Yericko Y. Nyerere

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Yericko Nyerere

Amezaliwa 14 Aprili 1983
Iringa, Tanzania
Nchi Tanzania
Kazi yake Muandishi wa Vitabu
Chama cha kisiasa CHADEMA


Yericko Yohanesy Nyerere (alizaliwa katika Kijiji cha Maduma, wilaya ya Mufindi, mkoa wa Iringa, Tanzania, 4 Aprili 1983), ni mfanyabiashara mwanzilishi wa Kampuni ya Yecco Group Limited. Ni mwanachama na mjumbe wa Mkutano Mkuu wa chama cha kisiasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Yericko Yohanesy Nyerere ni mshindi wa Tuzo ya Zikomo Africa Awards ya mwandishi Bora wa Vitabu Barani Afrika 2023 kupitia kitabu chake cha Ujasusi wa Kidola na Kichumi , toleo la 2016. Pia ameandika vitabu kama Mapambano ya Madaraka, toleo la 2017, Strategy The Road to Power, toleo la 2018, Mtu Baada ya Mtu, toleo la 2020 na MOSCOW: Oparesheni Ukraine, toleo la 2023. Pia amejinasibu hadharani kuwa anamwabudu Mungu kupitia Mizimu. Hivyo yeye sio "Mkristo" Wala " Muislamu"

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Yericko ana Stashahada ya Saikolojia ya kiuchunguzi kutoka katika chuo kikuu huria cha Uingereza (2016-2017), akapata Astashahada ya Uchunguzi na Upelelezi kutoka taasisi ya kimataifa ya Uchunguzi na upelelezi ya International institute of certified forensic investigation professionals inc kwa kushirikiana na Osulivan Associates International -USA (2015)

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Tangu 2010 hadi Julai 2015, Yericko Nyerere alikuwa mshauri wa Usalama na Ulinzi binafsi kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Wilbrod Peter Slaa. Kama mwanaharakati wa kisiasa anasifika kwa mazungumzo yake ya busara juu ya mabadiliko ya kisiasa na maendeleo ya kiuchumi nchini Tanzania, kazi zake hasa vitabu na makala mitandaoni zimesababisha ushawishi mkubwa kwa kura nyingi kwa watoa maamuzi na viongozi wa kisiasa. Amekuwa msukumo wa kisiasa kwa mabadiliko na ushiriki wa vijana na ushiriki katika ajenda ya serikali na mabadiliko ya kiuchumi.

Urithi wake wa fasihi juu ya uandishi pia unadhihirishwa juu ya mkakati wa ushindi wa ushirika wa vyama wa vyama pinzani nchini Tanzania (UKAWA) wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2015, ambapo aliandika mkakati huo ambao baadae aliufanya kitabu cha Strategy.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yericko Y. Nyerere kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.