoja ahurumie makala na kuwekeza wakati wake, au ifutwe. Kipala (majadiliano) 14:23, 30 Januari 2021 (UTC)[jibu]

Tayari. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:14, 31 Januari 2021 (UTC)[jibu]

Jambo halieleweki. Ni maelezo hafifu mno. Kiswahili chake kina makosa hadi kutoeleweka. Niliangalia makala ya enwiki, hata pale haieleweki kirahisi lakini angalau ukusoaji unaonyeshwa vizuri zaidi. Makala jinsi ilivyo haina faida kutokana na udhaifu wa lugha na udhaifu wa maelezo. Heri ifutwe. Kipala (majadiliano) 18:21, 31 Januari 2021 (UTC)[jibu]

Sehemu ya pili haieleweki. Tafsiri ya kompyuta? Hakuna vyanzo vyovyote. Isiporekibishwa haraka, iende. Kipala (majadiliano) 21:27, 8 Machi 2021 (UTC)[jibu]

Ni ukurasa wa mtumiaji alipoweka matangazo ya kibiashara. Nimemwonya tayari, naipeleka hapa nisisahau onyo. Kipala (majadiliano) 16:48, 13 Machi 2021 (UTC)[jibu]

Rosa hope IMEREKEBISHWA

[hariri chanzo]

Makala haifuati masharti ya fomati inayotakiwa hata kidogo (tahajia, matumizi ya mabano, jamii, interwiki, lugha). Ifutwe. Kipala (majadiliano) 21:49, 13 Aprili 2021 (UTC)[jibu]

Makala haifuati masharti ya fomati inayotakiwa hata kidogo (tahajia, matumizi ya mabano, jamii, interwiki, lugha). Ifutwe. Kipala (majadiliano) 21:51, 13 Aprili 2021 (UTC)[jibu]

Makala haielezi kitu kuhusu filamu hiyo, haionyeshi vyanzo, pia mtungaji alijaribu kuingiza picha kutoka google ambayo ni marufuku. Ifutwe. Kipala (majadiliano) 18:26, 23 Mei 2021 (UTC)[jibu]

Sioni faida ya hii. Ana taja vijiji 18 kati ya 50 au zaidi vilivyopo bila maelezo yoyote na bila chanzo. (Nikiangalia kurasa kadhaa za Orodha ya posta napata Bumilayinga , Ibatu , Ifupira , Ifwagi , Igombavanu , Igowole , Ikwega , Isalavanu , Itimbo , Itona , Kibao , Kihanga , Kikombo , Kinyanambo , Kisada , Kisasa , Kitelewasi , Kitiru , Lufuna , Lwing'ulo , Maduma , Mkalala , Mninga , Mninga , Mpanga , Mwitikilwa , Njojo , Nyololo , Nyololo Njiapanda , Nzivi , Rungemba , Sao Hill , Sawala , Ugute , Ulole, na hivi si vyote! Ifutwe. Kipala (majadiliano) 19:01, 23 Mei 2021 (UTC)[jibu]

Nikichungulia naona kuna mambo mawili tofauti 1) kitabu cha "The Kill Order" cha James Dashner (si James Dishner), soma undani hapa: en:The_Kill_Order kuhusu majanga asilia kama milipuko kwenye Jua, tsunami na jitihada ya kundi la watu kuokoa maisha yao katika hali ya fujo inayofuata baada ya majanga hayo

2) filamu ya "Kill order" (soma habari zake hapa: https://www.shockya.com/news/2018/02/21/interview-james-mark-talks-kill-order-exclusive/) kuhusu kijana mwenye vipaji vya ajabu vya kupigania akijitetea dhidi ya watu wabaya (ila bila swali la majanga asilia..).

ambayo ni vitu viwili tofauti kabisa. Sijui kama mchangiaji alijaribu kuunganisha yote mawili? Tumpe wiki 2,3 kusahihisha, baadaye tuone au tufute. Kipala (majadiliano) 19:55, 23 Mei 2021 (UTC)[jibu]

Sioni maana. Kipala (majadiliano) 20:08, 23 Mei 2021 (UTC)[jibu]

