Majadiliano ya mtumiaji:Molee4real
Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!
Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.
Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.
Kwa mawili matatu labda tazama:
- Kuhusu ukurasa wako wa mtumiaji na kurasa nyingine
- Ukurasa wa mwongozo
- Jamii:Msaada (makala zilizomo humo zinaweza kusaidia mara nyingi)
- Ukurasa wa jumuia (pamoja na Wikipedia:Wakabidhi, penye majina walio tayari kukusaidia)
- Makala za msingi za Wikipedia
Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.
Ujue miiko:
- usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje
- usiingize matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
- usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.
Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!
Welcome to Kiswahili Wikipedia!
We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:
- do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
- nor copied texts/images from other webs to this site!
- do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.
As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.
Kipala (majadiliano) 21:23, 8 Mei 2020 (UTC)
- Ahsante sana, nimefurahi sana kuwa hapa, na ninatazamia kuendelea kuwepo sana, kwa jailli ya kujifunza na kuchangia popote pale msaada unapohitajika kwa wakati wowote. Shukraan
Usaidizi wa upangiliaji wa makala
[hariri chanzo]Ndugu ricardo mimi ni mgeni hapa sina muda mrefu, ila mara kadhaa nimekua nikiona makala nyngi sana hasa za lugha ya Kiswahili zikiwa zime haririwa na wewe, una mchango mkubwa sana kwenye makala nyingi za Kiswahili Hongera kwako. Nina makala ambayo nimeaianzisha hapa, kwenye swwiki na ningependa uipitie kwa maboresho zaidi, Nafurahi sana kura miongoni mwa watumiaji wa swwiki na ninatazamia kutoa mchango mkubwa kwenye swwiki. Ahsante Na makala hiyo inaitwa Counsellorsalah.
- Ndugu, nimeshapitia na kurekebisha makala hiyo mara mbili, ila mwenyewe sijui kurekebisha vizuri sanduku la infobox mwanzoni. Kwa mengine namna ya kujifunza ni kuangalia kila mara marekebisho tunayofanya ili ufanye vizuri zaidi na zaidi. Unapoona katika "Mabadiliko ya karibuni" kwamba ukurasa wako umehaririwa na mwingine, bonyeza "tofauti" ili kuona wapi na wapi yamefanyika hayo mabadiliko. Polepole ndiyo mwendo. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:45, 9 Mei 2020 (UTC)
Mtagusano madhubuti
[hariri chanzo]Ndugu, tafsiri za mashine kwa Kiswahili hazieleweki. Afadhali uandike kidogo mwenyewe lakini ieleweke. Harakaharaka haina baraka. Sasa jaribu kupitia ukurasa huo na kuacha tu sentensi ambazo zinaeleweka. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:05, 9 Mei 2020 (UTC)
Mtagusano madhubuti
[hariri chanzo]Riccardo Riccioni Shukrani sana kiongozi, Mimi nilona mapendekezo ya kusaidia kuhariri baadhi ya machapisho muhimu yaliyokosekana kwa lugha ya Kiswahili, sikujua mwongozo, kwa sasa walau naweza kujaribu tena
Abbah Process
[hariri chanzo]Mimi simfahamu, ila sasa nimeshangaa kuona jina lake, mahali na tarehe ya kuzaliza ni tofauti... Ukweli ni upi? --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:19, 16 Mei 2020 (UTC) Riccardo Riccioni Abbah process ni muandaaji wa muziki lakini pia ni msanii, na asilimia 90% ya album ya harmonize afro east yeye na kampuni Yake ndo waandaaji, anamsimamia mwanamuziki kama darasa, marioo na Maua Sama. Kuhusu taarifa zake ninakusanya kutoka kwenye vyanzo vya habari tofauti tofauti, ila ivi karibuni Mtu wake wa masoko Alinitumia bar pepe yente uambatanisho wa tarehe sahihi ya kuzaliwa pia na Jina halisi la kuzaliwa. Ninaimani nimetoa ufafanuzi mzuri ndugu.
