Nenda kwa yaliyomo

Mtumiaji:Kipala/Archive 10

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ukurasa mama: Majadiliano ya mtumiaji:Kipala

Vyombo vya habari Tanzania

Vyombo vya habari ni muhimili muhimu katika nchi ya Tanzania kutokana na utoaji wake wa taarifa kwa umma.

Kabla hatujazama kwa kina zaidi kuangalia masuala mbalimbali kuhusu vyombo vya habari vya binafsi nchini Tanzania tuangazie sheria mbalimbali

Sekta ya Habari na Utangazaji ni moja ya sekta za huduma za jamii nchini. Sekta hii inatoa huduma ambayo ni haki ya msingi ya raia kama inavyotamkwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Ibara ya 18 ya Katiba inasema: (1)Kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati. (2)Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbali mbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii. Aidha, kutoa na kupokea habari kunatambuliwa duniani kote kuwa ni moja ya haki za binadamu.

Umoja wa Mataifa, na Umoja wa Afrika zina matamko rasmi ambayo serikali imeridhia kuhusu haki ya kupokea na kutoa habari. Haki hii, kama zilivyo haki nyingine zote, hutolewa kwa kuzingatia wajibu wa kila raia kwa jamii na uhuru binafsi wa binadamu. Dhima ya Sekta ya Habari na Utangazaji katika jamii ni kutoa habari, kuelimisha na kuburudisha.

Sekta hii inahudumiwa na vyombo vya habari ambavyo ni redio, magazeti, majarida, televisheni, filamu, video, intaneti, picha, vipeperushi, katuni na mabango. Maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano yamerahisisha upataji na utoaji habari.

Sekta hii imekua sana tokea Sera ya Habari na Utangazaji ilipotolewa mara ya kwanza mwaka 1993. Idadi ya magazeti ya kila siku imeongezeka kutoka mawili (2) mwaka 1992 hadi kumi na mbili (12) Januari, 2003.

Aidha, idadi ya magazeti ya kila wiki imeongezeka kutoka matano mwaka 1992 hadi 30 mwezi Januari, 2003. Kadhalika idadi ya vituo vya redio Tanzania Bara imeongezeka kutoka kimoja mwaka 1992 hadi 30 mwezi Januari, 2003.

Tanzania Bara hivi sasa ina vituo vya televisheni zaidi ya 30 ikiwemo Televisheni ya Taifa (TVT) iliyoanzishwa mwaka 2000. Wakati Sera inatolewa mwaka 1993, kulikuwa hakuna hata kituo kimoja. Aidha, idadi ya vyuo vyauandishi wa habari imeongezeka kutoka viwili mwaka 1993 hadi vinane mwezi Januari,2003. Viwili kati ya vyuo hivyo ni vyuo vikuu.Vilevile, Tume ya Utangazaji Tanzania ilianzishwa mwaka 1993 kusimamia Sekta ya Utangazaji na baadaye, mwaka 2003, iliunganishwa na Tume ya Mawasiliano kuanzisha Tume ya Usimamizi wa Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Asilimia kubwa ya magazeti na machapisho mengine husomwa zaidi mijini ambako usambazaji ni rahisi, na kiwango cha kujua kusoma na kuandika ni kikubwa. Baadhi ya Serikali za Mitaa na Halmashauri za Wilaya na Miji zimeanzisha vituo vya televisheni ambavyo hugharamiwa na halmashauri hizo. Aidha yapo magazeti na majarida yatolewayo na Asasi Zisizokuwa za Kiserikali na mashirika ya dini, ambayo mara nyingi hugharamia vyombo vyao vya habari.

Intaneti imeanza kuingia kwa nguvu nchini, na miji mingi sasa ina huduma hiyo. Hadi Desemba, 2002, kulikuwa na makampuni 21 ya huduma za intaneti (Dar es Salaam19, Arusha 1 na Mwanza 1). Idara za serikali, mashirika, na asasi za aina zote zinajitahidi kuwa na tovuti zao, ili wananchi wapate habari za vyombo hivyo kupitia mtandao huo wa kompyuta.

Tasnia ya habari ina vyama vya aina nyingi vilivyoundwa na wanahabari wenyewe. Kuna vyama vya kitaaluma, vyama vya kutetea maslahi na hali bora, kulinda maadili na uhuru wa vyombo vya habari, vyama vya kuendeleza maslahi ya wanahabari wanawake na kadhalika.

Aidha, zipo klabu za waandishi wa habari katika mikoa mingi. Hadi kufikia Desemba, 2002 mikoa 18 ilikuwa na klabu za waandishi wa habari, ambazo, licha ya kuratibu masuala ya taaluma ya habari katika mikoa, pia zinachangia katika kuhamasisha maendeleo ya wananchi.

Serikali ina Idara ya Habari (MAELEZO), ambayo wajibu wake umeainishwa katika Kanuni ya Kudumu C.16, na Sheria iliyofuta SHIHATA Na. 7 ya Mwaka 2000. Idara hii ina ofisi katika baadhi ya mikoa ya Tanzania Bara. Aidha, Wizara zote zimeteua maofisa watakaoshughulikia habari, elimu na mawasiliano.

Kuwapo kwa maofisa hao katika wizara na asasi, mashirika na makampuni mbalimbali huleta uhusiano mzuri katiya watoaji na watumiaji wa huduma hizo.Pamoja na maendeleo yaliyopatikana katika Sekta ya Habari na Utangazaji, utoaji wa huduma katika sekta umekuwa si wa kuridhisha kutokana na sababu mbalimbali.

Kosa la tafsiri

Kipala salaam. Ni sasa tu nikiona kwamba liko kosa la tafsiri katika fremu ya kushoto. Wingi wa -ingine kwa n-class si "zingine" lakini "nyingine" (tazama "Lugha zingine"). ChriKo (majadiliano) 22:58, 7 Januari 2013 (UTC)