Tafsiri ya kompyuta mbaya mno. Ifutwe. Sioni inafaa kusahihishwa, lakini kama yeyote anapenda, basi. Kipala (majadiliano) 15:04, 24 Mei 2021 (UTC)[jibu]

Ukurasa ulianzishwa na muhusika akijinadi (iliandikwa na mtumiaji:Czeus25 Masele 15:32, 27 Mei 2021‎)

Haina vyanzo wala umaarufu. Kipala (majadiliano) 09:32, 28 Mei 2021 (UTC)[jibu]

Haina vyanzo vya kuendana na makala, pia lugha yake sio ya kueleweka. Czeus25 Masele (majadiliano) 15:22, 1 Juni 2021 (UTC)[jibu]

Haina vyanzo, pia lugha yake si ya kueleweka. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:59, 5 Juni 2021 (UTC)[jibu]

Shule zisizo maarufu

[hariri chanzo]

Kwa jumla suala la shule halijaeleweka. Zipo zilizo maarufu kweli, lakini nakuta katika Kiingereza nyingi zisizo na sifa hiyo. Itakuwaje tukizifuta katika Kiswahili? --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:57, 23 Juni 2021 (UTC)[jibu]


Hili ni swala zito kidogo, ila kama tukiona tufuate utaratibu wa "notability" ipasavyo itakua rahisi kuzifuta. Pia nawaza watu weninge wanaweza kushawishi shule zao zitengenezewe kurasa Wikipedia kama njia ya kujitangaza na kuongeza credibility. Hivyo basi ni muhimu kuruhusu zile shule maarufu tu kutengenezewa kurasa. Suala ni tunaamua vipi umaarufu wa shule - ukongwe, marejeo yanayopatikana (references), kutoa watu wengi maarufu, rekodi ya ufualu, au...?

Aneth David (SLU) (majadiliano) 14:05, 2 Julai 2021 (UTC)[jibu]

Ni kweli shule sio maarufu lakini vyanzo au marejeo yanaweza kupatikana japo mpaka yachimbuliwe kiundani. Najitahidi kufukua vyanzo zaid na kuviongeza. Asante. MagoTech Tanzania (majadiliano) 20:33, 22 Juni 2021 (UTC)[jibu]

Kama hakuna vyanzo vya maana karibuni sana tufute. Kipala (majadiliano) 22:18, 22 Juni 2021 (UTC)[jibu]
Mpaka sasa nimeshapata baadhi ya vyanzo unaweza kuzitembelea. Asante MagoTech Tanzania (majadiliano) 08:46, 23 Juni 2021 (UTC)[jibu]

Lugha ni mbaya, (tafsiri ya kompyuta), haieleweki, tena sioni sana faida kutafsiri sehemu ndogo ya makala kuhusu amri ya kitaifa ya Uingereza ilhali mada yenyewe inahitaji kuelezwa kimsingi. Pia umbo la makala hailingani na masharti yetu. Ama iandikwe upya kabisa au ifutwe.Kipala (majadiliano) 20:18, 24 Juni 2021 (UTC)[jibu]

Tena lugha mbaya, tafsiri ya kompyuta, ni sehemu ndogo ya makala ndefu zaidi ambayo haielewki jinsi ilivyo. Iandikwe upya kabisa au kufutwa. Kipala (majadiliano) 20:23, 24 Juni 2021 (UTC)[jibu]

Tena tafsiri iliyofupishwa hadi kukosa maana. Pia jina halisi la Kiingereza limetafsiriwa kama lemma, ambayo tusifanye (taskforce - "kikosi kazi" ???). Iandikwe upya kabisa au kufutwa.Kipala (majadiliano) 20:27, 24 Juni 2021 (UTC)[jibu]

Kama makala megine za mtumiaji huyu, tafsiri iliyofupishwa hadi kukosa maana, sentensi ambazo hazieleweki, anatumia Wikipedia kama marejeo, umbo halilingani na masharti. Iandikwe upya kabisa au kufutwa. Kipala (majadiliano) 20:33, 24 Juni 2021 (UTC)[jibu]

Kama makala mengine za mtumiaji huyu, tafsiri iliyofupishwa hadi kukosa maana, sentensi ambazo hazieleweki, anatumia Wikipedia kama marejeo, umbo halilingani na masharti. Iandikwe upya kabisa au kufutwa. Kipala (majadiliano) 20:37, 24 Juni 2021 (UTC)[jibu]