Moses tafadhali usikate tamaa kama makala hizi zinafutwa. Tatizo ni kubwa kweli ya A) kutumia marejeo ambayo hayathibitishi habari na B) marejeo machache ambayo yanaonyesha kitu ni hasa ya wenyewe. Kwa hiyo makala zinaweza kufutwa, tusubiri maoni. Labda unaweza kuziokoa ukizifupisha sana sana na kweli kuacha yale tu ambayo inathibitishwa moja kwa moja. Mimi sina muda kwa kazi hii - ni juu yako ilhali ulianzisha. Lakini huwezi kuandika "kampuni ya Tanzania" na kuweka marejeo yanayosema "kampuni ya China" jinsi ulivyofanya. Kipala (majadiliano) 10:20, 14 Septemba 2020
Naomba kuzirudisha upya na kutoa uthibitisho
[hariri chanzo]Kipala Nimeona sababu iliyotolewa kwa ajili ya ufutaji wa makala hizo mbili, nimejifunza jambo juu ya uundaji wa makala hapa wiki. kama ulivyoelezea kwenye ukurasa wa makala ya ufutaji, nilijaribu kuziingiza enwiki lakini zilikosa mantiki. nipo katika kujifunza kuhariri hapa wiki ili na mimi baadae niweze kuisaidia swwiki katika makala tofauti tofauti. hivyo naomba kuanzisha tena makala hizo mbili ambazo tayari zimefutwa, na kwa sababu ambazo ni sahihi, ila nimefanyia marekebisho sababu ya awali na kufupisha maneno, na kuelezea kile tu ambacho kina uthibitisho. ahsante. molee4real (majadiliano)
- Ndugu Moses Makala inakosa vyanzo mbalimbali, sio sahihi sana kutumia tovuti ya kampuni kama chanzo cha kuandika makala juu ya kampuni husika.
Hivyo usipojitahidi kuweka vyanzo makala inaweza kupendekezwa kufutwa. Amani! Czeus25 Masele (majadiliano) 15:34, 23 Septemba 2020 (UTC)
- Ndugu Molee4real, naona unajitahidi kujifunza nafurahi kuiona. Kwa sasa ninakuomba utumie njia ya kawaida ukichangia chochote kwenye kurasa za majadiliano uweke sahihi yako kwa umbo la ~~~~ pekee, yaani alama ya ~ mara nne. Hii itageukua kuonyesha jina lako pamoja na tarehe na saa, baadaye inarahishia mawasiliano. Kipala (majadiliano) 20:31, 23 Septemba 2020 (UTC)
Makala hii imependekezwa kufutwa, Hivyo inaweza kuboreshwa kwa kutoa vyanzo vya awali vyenye taarifa sahihi juu ya makala kwa kufuata taratibu za uandishi wa makala. Czeus25 Masele (majadiliano) 14:07, 25 Septemba 2020 (UTC)
We sent you an e-mail
[hariri chanzo]Hello Molee4real,
Really sorry for the inconvenience. This is a gentle note to request that you check your email. We sent you a message titled "The Community Insights survey is coming!". If you have questions, email surveys@wikimedia.org.
You can see my explanation here.
MediaWiki message delivery (majadiliano) 18:54, 25 Septemba 2020 (UTC)
- Tyari nimejibu ndugu. Molee4real (majadiliano) 05:14, 1 Oktoba 2020 (UTC)
Lugha ya michango yako
[hariri chanzo]Nimepitilia sasa hivi makala ya Foby uliyoanzisha. Nilisahihisha makosa mengi kupita kiasi, hasa katika tahajia pia mpangilio wa sentensi. Kiswahili kina kanuni zake , naomba tujitahidi kuziheshimu jinsi tunavyoweza, maana tunapozipuuza hatusaidii wasomaji. Naomba sana usome vema matini kabla ya kupakua. Labda anzisha makala katika nafasi yako binafsi (mfano Mtumiaji:Molee4real/JARIBIO umwombe mtu mwingine kuisoma. Tatizo la kurudia sana lilikuwa matumizi ya herufi kubwa na ndogo. Lingine matumizi ya tanbihi ambazo hazithibtishi unachoandika. Tovuti ya shule haithibitishi alisoma pale, na kadhalika. Google search si rejeo. Kipala (majadiliano) 17:57, 2 Oktoba 2020 (UTC)