Kweli kabisa! Una macho kama tai. Ila tu sijui namna ya kubadilisha. Nisipokosei ilikuwepo tayari wakati mimi niliingia 2005 kwa makala no. 150. Sasa tufanyeje? Nitauliza "juu" maana ninataka kuendelea kufuatilia badiliko la haki ya kuanzisha makala. Wasalaam. Kipala (majadiliano) 07:02, 8 Januari 2013 (UTC)
Wazee wangu, salaam. Msitoe macho sana! Hebu mwulize dada wa Kiwelisi ana jibu la swali lako bila kinyongo! Kingine lugha inakua - sio kila siku ipo palepale. Labda matumizi badala yake yawe: Lugha nyengine na si "Nyingine". Nyingine ni moja tu na si nyingi-nyingi!--MwanaharakatiLonga 06:36, 9 Januari 2013 (UTC)
"Lugha nyengine" labda ni Kiswahili kipya. Mimi nimefundishwa kwamba umoja na wingi za -ingi kwa n-class ni nyingine. ChriKo (majadiliano) 23:14, 9 Januari 2013 (UTC)
Nilijifunza vile, nadhani ni tofauti ya lugha sanifu na lugha inayozungumzwa halafu kuandikwa kwenye blogu za intaneti labda. Nikiangalia lugha ya kuandikwa sanifu ni "nyingine" (mfano: "sehemu nyingine za bara letu la Afrika" - katika "Ripoti ya mwaka ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali" http://www.parliament.go.tz/docs/reports/1251958625.pdf - kwa hiyo sidhani ya kwamba lugha sanifu imebadilika.) Kipala (majadiliano) 05:37, 10 Januari 2013 (UTC)
Haya, vyovyote kwangu sawa tu. Haohao uliowataja wa serikalini ndiyo wanaoandika katika ripoti zao "udhibitisho" badala ya "uthibitisho"! Sio watu wa pwani wale ni wabara wote wanaoandika zile ripoti - therefore I'm not so surprised! Nimekupa mwangaza tu kama unavyoona sasa hivi hatuandiki tena "onyesha" bali "onesha! Kazi kwenu!--MwanaharakatiLonga 08:27, 10 Januari 2013 (UTC)
"Udhibitisho" sijaona katika taarifa ile - wanaandika "hati ya ukaguzi ni thibitisho", "kupata uthibitisho wa kutosha". Kuhusu "nyingine" kuwa uwingi naona sasa pia mfano kwenye tovuti ya Zanzibar: "SMZ imepiga marufuku vipindi vya Uamsho vilivyokuwa vinatangazwa na Sauti ya Tanzania Zanzibar pia katika Radio nyingine zote." Labda tofauti kati ya Kiunguja na Ki-Dar? (http://zanzibarnikwetu.blogspot.com/2012/10/uamsho-sasa-yabanwa.html) Kipala (majadiliano) 12:30, 10 Januari 2013 (UTC)
Shida inakuja unategemea sana mtandao wakati mie ninapata habari mahali tofauti-tofauti. Mfano, kuna kipindi kipo Redio One kila siku ya Ijumaa kuna wataalamu wa lugha ya Kiswahili wanazungumza! Kuna mambo mengi yanazungumzwa humu na wala katika mtandao sijayaona. Sijui mnfanyaje kwa taarifa ambazo hazipo katika mtandao na wala katika hati ulizonazo hazipo? Kuna mamabo mengi yamebadilishwa katika Kiswahili, lakini mtandaoni huyakuti isipokuwa katika maredio ya Tanzania bara sana-sana. Kazi ipo. Narudia tena, nimesema yote sawa tu. Bonge a.k.a,--MwanaharakatiLonga 15:03, 10 Januari 2013 (UTC)
Muddy unasema kweli kabisa ni vigumu kuhariri na kuandika wakati wa kukaa mbali na watu wanaoongea! Lugha inaendelea tu kila mahali - kwa bahati nzuri lugha ya kiandishi imesanifishwa kwa hiyo inabadilika polepole kuliko lugha hai. Kipala (majadiliano) 12:00, 14 Januari 2013 (UTC)

Hi, sorry for writing in English. I'm writing to ask you, as a bureaucrat of this wiki, to translate and review the notification that will be sent to all users, also on this wiki, who will be forced to change their user name on May 27 and will probably need your help with renames. You may also want to help with the pages m:Rename practices and m:Global rename policy. Thank you, Nemo 17:15, 3 Mei 2013 (UTC)

Hi, sorry for writing in English. I'm writing to ask you, as a bureaucrat of this wiki, to translate and review the notification that will be sent to all users, also on this wiki, who will be forced to change their user name on May 27 and will probably need your help with renames. You may also want to help with the pages m:Rename practices and m:Global rename policy. Thank you, Nemo 17:15, 3 Mei 2013 (UTC)

Hi, sorry for writing in English. I'm writing to ask you, as a bureaucrat of this wiki, to translate and review the notification that will be sent to all users, also on this wiki, who will be forced to change their user name on May 27 and will probably need your help with renames. You may also want to help with the pages m:Rename practices and m:Global rename policy. Thank you, Nemo 17:15, 3 Mei 2013 (UTC)

Hi, sorry for writing in English. I'm writing to ask you, as a bureaucrat of this wiki, to translate and review the notification that will be sent to all users, also on this wiki, who will be forced to change their user name on May 27 and will probably need your help with renames. You may also want to help with the pages m:Rename practices and m:Global rename policy. Thank you, Nemo 17:15, 3 Mei 2013 (UTC)

Kigezo:Kituo cha redio

Hi Kipala. Sorry to write you in English, but translating this into Swahili would take me a bit long. I have a problem with a new template I created. I modelled it on Kigezo:Uainishaji. It seems to be working except for the fact that when employed in an article, e.g. Radio France Internationale, the main text is included in the infobox. I have stared at it for a long time and counted the braces (curly brackets) many times. I still don't understand what is going on. Can you please have a look at it? Thanks. ChriKo (majadiliano) 22:25, 1 Septemba 2013 (UTC)

Hi ChriKo. On behalf of Mzee Kipala, allow me to take the wheel. But before to go through it, I've got one question: where did the template come from? Did you just create it from the scratch or you have just imported it from the English Wikipedia? There is a million factors for asking such a question. Cheers!--MwanaharakatiLonga 04:37, 2 Septemba 2013 (UTC)
Now I understood you. You have just copied the Uainishaji Template. Sighs! Let me check it out.--MwanaharakatiLonga 04:42, 2 Septemba 2013 (UTC)
Sorry Muddyb for giving you extra work. I thought changing the Uainishaji template would be rather straightforward. The corresponding one in English is too complicated for me. It would take me many days to figure it out and adapt to the Swahili Wikipedia. The one I created seemed to work, but then I noticed that it sucked the the main text of the article in the infobox. ChriKo (majadiliano) 12:33, 2 Septemba 2013 (UTC)

Haya nimeanzisha kigezo kipya kigezo:rediotv kwenye msingi wa kigezo:mto inafanya kazi. Inahitaji masahihisho lakini sasa naenda kulala. Kipala (majadiliano) 21:03, 14 Septemba 2013 (UTC)

Asante sana, Mzee Kipala, kazi nzuri! ChriKo (majadiliano) 11:54, 15 Septemba 2013 (UTC)

Thanks

Thank you Kipala for your Welcome!--Angler45 (majadiliano) 18:14, 29 Oktoba 2013 (UTC)

Karibu sana! --Kipala (majadiliano) 21:05, 30 Oktoba 2013 (UTC)

Hi, dear Kipala, how are you? Thanks a lot for you welcome message!