Sioni maana yoyote kuanzisha "orodha" bila kitu kinachoorodheshwa. Kama makala mengine za mtumiaji huyu, tafsiri iliyofupishwa hadi kukosa maana, sentensi ambazo hazieleweki, anatumia Wikipedia kama marejeo, umbo halilingani na masharti. Iandikwe upya kabisa au kufutwa. Kipala (majadiliano) 20:39, 24 Juni 2021 (UTC)[jibu]

Kama makala mengine za mtumiaji huyu, tafsiri iliyofupishwa hadi kukosa maana, sentensi ambazo hazieleweki, anatumia Wikipedia kama marejeo, umbo halilingani na masharti. Iandikwe upya kabisa au kufutwa. Kipala (majadiliano) 20:42, 24 Juni 2021 (UTC)[jibu]

Nilimwandikia hivi: Umehariri ukurasa wa Mtumiaji:Brightonbaraka. Ama umehariri ukurasa wa mtumiaji mwingine -ambacho ni kosa- au umeanzisha nafsi ya pili kwa kumwandikisha mtumiaji tofauti - ambayo haitakiwi. Naomba ujieleze karibuni hapa au kwenye ukurasa wangu wa majadiliano au akaunti hii itafungwa. - Asipojibu katika siku zinazofuata, tufute ukurasa na kumzuia. Kipala (majadiliano) 05:12, 26 Juni 2021 (UTC)[jibu]

Nimemwandikia hivi: Ndugu, nimewahi kukuonya dhidi ya matangazo ya kibiashara. Hukujibu. Sana umeingiza viungo kwenye tovuti za makampuni kwenye ukurasa wako wa kibinafsi. Pia umeweka habari zote kwa lugha ya Kiingereza ilhali hapa tuko kwenye wikipedia ya Kiswahili. Pamoja na matangazo ya kampuni hizo zote ukurasa wako unaonekana kama tanganzo la kibiashara. Ninakupa siku 7 kuondoa matangazo ya kibiashara na kujitambulisha kwa Kiswahili. Menginevyo ukurasa wako utafutwa.

Asipojibu na kubadilisha napendekeza afutwe baada ya wiki 1. Lakini karibuni, kama wengine wanaona sababu nilizotaja hazitoshi, maana nikikumbuka vema ni mara ya kwanza kuona tatizo hilo kwamba mtumiaji anatumia ukurasa wake kujitangaza kwa Kiingereza. Kipala (majadiliano) 05:12, 26 Juni 2021 (UTC)[jibu]

Sijachungulia kama mwandishi alitumia google translate. Kwa namna yoyote, matini hii haina maana ikijaa makosa mabaya mno. "Anarchic" inatafsiriwa mara kama "anarchisim" - ilhali tuna makala ya uanakisti, maana hajafanya utafiti wowote. Sehemu nyingine anatafsiri "anarchic elements" kama "mambo ya kishirikina". ""anarchic" features of traditional African societies" ametafsiri kama "baadhi ya "anarchic" makala ya jamii za jadi za Kiafrika". Hii ni haiwezekani. Hajui Kiswahili? Au haelewi hata kidogo anachojaribu kutafsiri??? Ifutwe. Kipala (majadiliano) 23:55, 1 Julai 2021 (UTC)[jibu]

Kompyuta ya wingu maudhui yamefutwa, lemma imeunganishwa

[hariri chanzo]

Mtungaji wa makala ametumia google-translate neno kwa neno akifanya masahihisho machache sana. Alichagua matini gumu ya Kiingereza ambayo haielezi mada yake kwa njia inayoeleweka vizuri. Kutumia google translate badala ya kutafakari haisaidii. Hakujaribu kuondoa mfumo wa sentensi ndefu za Kiingereza. Kiswahili ni kibaya. Pamoja na yote tunayo tayari makala mfupi sana Wingu (mtandao) inayohitaji kupanushwa. Kwa kawaida tungesema "unganisha" lakin i sioni faida kunganisha mbegu na matini hiyo. Kipala (majadiliano) 19:22, 2 Julai 2021 (UTC)[jibu]

