Nenda kwa yaliyomo

Foby

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Foby
Foby akijiandaa kuzindua wimbo wake mpya.
Foby akijiandaa kuzindua wimbo wake mpya.
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Frank Ngumbuchi Felix
Pia anajulikana kama Foby
Amezaliwa 02.12.1992
Asili yake Tanzania
Aina ya muziki Bongo Flava
Kazi yake Mwanamuziki, Mtunzi, na Mwandishi
Ala R&B, Soul, Blues
Miaka ya kazi 2006 (14)
Ame/Wameshirikiana na Nandy, Gigy Money, Barnaba

Frank Ngumbuchi Felix (alizaliwa 2 Desemba 1992 (1992-12-02) (umri 32), katika Hospitali ya Mbesa Mission kwenye kijiji cha Mbesa, Mkoa wa Ruvuma, Tanzania) ni mwanamuziki wa Bongo Flava, lakini pia ni mtunzi wa mashairi na muandaaji wa ala za muziki.[1][2]

Elimu na maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Foby alisoma shule ya msingi Mbesa kuanzia awali mpaka darasa la saba na baadaye alichaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari katika shule ya Mbesa Sekondari ila baadaye alihamia katika shule ya kijeshi ya Ruhuwiko ya kikosi cha jeshi. Akiwa shuleni kupitia vipaji vyake vingine alijizolea umaarufu na kutwaa tunzo kupitia mchezo wa mpira wa miguuna Sarakasi, alinyakua vikombe kadhaa kwa ngazi ya mkoa, wilaya, kata na shule. [3]

Rasmi Foby alianza muziki akiwa bado shuleni, ambapo alikuwa ana tumbuiza kila jumapili kwenye siku ya sanaa, Foby alikuwa akipendwa zaidi kwa sababu ya vipaji vyake, alikuwa akicheza sarakasi, mpira na muziki. Wakati akiwa shule alipata ajali akiwa mchezoni na alivunjika mguu, hapo ndo ikawa mwisho wa ndoto yake kuwa mchezaji wa mpira wa miguu. Mwaka 2006 ndio mwaka aliingia rasmi kwenye sanaa ya muziki. Alianza kwa kutunga mashairi na kuwapa wasanii wengine, mfano "Madame hero" ya Hamissa Mobetto, "Sitanii" ya Banana zoro, "Mimina

Baadhi ya wasanii na nimbi zao
Jina la wimbo msanii
Madame hero Hamissa Mobetto
Sitanii Banana zoro
Nandy
Selena
Mimina Gigy Money
  1. "Muziki Ijumaa - Foby mwanamuziki, mtunzi anaetusua na wimbo wake Ng'ang'ana". RFI. 2018-02-14. Iliwekwa mnamo 2020-05-13.
  2. "Foby Releases New Song 'Punguza' - News | Mdundo.com". mdundo.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-05-13.
  3. "Jinsi Foby alivyopata 'demu' kiulaini | East Africa Television". www.eatv.tv (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-05-13.

Viungo via nje

[hariri | hariri chanzo]