I made only two pages, and I ask your help to correct them, because I'm not Kiswahili native speaker. Please...

Caselle Landi is the small village where I live, and it's near the Po. Please, I ask your help also for the future, if you want. I'll translate or make new pages in Italian or Portuguese for you!

Thanks a lot, my new friend!

Rei Momo (majadiliano) 22:53, 30 Oktoba 2013 (UTC)

Thank you very much! Rei Momo (majadiliano) 23:09, 31 Oktoba 2013 (UTC)

Hi Kipala, I'm here to ask again your help, if you have 20 minutes for me. Can you make a new Kiswahili page for me? I can help you to make a new page in Italian or Portuguese Wikipedia. Thank a lot for your reply. Sincerely Rei Momo (majadiliano) 23:36, 3 Novemba 2013 (UTC)

No idea. Post your text here and I see if I find time. (BTW: "majadiliano" means "discussion") --Kipala (majadiliano) 05:22, 4 Novemba 2013 (UTC)
Thank you very much! I corrected also Majadiliano with your name Kipala!!! The page is [[:en:Benedicta Boccoli|Benedicta Boccoli, a wonderful Italian actress. You can put the two pictures, and to say she moved from Milan to Rome, and she has a sister actress, Brigitta Boccoli.
The important is to say that she started at televisione and films, but now she acts in thetaer, she became great in theater!!!
Thanks a lot Rei Momo (majadiliano) 10:25, 4 Novemba 2013 (UTC)

Wiki Indaba conference

Salaam, mzee wangu. Kuna mpango wa mkutano mjini Johannesburg mwezi wa pili mwakani, angalia http://wikiindaba.net/index.php?title=Main_Page - pia, umeombwa kujibu maswali yao kwenye tovuti la Google docs: https://docs.google.com/forms/d/1zEk6hw4IiQYVrdJGYphPhQHOQFi4wdOIXvzVj9vy_gU/viewform Asante kwa msaada wako. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 12:24, 4 Novemba 2013 (UTC)

Barua pepe

Salaam, Kipala. Ndugu, nimekutumia barua pepe. Tafadhali naomba utazame!--MwanaharakatiLonga 06:11, 6 Novemba 2013 (UTC)

Salaam. Yule jini niliyemtoa katika ile chupa naona sasa ameanza kazi yake! Ahante kwa chupa ya ajabu. Nimefanya kadiri ipasavyo kupitia email.--MwanaharakatiLonga 11:38, 7 Novemba 2013 (UTC)

Thank you

Good morning Kipala,
It looks like muy talk page has recently been vadalized. Thank you for taking care of it. As I do not speak a single word of swahili, I would not even have been to understand able what was happening and why nor to do so. Thanksfully, the community is able to provide efficiently. Thanks again and friendly regards.
Hop ! [[Utilisateur:Kikuyu3|Kikuyu3]] [[Discussion utilisateur:Kikuyu3|Sous l'Arbre à palabres]] (majadiliano) 10:14, 7 Novemba 2013 (UTC)

On essaie! Kipala (majadiliano) 14:26, 7 Novemba 2013 (UTC)

Tanzania

Yes I would certainly be able to help. Where is the census data? Rich Farmbrough , 21:55, 17 Novemba 2013 (UTC).

OK I have the data. Rich Farmbrough , 01:06, 18 Novemba 2013 (UTC).
Wow so you were faster ! That is great. Appreciate very much if you can help. There are some changes besides the numbers. a) a number of kata (commune, village, township, city subdistrict) now belongs to a different wilaya (district) because there some vilaya have been divided into two. But maybe this will not affect a change of numbers. b) I have seen some possibly new kata this is either a mistake in the old data or we left them out BUT it could also mean that they have divided some kata. Anyway i guess for the majority it should work fine.
Now if you are familiar with bots maybe you could advise me later how to change the data for new wilaya. i did it by hand for the kata of wilaya ya Bahi; they all were before part of wilaya ya Dodoma Vijijini and so there are 4 places where the wilaya is mentioned, 2 in the text body and others in the tables....
Yes I saw that a couple of wilaya had been divided. The easy way is to make a list of the pages and use AWB to make the changes, I was planning on fixing these up. It would be best to mention in the article that the wilaya of the kata has changed. I am happy to run the AWB if you wish, but I need the Kiswahili phrase for the change "(formerly part of wilaya Dodoma)".
As to the rest of the articles, once the wording is fixed updating them is something I can take care of if you wish. I had a quick effort with Kigogo (kata) - doubtless all the Kiswahili words I added are wrong, if you of Muddy can fix them up I will take it as a model.
All the best. Rich Farmbrough , 15:12, 18 Novemba 2013 (UTC).
Rich, I went thru your example Kigogo_(kata) (which I moved). My proposal: sex ratio and household size is nothing to be mentioned here in the stub. It looks to me like very special interest and who wants that can look it up in the reference. But for any stub that gets additional information (what we aim for by creating these stubs, with a bit success) it makes a pretty unreadable entry if you first have to fight your way thru all these figures. One would do (residents total), three are enough (total, men, women). What do you think? Kipala (majadiliano) 20:01, 18 Novemba 2013 (UTC)
As for mentioning ""(formerly part of wilaya Dodoma)" - why should we mention this on kata-level? for wilaya-level ok. I am going to work on a list of the new wilaya. Lets communicate then. --Kipala (majadiliano) 21:55, 18 Novemba 2013 (UTC)

Now another question: do you know where to change the menue items of a wikipedia edit window? when the new menue layout came somebody (who??) set this up for us and there are labels connected to icons which are not really understandable. And one icon for references disappeared. i have no idea where to look for it and whom to ask. --Kipala (majadiliano) 06:54, 18 Novemba 2013 (UTC)