Makala inagusa mada muhimu katika historia lakini lugha ni mbaya mno. Nahisi ni tafsiri ya kompyuta ambayo haikuangaliwa tena. Haiwezi kubaki. Ama iandikwe upya kabisa , na kwa lemma tofaut (na sahihi), au ifutwe. Tena sijui amechukua wapi, kichwa cha Kiingereza kilikuwa kitu kama "Brussels Conference Act"; "conference act" ni maazimio ya mkutano, si "sheria". Kipala (majadiliano) 06:14, 10 Julai 2021 (UTC)[jibu]

Sehemu za matini hazieleweki. Ni tafsiri mbaya ya kompyuta. Itengenezwe kabisa au ifutwe. Kipala (majadiliano) 10:56, 12 Julai 2021 (UTC) ---Naomba kuipitia na kuitengeneza.[jibu]

Tafsiri ya kompyuta mbovu sana. Labda ieleweke kwanza. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:14, 12 Julai 2021 (UTC)[jibu]

Tafsiri ya kompyuta mbovu sana. Kichwa chenyewe ni kichekesho: kutafsiri races mbio badala ya makabila! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:14, 12 Julai 2021 (UTC)-- Olimasy (majadiliano)[jibu]

Mada muhimu lakini tafsiri mbaya ya komyuta, sehemu hazieleweki. Irekebishwe sana au kufutwa. Kipala (majadiliano) 14:23, 12 Julai 2021 (UTC)[jibu]

Makala imeundwa kwa kutumia tafsiri ya komyuta. Sehemu hazieleweki au si kweli tena (Sara hakuwa mjukuu wa Malkia Victoria, bali mtoto wa ubatizo). Habari za maisha yake yamefupishwa kiasi kwamba makala haieleweki tena (alikata ovyo katika sehemu ya "Early life" ). Inafaa kusahihishwa, jinsi ilivyo heri ifutwe. Kipala (majadiliano) 18:28, 12 Julai 2021 (UTC)[jibu]

Tafsiri ya kompyuta kama kawaida, mpaka kichwa hakilingani kabisa na yaliyomo. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 15:17, 14 Julai 2021 (UTC)[jibu]

Kiswahili ni kibaya mno, tafsiri ya kompyuta. Zitafsiriwe upya au kufutwa. Kipala (majadiliano) 07:37, 31 Julai 2021 (UTC)[jibu]

Kurasa juu ya VVU/UKIMWI katika nchi za Afrika

[hariri chanzo]

Zisiporekebishwa, naona zifutwe zote. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:13, 4 Agosti 2021 (UTC)[jibu]

Tafsiri mbaya ya kompyuta. Isahihishwe au kufutwa. Kipala (majadiliano) 10:48, 11 Agosti 2021 (UTC)[jibu]

Makala jinsi ilivyo ni tokeo la google translate. Sentensi kadhaa za Kiswahili ni kinyume cha maana ya kiasili ya Kiingereza. Pamoja na hayo makala ya enwiki haileti picha halisi ya hali ya Ukimwi nchini Uganda. Ama iandikwe upya au kufutwa. Kipala (majadiliano) 07:59, 25 Agosti 2021 (UTC)[jibu]

Ngono Kavu IMEREKEBISHWA

[hariri chanzo]

Vilevile. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:13, 4 Agosti 2021 (UTC)[jibu]

Vilevile. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:15, 4 Agosti 2021 (UTC)[jibu]

Vilevile. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:15, 4 Agosti 2021 (UTC)[jibu]

Virodene IMESAHIHISHWA

[hariri chanzo]

Tafsiri mbaya ya kompyuta, sentensi ya kwanza tu ya makala ya enwiki. Ifutwe, haina tija. Kipala (majadiliano) 21:16, 10 Agosti 2021 (UTC)[jibu]

Hii ni tafsiri ya makala ya enwiki Bagamoyo Port iliyotungwa 2018. Habari zake si kweli tena, mradi umeshabatilishwa, hakuna uhakika kama utaanza upya. Kimsingi mada inafaa, kuna historia na majadiliano meni. Lakini jinsi ilivyo isahihishwe au heri kufutwa kwa sasa. Kipala (majadiliano) 10:10, 12 Agosti 2021 (UTC)[jibu]

