Miranda Naiman

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Miranda Naiman
Nchi Bendera ya Tanzania Tanzania
Kazi yake Mjasirilamali

Miranda Naiman ni mjasiriamali Mtanzania, mmiliki na mwanzilishi wa kampuni iitwayo Empower na mmoja wa waanzilishi wa mgahawa ujulikanao kama Inspire cafe[1][2].

Aliwahi kutajwa kama mmoja kati ya wanawake 20 wenye nguvu na waliofanikiwa nchini Tanzania na pia aliwahi kutajwa na gazeti maarufu la Marekani (Forbes) linaloangazia mambo ya biashara kuwa ni mtaalamu wa kukuza vipaji vya watu[3].

Mbali ya hayo, kuanzia Julai 2019 mpaka sasa Miranda Naiman ni rais katika umoja wa Wajasiriamali unaojulikana kama Enterprenuership Organization (EO)[4][5].

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Miranda ni mmoja wa wahitimu katika shule ya International School of Tanganyika (IST) mwaka 2000. Baada ya hapo Miranda alijiunga na chuo cha Central school of speech and Drama cha jijini London akichukua masomo ya shahada ya BA (HONS) Drama, applied Theatre and education. Baada ya hapo aliunganisha masomo ya shahada ya uzamili chuo cha Leeds katika masomo ya Theatre and development studies. Aliendelea kusoma huku akifanya kazi mbalimbali nchini humo. [6]

Kazi yake[hariri | hariri chanzo]

Miranda Naiman mbali na kuwa mjasiriamali pia ni mama wa mtoto mmoja wa kiume. Mwaka 2019, Miranda alichaguliwa kuwa mmoja kati ya wanawake mia nchini chini ya mtandao unaojulikana kama Sheroes, ikiwa ni wanawake wenye michango chanya kwenye jamii.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Miranda Naiman kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.