Salaam, Kipala. Eti mzee wangu - wapi umekwama kwenye swali lako la pili? Kuhusu sura mpya.. Niambie labda naweza kukusaidia kwa vile mara nyingi huwa nashirikishwa katika masuala hayo ya tafsiri za kusano zetu!--MwanaharakatiLonga 08:56, 18 Novemba 2013 (UTC)
Asante kwa kujibu! Sasa nimeangalia kidogo Wikipedia:Mwongozo maana niliitunga kabla ya mabadiliko haya kwa hiyo picha za icons haziligani tena. Hapo nimeona tena maelezo yanayo tokea ukigusa icon. Je unajua wewe "faili futike" ni mnyama gani?? Inamaanisha "ingiza picha" (ing. wanasema: Embedded File, lakini hali halisi ni picha) na hii nataka kuona pale. Kingine ilikuwa maelezo ya icon hii sikumbuki maneno lakini haikueleweka pia. Ila tu tangu siku 3 imepotea sijui namna gani. Nani anafanya mabadiliko haya? Kipala (majadiliano) 20:01, 18 Novemba 2013 (UTC)
Haya, tulifanya hizi tafsiri na yule dada wa Wales kwa kutumia "klnX IT Extended Glossary May 2009" ndiyo iliyotoa tafsiri ya "embedded" = "futike". Mimi na dada hatukuweza kubishia tafsiri za wanazuoni! Na hiyo icon ni ya "reference". Imeandikwaje? Wazo: pendekeza jinsi unaona itakuwa rahisi kueleweka kisha niyapeleke kule!--MwanaharakatiLonga 06:11, 22 Novemba 2013 (UTC)
Kumbe futike! Sidhani mtu anaielewa. Lakini si lazima kutafsiri "embedded file" maana hata kwa Kiingereza haieleweki mara moja ya kwamba "File" = picha na "embedd" maanake kuingiza kiungo cha picha itakayoonekana. Mimi napendekeza lugha kama "ingiza picha" au "kiungo cha picha".
Kuhusu reference ile picha imerudi kwangu baada ya kutoonekana siku 1.5. Maandishi yake ni "tiniwayo". Je umewahi kuona neno hili? Naomba turahisishe maana kwa kawaida tumetumia hadi sasa lugha ya "marejeo". Hata ukibofya alama unapata diriha inayosema "Ingiza marejeo". Iwe hivyo hata kwenye hatua ya kwanza. Mimi nataka kusahihisha makala za msaada na mwongozo hapa sababu naangalia.Kipala (majadiliano) 08:56, 22 Novemba 2013 (UTC)
Sawa. Nitaongea na dada tubadilishe lugha hiyo kwenda "Ingiza Picha". Je, nini tofauti ya "footnote" na "reference"? Hapa KlnX IT wanasema: "footnote" = "tiniwayo". Mwongoza tafadhali!--MwanaharakatiLonga 10:03, 22 Novemba 2013 (UTC)
Kiingereza si tofauti. Nilifikiri tu "tiniwayo" ni neno lisilofahamika lakini labda ujinga wangu tu. kama wewe ulijua neno hili kabla ya kuhariri hapa ibaki na mimi nimejifunza. Lakini kama umeikuta hapa mara ya kwanza heri tutumie lugha rahisi. Kipala (majadiliano) 10:53, 22 Novemba 2013 (UTC)
Nimebadilisha tiniwayo iwe "marejeo". Nimebadilisha "Faili futike" iwe "ingiza faili". Faili mara nyingi ni picha, lakini inaweza kuwa faili ya sauti au video. Usipopenda "ingiza faili" tungeweza kusema "ingiza picha au faili lingine". Mabadiliko yamefanyika kule translatewiki.net. Yataonekana hapa baada ya siku chache. Ukipenda kusaidia kutafsiri jumbe za MediaWiki, tafadhali sajili akaunti pale. Kuna kazi nyingi za kufanya pale. Kwa mfano, bado core messages hazijakamilishwa. Mwanaharakati hajapata nafasi ya kupitia jumbe zote nilizopendekeza mimi; si mbaya kama mwingine angetekeleza kazi hiyo. Jumbe zinazotakiwa kupitiwa hasa kwa sababu fulani fulani zinapatikana katika fungu la "outdated", hasa core na extensions. Ukipata shida kuelewa jinsi ya kufanya kazi pale translatewiki.net unaweza kuniuliza katika ukurasa wangu pale. Lloffiwr (majadiliano) 19:30, 23 Novemba 2013 (UTC)
Maneno ya teknolojia hayazungumzwi katika lugha za mawasiliano ya kawaida. Labda marejeo ni rahisi kuliko "tiniwayo".--MwanaharakatiLonga 13:51, 22 Novemba 2013 (UTC)

Clean up

Hallo Kipala, hast du Zeit, die Artikel aus der Löschkat (Jamii:Makala kwa ufutaji) zu entfernen? Danke --Kolja21 (majadiliano) 13:43, 19 Novemba 2013 (UTC)

Google translation

Hey Kipala

Would be interested to hear from your perspective what you feel went wrong with the Google translation project? We are hoping that the work we are doing in collaboration with Translator Without Borders will be positive for all involved. Further details can be seen here [1] James Heilman, MD (talk · contribs · email)(please leave replies on my talk page) 05:11, 28 Novemba 2013 (UTC)

Request for username change : Hosiryuhosi -> Rxy

Hello. Could you please change my username?

  • Current username: Hosiryuhosi
  • Target username: Rxy
  • Reason: I want to change my current username to short username at WMF wikis globally. Note: Global account "Rxy" is my account (confirm). I'm sorry for request to here. I can't find request page. Thanks. --Hosiryuhosi (majadiliano) 18:27, 8 Machi 2014 (UTC)

Thanks for moving my user page. However I want to change my user name to rxy. It should use Special:RenameUser. Regards,--Hosiryuhosi (majadiliano) 12:34, 19 Machi 2014 (UTC)

Update on Upcoming Wiki Indaba Conference

Hello Sir. My name is Rexford Nkansah, currently serving as a Wikipedian in Residence at the Africa Centre in Cape Town.

The Wikimedia Foundation has shared with us the incredible number of edits that you have done on this Wikipedia. You have are one of those with the high contribution to this Wikipedia.

As one of the highest contributors to one of the languages of the African continent, I want to inform you about the upcoming Wiki Indaba Conference which is similar to Wikimania, however, its designed by Africans for Africans.

This message is to inform you about scholarship to attend application currently open. You're invited to apply for scholarship to attend this conference.

Please see the main Wiki Indaba Website for more details on Eligibility and Deadline – look at www.wikiindaba.net for more details. And like the facebook page for updates.

Please don't hesitate to get in touch should you have any questions.

my contact is rexford@wikiafrica.net

Thanks for your message. I wanted to say: "Yaba Angelosi (born in South Sudan) is a singer, musician and a music producer living in the the United States. He also runs his own studio and production house "Assida Records / Assida Productions". "

Could you please correct the text in Swahili accordingly? I simply don't known Swahili and would depend on your help. Many thanks for your interest. Werldwayd (majadiliano) 11:42, 11 Aprili 2014 (UTC)

Jibu langu: Naomba ushirikiano wako!

Mpendwa Kipala. Uliona jibu langu (Majadiliano_ya_mtumiaji:ChriKo#Naomba ushirikiano wako!)? ChriKo (majadiliano) 21:06, 18 Mei 2014 (UTC)

Re: Naomba ushirikiano wako!