Makala ifutwe. Ni tafsiri ya makala ya enwiki kuhusu mipango iliyotangazwa mwaka 2004 iliyolenga 2020. Makala haikuendelezwa; kuianzisha sasa kwenye mwaka 2021 ingefaa kama ingeonyesha utathmini wa mipango hiyo ambayo haipo. Tena hakuna vyanzo, lemma yenyewe si sahihi. Jinsi ilivyo ni bure. Kipala (majadiliano) 13:09, 16 Agosti 2021 (UTC)[jibu]

Makala imeundwa bila marejeo yoyote yenye maana. Wikipedia ya Kiingereza hairuhusiwi kama chanzo. Pia mchangiaji ametumia google translate; ingawa sijaona makosa mazito ya msamiati, lakini sentensi si Kiswahili kweli, amefuata mtiririko wa Kiingereza. aseme kwa maneno yake. Kipala (majadiliano) 10:30, 19 Agosti 2021 (UTC)[jibu]

Makala ya ajabu; mkusanyiko wa viungo ambavyo havisemi kitu, haieleweki kiungo gani inataka kuonyesha nini, isipokuwa taarifa ya gazeti yenye habari ambazo hazionekani kwenye makala. Iandikwe upya kabisa au kufutwa. Sijui, ni makala ya mwenyewe nikiona hati za chuo ? Kipala (majadiliano) 23:04, 6 Septemba 2021 (UTC)[jibu]

Pengine ni mpangilio tu ambao arekebishe au asaidiwe kurekebisha. Makala ni nzuri sio ya ajabu

Makala hizo ziliundwa na mtumiaji mwenye matatizo ya lugha, sehemu kubwa ya matini haieleweki, hakuna vyanzo. Sioni maana kutumia muda kusahihisha makala isiyo na maana kwa wasomaji wetu. Kipala (majadiliano) 08:33, 23 Septemba 2021 (UTC)[jibu]

Ifutwe. Chanzo ni hasa enwiki kisichokubalika, sehemu iliyotafsiriwa haina habari inayoonyehsa umuhimu wowote, inaonyesha tafsiri ya kompyuta. Kipala (majadiliano) 10:14, 5 Oktoba 2021 (UTC)[jibu]

Ifutwe. Chanzo ni hasa enwiki kisichokubalika, maudhui kuna tafsiri ya kompyuta mbaya sana. Kama hakuna anayetaka kuiandika upya, iende tu. Kipala (majadiliano) 10:18, 5 Oktoba 2021 (UTC)[jibu]

Ifutwe. Chanzo ni hasa enwiki kisichokubalika, maudhui kuna tafsiri ya kompyuta mbaya sana. Sehemu iliyotafsiriwa haionyesha umaarufu wowote. Kipala (majadiliano) 10:20, 5 Oktoba 2021 (UTC)[jibu]

Ifutwe. Chanzo ni hasa enwiki kisichokubalika, maudhui kuna tafsiri ya kompyuta mbaya sana. Umaarufu haueleweki. Kipala (majadiliano) 10:24, 5 Oktoba 2021 (UTC)[jibu]

Makala zote nne zinatumia enwiki kama chanzo ambacho hakikubaliki, maudhui kuna tafsiri ya kompyuta mbaya sana. Sioni umaarufu kwa wote. Kipala (majadiliano) 10:32, 5 Oktoba 2021 (UTC)[jibu]

Makala haina mpangilio wa kueleweka na inategemea kumbukumbu za mtumiaji. Habari ziko kwa usahihi sehemu nyingine. Ifutwe. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:19, 11 Oktoba 2021 (UTC)[jibu]

Tafsiri ni mbovu, mtu ni maarufu kweli? --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:52, 30 Oktoba 2021 (UTC)[jibu]

Inaonekana huko Uganda ni maarufu kweli, tazama https://ugandatimes.ug/how-haruna-sentongo-of-haruna-enterprises-made-his-money-and-became-a-billionaire/ na https://nilepost.co.ug/2021/03/14/he-is-shy-and-reclusive-his-businesses-rake-in-billions-a-year-meet-haruna-ssentongo/, https://thecapitaltimes.co.ug/2019/08/22/meet-sentongo-haruna-the-ugandan-slum-youth-who-earns-26-million-a-year-in-rent-and-factory-sales/ Kipala (majadiliano) 09:39, 29 Novemba 2021 (UTC)[jibu]
Hata hivyo sioni ukurasa wake katika Kiingereza. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:46, 29 Novemba 2021 (UTC)[jibu]