Yeah, uhakika. Pia mimi aliongeza. [2]. Best upande --Cekli829 (majadiliano) 05:21, 20 Mei 2014 (UTC)

Kura kwa Malangali

Salaam, Kipala. Nilivyoandika kwenye ukurasa wa Wakabidhi, nimefurahi sana kuwa Ndg Malangali amerudi kwetu. Sasa ungeweza kutafakari kura yako tena kuhusu kumwondolea haki au la. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 07:27, 20 Mei 2014 (UTC)

Why was this useful book page deleted without any discussion?
Varlaam (majadiliano) 01:27, 22 Mei 2014 (UTC)

Thanks for asking. There was a discussion. Wikipedia:Makala_kwa_ufutaji/Nyaraka_3#Vitabu_bora_100_vya_gazeti_Le_Monde The page was proposed for deletion on 11th January and got the deletion tag. Was deleted on 28th January. Obviously it was not a page in Swahili language. Cheers! Kipala (majadiliano) 05:38, 22 Mei 2014 (UTC)

Habari yako, Ndg Kipala? Je, bado unahitaji ukurasa huo au inawezekana kuufuta? Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 05:03, 12 Juni 2014 (UTC)

An important message about renaming users

Dear Kipala, My aplogies for writing in English. Please translate or have this translated for you if it will help. I am cross-posting this message to many places to make sure everyone who is a Wikimedia Foundation project bureaucrat receives a copy. If you are a bureaucrat on more than one wiki, you will receive this message on each wiki where you are a bureaucrat.

As you may have seen, work to perform the Wikimedia cluster-wide single-user login finalisation (SUL finalisation) is taking place. This may potentially effect your work as a local bureaucrat, so please read this message carefully.

Why is this happening? As currently stated at the global rename policy, a global account is a name linked to a single user across all Wikimedia wikis, with local accounts unified into a global collection. Previously, the only way to rename a unified user was to individually rename every local account. This was an extremely difficult and time-consuming task, both for stewards and for the users who had to initiate discussions with local bureaucrats (who perform local renames to date) on every wiki with available bureaucrats. The process took a very long time, since it's difficult to coordinate crosswiki renames among the projects and bureaucrats involved in individual projects.

The SUL finalisation will be taking place in stages, and one of the first stages will be to turn off Special:RenameUser locally. This needs to be done as soon as possible, on advice and input from Stewards and engineers for the project, so that no more accounts that are unified globally are broken by a local rename to usurp the global account name. Once this is done, the process of global name unification can begin. The date that has been chosen to turn off local renaming and shift over to entirely global renaming is 15 September 2014, or three weeks time from now. In place of local renames is a new tool, hosted on Meta, that allows for global renames on all wikis where the name is not registered will be deployed.

Your help is greatly needed during this process and going forward in the future if, as a bureaucrat, renaming users is something that you do or have an interest in participating in. The Wikimedia Stewards have set up, and are in charge of, a new community usergroup on Meta in order to share knowledge and work together on renaming accounts globally, called Global renamers. Stewards are in the process of creating documentation to help global renamers to get used to and learn more about global accounts and tools and Meta in general as well as the application format. As transparency is a valuable thing in our movement, the Stewards would like to have at least a brief public application period. If you are an experienced renamer as a local bureaucrat, the process of becoming a part of this group could take as little as 24 hours to complete. You, as a bureaucrat, should be able to apply for the global renamer right on Meta by the requests for global permissions page on 1 September, a week from now.

In the meantime please update your local page where users request renames to reflect this move to global renaming, and if there is a rename request and the user has edited more than one wiki with the name, please send them to the request page for a global rename.

Stewards greatly appreciate the trust local communities have in you and want to make this transition as easy as possible so that the two groups can start working together to ensure everyone has a unique login identity across Wikimedia projects. Completing this project will allow for long-desired universal tools like a global watchlist, global notifications and many, many more features to make work easier.

If you have any questions, comments or concerns about the SUL finalisation, read over the Help:Unified login page on Meta and leave a note on the talk page there, or on the talk page for global renamers. You can also contact me on my talk page on meta if you would like. I'm working as a bridge between Wikimedia Foundation Engineering and Product Development, Wikimedia Stewards, and you to assure that SUL finalisation goes as smoothly as possible; this is a community-driven process and I encourage you to work with the Stewards for our communities.

Thank you for your time. -- Keegan (WMF) talk 18:24, 25 Agosti 2014 (UTC)

--This message was sent using MassMessage. Was there an error? Report it!

Kupakia mafaili, Sogora ya kupakia?

Wikimedia Commons logo

Hello! Sorry for writing in English. As you're an administrator here, please check the message I left on MediaWiki talk:Licenses and the village pump. Thanks, Nemo 19:22, 18 Septemba 2014 (UTC)

Your revert at John F. Kennedy

Hello, I inform you that you're wrong on this revert, the phrase introduced by the IP is distorted and therefore is false; true sentence says exactly the opposite. Greetings.--Syum90 (majadiliano) 18:58, 15 Novemba 2014 (UTC)

Hello! Could you translate an article about boycott of Russian goods in Ukraine for the Swahili Wikipedia? Thanks for the help.--Trydence (majadiliano) 19:27, 23 Novemba 2014 (UTC)

Mabadiliko

Asante sana Kipala vipi upo Iran au upo wapi natumaini upo salama lakini kama ungekuwa Dar es salaam ningekualika angalau uje kwenye semina mojawapo, ManawaElimu kwanza 06: 15, 11 December 2014 (UTC)

Asante kwa salamu sijambo. Unataja semina - ya aina gani? Kipala (majadiliano) 21:43, 10 Desemba 2014 (UTC)

Wikipedia font

Hi Kipala. Is really nice to meet you! I'm not the author of any Wikipedia logo. Perhaps there is a mistake because I've done some images to illustrate an article about Wikipedia's logos. Buy, anyway: the font used to write "Wikipedia, the free encyclopedia" es Linux Libertine, BUT... the "W" must be wrote with Hoefler text.

You can find detailed instructions about how to make the Wikipedia logo here (Word mark creation).

Hope my advice was useful for you. Kind regards. Kipala. Hakuna matata. Pepe.--Roblespepe 23:50, 6 Februari 2015 (UTC)

VisualEditor here

Hi there! You have messages here. Best, --Elitre (WMF) (majadiliano) 16:11, 16 Machi 2015 (UTC)

More answers in the same place! Whatamidoing (WMF) (majadiliano) 23:15, 23 Machi 2015 (UTC)

Ripoti ya warsha

Naona muswada wako unaendelea vizuri. Napendekeza uongeze kwamba walishiriki pia walimu 2 wa chuo kikuu. Pia ufute swali kuhusu inveta na betri zetu: ilikuwa na uwezo wa kutoa umeme kwa saa nyingi. Mbali ya hayo, nimepitia kidogo kitabu chako cha Historia ya Kanisa. Hujawaza kutumia sehemu zake kwa ajili ya Wikipedia? Au kuna suala la hakimiliki? Pasaka njema! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:32, 3 Aprili 2015 (UTC)

kuhusu warsha morogoro

Habari! kipala mimi ni mmoja wa wanawarsha ambayo ilifanyika morogoro kwahiyo nimejifunza mambo mengi kuhusu Wikipedia hasa ya Kiswahili kwahiyo mzee kipala nimekufahamu kupitia warsha iliyofanyika Morogoro. Asante!Enock John (majadiliano) 17:00, 6 Aprili 2015 (UTC)

Ndugu Enock John, asante kwa kuniarifu! Nafurahi sana kukuona hapa! Kwangu zilikuwa siku nzuri sana kwenu Alfagems. Nimebarikiwa! (halafu ombi dogo: ukiandika kwenye kurasa za majadiliano, andika chini ya matini iliyopo, si juu. Ni kawaida tu, samahani, kuna mengi ya kuzoea katika mazingira mapya...) Kipala (majadiliano) 05:30, 7 Aprili 2015 (UTC)

Mchango wa mawazo

Ndugu Kipala, kuna makala nimetunga, lakini kumbe yapo mengine (ijapokuwa ile yangu imetanuka zaidi). Tafadhali tupieni jicho hapo: Majadiliano:Uislamu nchi kwa nchi.. Kisha fanyeni uamuzi.--MwanaharakatiLonga 19:05, 15 Aprili 2015 (UTC)

Sfinksi

Ndugu, nadhani bila kukusudia umefuta mabadilisho niliyokufanyia katika mada hii. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 15:31, 18 Aprili 2015 (UTC)

Nadhani ni kweli. Nikihariri narudi mara kadhaa nakumbuka nikapata tangazo kuwa hariri ziligongana lakini sijachungulia. Utanisamehe? Kipala (majadiliano) 16:06, 18 Aprili 2015 (UTC)

Hi. Please delete Kigezo:Link GA the same way you deleted Link FA so that we finish the task. Thanks, Magioladitis (majadiliano) 13:28, 22 Aprili 2015 (UTC)

RE:Tahajia ya kifaransa

Hello, Kipala! Thanks a lot for your message and comments.
Although not used all the time, these links and changes ([3] [[Société Générale|Societe Generale de Banques en Côte d'Ivoire]] --> [[Société Générale|Société Générale de Banques en Côte d'Ivoire]], [4]: Saint-Etienne --> Saint-Étienne) prove that French spelling is not unknown on swWP. Nevertheless, this could be an exception to the rule, considering what you wrote about "the average East African user".
That is why, only if you approve, I am willing to redirect those red links I have changed according to the French spelling ([5], [6], [7], [8], [9], [10]) — the rest of the changes did not affect links: proper names that remained "blue-linked" ([11], [12], [13], [14], [15], [16], [17]), or were already red links ([18], [19]), non-linked proper names ([20], [21]) external links ([22]) and references ([23]).

Thanks a lot for reading this message. Best wishes!--Alpinu (majadiliano) 21:33, 2 Mei 2015 (UTC)

Hi Alpinu, thx for the fast reaction. Please go ahead with the redirects. For eample, you may have noticed that our lemma for the country is labeled Cote d'Ivoire, whereas the text itself starts with Côte d'Ivoire; the article can be reached via redirects Côte d'Ivoire, Ivori Coast , Ivory Coast , Kodivaa. Orthography is often fluent in Swahili, and same for form of names of distant places that is why we amply work with redirects. As you have a nose for French names - be welcome to do redirects (without accents) also to other Lemmas which are there with accent - like e.g. Saint-Etienne as a redirect for Saint-Étienne. Reason is - where we have accent (similar for Spanish ~ etc) either someone copied from a different language wikipedia or a Non-Swahili-Speaker like you started a stub. But nearly no East African user will know how to write an accent on his keyboard... It is not a problem for searching as the search-function in wikipedia ignores accents, as far as I can see.. But if someone writes a link into an article it will not connect if the lemma is with accent and no redirect in place. Kipala (majadiliano) 06:26, 3 Mei 2015 (UTC)

RE:Makala ya Wiki - FIFA

Salaam. Haya, nimesawazisha tayari. Lakini mzee wangu unawaza sana. Dawa yake ndogo mno. Ni kunakili maelezo makala mengine ambayao tayari yamo kwenye orodha na kuyachukua kama mfano tu, kisha unasongesha! Halafu unarudi kwenye Wikipedia:Makala ya wiki na kuongeza idadi. Pole sana.. Nimeiona FIFA. Ngoja nitazame tena.--MwanaharakatiLonga 08:35, 29 Mei 2015 (UTC)

Ndugu Kipala, salaam. Nimeanza kuchoka na Silausi alivyochoka pia Ndg Muddyb. Huyo Silausi akiendelea kubadilisha makala bila kufuata mashauri yetu na kanuni za Wikipedia:Umaarufu, nitamzuia kwa muda kadhaa. Bahati mbaya inaonekana kama ataanzisha akaunti nyingine tena alivyofanya baada ya kuzuiliwa kama Mtumiaji:Lusajo Chicharito Brown. Unaonaje? Wasalaam, Baba Tabita (majadiliano) 16:41, 29 Juni 2015 (UTC)

Sina muda mwingi siku hizi, samahani. Sijui kama itasaidia kufuta makala zake kadhaa; machoni pangu ni sawa kumpa muda wa siku 3 kujibu swali kuhusu umaarufu au kusahihisha halafu kufuta kama umbo ni tatizo. Kama hachoki naona a) kumwonya tena asianzishe kitu tena bila kuwasiliana, b) kwenda juu (sina uhakika kwa nani) na kumwomba steward kumfunga . Lakini labda rahisi zaidi kumpa muda halafu kufuta makala kadhaa na kuona kama anachika badala kuingia kwanza katika majadiliano marefu na masteward. Kipala (majadiliano) 18:51, 29 Juni 2015 (UTC)

Kumbe amejibu hapa Wikipedia:Makala_kwa_ufutaji#Omben_Gerod_Ngogo. Kama anaanza kujibu naona . Unaonaje?Kipala (majadiliano) 19:16, 29 Juni 2015 (UTC)