Halieleweki kabisa. Ifutwe. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 06:18, 29 Novemba 2021 (UTC)[jibu]

Halieleweki kabisa. Ifutwe. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 06:18, 29 Novemba 2021 (UTC)[jibu]

Halieleweki kabisa. Ifutwe. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 06:18, 29 Novemba 2021 (UTC)[jibu]

Tafsiri ya kompyuta, umbo la hadithi... Ifutwe. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:18, 29 Novemba 2021 (UTC)[jibu]

Tafsiri ya kompyuta isiyoeleweka na isiyo na orodha yoyote. Ifutwe. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:33, 29 Novemba 2021 (UTC)[jibu]

Makala haifuati fomati wala haikupangwa katika jamii. Iboreshwe au kufutwa.Kipala (majadiliano) 08:40, 3 Desemba 2021 (UTC)[jibu]

Makala duni sana. Ifutwe. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:05, 3 Desemba 2021 (UTC)[jibu]

Michael Brake IBAKI IMETENGENEZWA

[hariri chanzo]

Hakuna vyanzo vinavyokubalika. Kipala (majadiliano) 12:10, 3 Desemba 2021 (UTC)[jibu]

Habari ndugu,
Vyanzo vimeongezwa katika makala husika HappyDeLuckiest (majadiliano) 20:33, 3 Desemba 2021 (UTC)[jibu]

Makala haifuati fomati wala haikupangwa katika jamii. Mtu mwenyewe ni maarufu kweli? Iboreshwe au kufutwa. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:32, 5 Desemba 2021 (UTC)[jibu]

Tafsiri ya kompyuta ya kutetea madhehebu fulani dhidi ya mengine. Irekebishwe au ifutwe. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:27, 16 Desemba 2021 (UTC)[jibu]

Tafsiri ya kompyuta. Isahihishwe au kufutwa. Kipala (majadiliano) 06:42, 23 Desemba 2021 (UTC)[jibu]

Baada ya kuhariri kiasi nimetambua makala ni tafsiri ya sentensi kwa sentensi kutoka https://en.wikishia.net/view/Usul_al-Din. Sina uhakika kama hii inaruhusiwa tukizingatia kanuni za Wikipedia:Hakimiliki. Pamoja na hayo si nzuri tukichukua moja kwa moja lugha ya kidhehebu katika makala za kidini. Nilipoanza kuhriri niliona tayari kwamba makala hii ilisema mara kwa ma "Uislamu" ambako ni lazima kusema "Shia", kwa sababu mambo haiwezekani kudai vile kwa Waislamu wote, na kwa jumla Washia ni idadi ndogo zaidi duniani na Afrika ya Mashariki. Vilevile nilishangaa kidogo kuona walimu (maayatollah) wa dini ambao wanatajwa tu bila kuwaeleza (kama wote wangewajua), kumbe asili ni tovuti ya Kishia.

Nataka kumpa mchangiaji "Pole". Ningependekeza atumie makala za en-wikipedia (ziko nyingi kuhusu Uislamu) ambako yuko huru kupanusha sehemu juu ya mafundisho ya Kishia. Ila tu hata kama Mkatoliki anachangia kuhusu mafundudisho ya kikatoliki, si sawa kutumia lugha inayodokeza mafundisho hayo ni "ya kikristo" kama madhehebu mengine yanatofautiana; ni sawa kabisa kuionyesha kama mafundisho ya kikatoliki. Hivyo ndivyo jinsi tunavyotakiwa kuandika kuhusu dini nyingine pia, hapa tukiweza kutambua tofauti zilizopo. Naomba majadiliano hapa na kwenye ukurasa wa ufutaji. Kipala (majadiliano) 18:49, 23 Desemba 2021 (UTC)[jibu]

Makala haifuati fomati, haina ushuhuda wa kuwepo kwa msamiati huu. Kama upo uongezwe, kama la tufute? Kipala (majadiliano) 17:58, 27 Desemba 2021 (UTC)[jibu]