Arusha

Kipala vipi ndugu yangu..samahani kwa makosa yangu sikuwa nimesoma wikipedia mwongozo..bado najifunza.Maneno mengine ni vigumu kupata tafsiri yake hapo ndo natumia google translate lakini kwa neno moja moja tu...tuzidi kusaidiana. 178.156.230.129 13:00, 23 Julai 2015 (UTC)

Ningekushukuru ikiwa unaweza kuzaidia kurekebisha ukurasa wa Botswana. Niliwahi kujaribu kuongeza information walakini nikawa kufanya makosa na sahisi ukurasa huo huonekani vizuri. Nakushukuru. 178.156.230.129 13:00, 23 Julai 2015 (UTC)

Ndugu, hongera kwako na kwa wenzetu wengine kwa kuchangia kufanya Kiswahili kuwa lugha ya Afrika yenye kurasa nyingi zaidi! Tumepiku Afrikaans! Tuendelee hivi kukuza lugha yetu! 178.156.230.129 13:00, 23 Julai 2015 (UTC)

Nimeongeza pendekezo lingine kwenye makala ya Uingereza, na kutoa mawazo kwenye ukurasa wa majadiliano. Ni kweli kwamba hii si jambo rahisi! 178.156.230.129 13:00, 23 Julai 2015 (UTC)

Salaam kutoka Ulaya. Nimejaribu kuongeza kigezo cha jaribio kama nilivyoeleza kwenye ukurasa wa jumuia. Sijapata 'feedback' kwa hiyo siwezi kumaliza shughuli. Umewahi kutoa mawazo kuhusu mada hii kwa hiyo nimeona vyema nikuulize unisaidie kwa kutoa mawazo tena. 178.156.230.129 13:00, 23 Julai 2015 (UTC)

Salaam. Kwa niaba ya Mzee Kipala, nitakusaidia.. Wapi umekwama? Wako, Muddyb au,--MwanaharakatiLonga 14:40, 23 Julai 2015 (UTC)
Habari, niko safari siku hizi hivyo nina muda mara chache tu kuangalia wikipedia. Je wewe u nani? Maana mambo haya yote umeandika lakini ulisahau kujiandikisha. Mimi nashindwa kuelewa umechangia nini au uliweka maswali yako wapi. Naomba utaje tena makala ulipojaribu kuchangia, ikiwezekana kwa njia kiungo hapohapo. Nafurahi tukipata nafasi ya kushauriana na kusaidiana. Kipala (majadiliano) 20:33, 24 Julai 2015 (UTC)

newsgroups.derkeiler.com/Archive/Soc/soc.culture.greek/2009-06/msg00015.html

Hello everyone!

I believe it was about time I told everyone in the world about myself. My name is Lukas Pietsch and I specialise in English Linguistics. Instead of spending my time conducting research, I edit wikipedia articles all day (sometimes even a hundred of them a day)! I am a wikipedia administrator and I go by the user name Future Perfect at Sunrise. I am very interested in Balkan politics, so I often argue against the use of scholarly sources, misquote other people's work and misrepresent historical facts in order to push my view in wikipedia. That is so cool! I honestly feel that I should never have been born a German as my heart trully lies with the former Yugoslav Republic of Macedonia. I even find myself arguing that the ancient kingdom of Macedonia was never Greek!

Here is a link to my facebook account in case you want to check out more:

http://www.facebook.com/lukas.pietsch

Yours truthfully,

Lukas Pietsch

PS: Peace out to the suckers funding my research! I bet you had no idea of how I've been using the time you've been paying me for!

PPS: I am including links to my university and wikipedia websites: http://freenet-homepage.de/LukasPietsch/ http://en.wikipedia.org/wiki/User:Future_Perfect_at_Sunrise

Lukas , sina uhakika kama ni lazima sana kwa dunia kukujua. Hata hivyo ubarikiwe, umetuambia na sasa ishi kwa amani. Kipala (majadiliano) 11:58, 9 Agosti 2015 (UTC)

Makala za mamalia

Muddyb na Kipala, salaam. Nawaandikia tena kuhusu rafiki yetu Mjanja. Ameanzisha makala nyingi kuhusu mamalia ambao hawatokei Afrika. Pengine naweza kukubali majina anayotumia, lakini kuna mengine ambayo ameyabuni kabisa au anayatumia kwa njia mbaya. Sidhani ni mzuri kama msemaji asiye mwenyeji anabuni majina mapya. Tafadhali hii ifanywe na wataalamu wa kienyeji. Majina nisiyoyakubali ni yafuatayo:

Mnajua wataalamu (wanazoolojia) ambao watakubali kubuni majina ya wanyama haya kwa Kiswahili? Zamani nimeandikia wanazoolojia katika Tanzania na Kenya, lakini hakuna mtu aliyejibu. 107.167.91.251 15:56, 7 Agosti 2015 (UTC)

Ulisahau kujiandikisha - ni ChriKo, sivyo? Basi Mjanja hajaonekana tena kwa miaka 3 (tangu 2012). Basi hapa ni wikipedia, tena ya Kiswahili, ChriKo ni mtaalamu wetu wa viumbehai, nenda ukachinje. Hapa Majadiliano_ya_mtumiaji:Mjanja#Animal_names alitaja mweyewe vyanzo vyake pamoja na mawazo kuhusu majina badili. Niseme kweli sijui kufanya nini kuhusu wanayama walio mbali kabisa na utamaduni na mazingira wa Afrika ya Mashariki. Naona kimsingi njia ya kuunda makala kwa kutumia jina la kisayansi ni bora halafu kuongeza viungo kama majina (hata kama si kawaida) yanapatikana katika tovuti au vitabu kwa Kiswahili hata kama si kitaalamu (na hapa tunaweza kuona "biva", "pengwini" n.k. Kipala (majadiliano) 23:41, 7 Agosti 2015 (UTC)
Salaam. Ninaunga mkono hoja ya Mzee Kipala. Viumbe vingi vya namna hiyo havipatikani Afrika Mashariki. Kheri tubaki na jina la kisayansi tu. Wenu--MwanaharakatiLonga 06:31, 8 Agosti 2015 (UTC)
Gila monster - Dubwana-gila ni kukosa. 107.167.91.240 17:53, 8 Agosti 2015 (UTC)
Ukikubali kujitambulisha, tutaweza kuzungumza kuhusu mada hii. ChriKo (majadiliano) 22:58, 8 Agosti 2015 (UTC)
Mimi nina bila majina. 107.167.91.202 09:00, 9 Agosti 2015 (UTC)
Basi afadhali ujiandikishe. Kiungwana tu. Wasalaam Kipala (majadiliano) 12:00, 9 Agosti 2015 (UTC)

Makala za Wabunge wa Tanzania

Kuhusu kuingiza habari za miaka ya ubunge kwa kila mbunge: Inaonekana ni lazima kutumia tovuti rasmi ya Bunge la Tanzania. Sasa, sioni njia kuingiza habari hizo moja kwa moja - au una wazo lingine? Wasalaam 162.213.252.44 18:32, 8 Agosti 2015 (UTC)

Asante kwa ujumbe. Lakini samahani nikiuliza: wewe u nani? umejiandikisha? Kama la tafadhali ufanye hivyo. Halafu tushauriane. Kipala (majadiliano) 22:01, 9 Agosti 2015 (UTC)

Mafuriko Tanzania Jamani uniiraaaah!!!

Kipala salam, wenzenu huku mjini Dar es Salaam na baadhi ya mikoa ya Tanzania tuna hali mbaya vibaya mno. Kuna mvua inaendelea kunyesha kwa kasi ya ajabu na mafuriko hadi sasa yauwa na kuharibu majumba kibao hakuna mfano. Chakusikitisha, bado haijasimama. Inaendelea kuleta ladha ya vifo kwa wakazi wa Tanzania. Mtuombeee huko!!!! Wenu! 131.103.139.76 07:46, 17 Agosti 2015 (UTC)

We Babu hayo mafuriko yapo wapi? Mbona sijaona hata katika taarifa ya habari? Habari hii si sahihi...--MwanaharakatiLonga 11:58, 17 Agosti 2015 (UTC)

Mafuriko Tanzania Jamani uniiraaaah!!!

Kipala salam, wenzenu huku mjini Dar es Salaam na baadhi ya mikoa ya Tanzania tuna hali mbaya vibaya mno. Kuna mvua inaendelea kunyesha kwa kasi ya ajabu na mafuriko hadi sasa yauwa na kuharibu majumba kibao hakuna mfano. Chakusikitisha, bado haijasimama. Inaendelea kuleta ladha ya vifo kwa wakazi wa Tanzania. Mtuombeee huko!!!! Wenu! 131.103.139.76 07:46, 17 Agosti 2015 (UTC)

Pole sana mwenzangu. Kama ni vile ni kweli hali ya kusikitisha. (je umemaanisha ?) Ila tu sina uhakika kama tatizo kuu ni mvua kunyesha au zaidi uharibifu wa mazingira (kukata miti kunapunguza uwezo wa udongo kupokea maji ya mvua = kuongezeka kwa mafuriko) pamoja na uzembe wa watu na serikali (kujenga kwenye njia asilia za maji wakati wa miaka ya mvua kidogo, kuvumilia ujenzi huo). Kwa namna yoyote ni balaa. Kipala (majadiliano) 12:12, 17 Agosti 2015 (UTC)
Ndiyo, haya. 162.218.113.38 15:34, 17 Agosti 2015 (UTC)
Kumbe ni hii. Pole. Unakaribishwa kujiandikisha (juu kwenye skrini upande wa kulia) ma kuchangia pamoja nasi! Kipala (majadiliano) 23:37, 17 Agosti 2015 (UTC)

Ahsante

Salaam, ahsante kwa juhudi zako kwenye sw.wiki. Endelea vivyo hivyo! 131.103.139.76 07:54, 17 Agosti 2015 (UTC)

Kura juu ya utaratibu wa kuanzisha makala mapya

Salaam Kipala,

There is discussion again about allowing IP users to create articles. This was blocked for 6 months, but it is only temporary. Your comments would be welcome.

Previous discussion on the Jumuia.

Sj + 02:45, 10 Septemba 2015 (UTC)

Hatua

Ndugu zangu, hongera ninyi nyote kwa kufikia makala 30,000, kazi nzuri! Mlifanya mbio za nyika kweli. Nilisafiri kwa hivyo sikuiona sasa hivi. Tuendelee mpaka hatua ijayo: 40,000. ChriKo (majadiliano) 17:46, 24 Septemba 2015 (UTC)

Medical Translation

Could you please have a look at [24]. If the translator doesn't fix it, we need to change the captions for the infobox and do general clean-up. Lucas559 (majadiliano) 16:00, 30 Septemba 2015 (UTC)

Kipala,please look at [25]. I tried to fix the [ [ and [( issues in the translation. There was lots of improper wikicode. I choose the Swahili title, not onchocerciasis.--Lucas559 (majadiliano) 20:18, 6 Novemba 2015 (UTC)

Hi, I really don't see the need to make a distinction between this article and NSDAP. There are no other languages that make that distinction, so why do it here? All that's needed is to make it a redirect and put in one line in the NSDAP article about the name. Jon Harald Søby (majadiliano) 05:01, 14 Oktoba 2015 (UTC)

Mpendwa, jina la kawaida (=lemma, jinsi inavyopokelewa na Kiingereza) ni la ajabu kwa Kiswahili (nazi= tunda la mnazi) lakini imekuwa kawaida. Nahisi watu wengi kama wanatafuta "Nazi" kwa maana ya kisiasa/ Kihistoria hawataitambua mara moja wakifika "NSDAP". Kifupi hiki karibu hakijulikani kati ya Waswahili. Naona tuna nafasi ya kupanga makala zote mbili sioni kosa lakini msaada. Unaonaje? Kipala (majadiliano) 06:55, 14 Oktoba 2015 (UTC)
NB: just in case you don`t understand Swahili: yes, I see a reason why for Kiswahili there can be 2 entries, even if that is not the case in other langauge editions. Kipala (majadiliano) 19:32, 14 Oktoba 2015 (UTC)

sensa ya mwaka 2012

Habari za kazi ndugu, naomba unisaidie nama ya kupata takwimu ya sensa ya mwaka 2012 kwani inaniwia vigumu kubadili takwimu za sensa ya mwaka uliopita ninapohitaji kufanya hivyo, Asante!Enock John (majadiliano) 06:04, 17 Oktoba 2015 (UTC)
Sensa ya Tanzania ya 2012 inapatikana hapa: http://www.wavuti.weebly.com/uploads/3/0/7/6/3076464/census20general20report20-202920march202013_combined_final20for20printing1.pdf. Ni faili moja ya megabaiti 7. Ukitaka kuitumia mara kadhaa nashauri uihifadhi kwako. Kila kata iliyobadilishwa tayari (k.m. mikoa kama Mtwara, Iringa, Singida) ina kiungo kwenda faili hii. Kwenye ukurasa wa muda Wilaya_za_Tanzania_4 unaona maendeleo ya kazi ya kusahihisha makala za kata. Wasalaam Kipala (majadiliano) 06:42, 17 Oktoba 2015 (UTC)