Majadiliano ya mtumiaji:Lloffiwr

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Karibu sana ndugu Lloffiwr kwenye Wikipedia ya Kiswahili! Twanmfurahia kila mmoja anayejiunga nasi maana sisi ni watu wachache mno (hata kama tumefika kiwango cha makala 10,000 sasa hivi!). --Kipala (majadiliano) 08:15, 23 Februari 2009 (UTC)[jibu]

Lloffiwr, Salam! Nami pia ninapenda kukukaribisha kama jinsi alivyofanya Bwana Kipala! Karibu sana Uswahilini.--Mwanaharakati (Longa) 06:23, 24 Februari 2009 (UTC)[jibu]

Ukurasa mpya wa mwanzo[hariri chanzo]

Lloffiwr, salaam! Haya, ukurasa mpya wa Wikipedia ya Kiswahili, leo hii umefikia siku yake!!! Nimebadilisha tayari. Ahsante kwa ushirikiano wako. Wako kijana, Muddyb, au,--Mwanaharakati (Longa) 12:56, 20 Juni 2009 (UTC)[jibu]

Nimemteua Flowerparty achaguliwe kuwa mkabidhi pamoja nasi. Naomba upige kura kwenye ukurasa wa Wakabidhi. Ahsante! --Mwanaharakati (Longa) 10:32, 9 Julai 2009 (UTC)[jibu]

mradi wa Google kwa ajili ya wikipedia yetu[hariri chanzo]

Bwana Lloffiwr, salaam!
Nimepata mawasiliano kutoka Christine Moon huko Palo Alto, California. Yeye anafanya kazi kwa shirika la Google, nao wameanza kupanga mradi au huduma kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Tanzania na Kenya ili waelimishwe kuandika makala kwa wikipedia ya Kiswahili. Kumbe!
Christine sasa ametualika kumwandikia maoni yetu, angalia tovuti hiyo:
http://docs.google.com/Doc?docid=0AbIPJ9Nv6udZZGd6MndwcGdfMzFkODNzOG0zYw&hl=en
Bahati mbaya yeye haelewi Kiswahili, kwa hiyo itakuwa lazima kumwandikia kwa Kiingereza. Asante kwa michango yako!
Ni wako katika ujenzi wa lugha yetu, --Baba Tabita (majadiliano) 08:14, 10 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]

Asante kwa mchango wako. Nimeuingiza humo. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 10:06, 26 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]

majadiliano kuhusu utafsiri wa istilahi[hariri chanzo]

Bwana Lloffiwr, salaam! Nimeanzisha majadiliano mapya kuhusu utafsiri wa istilahi ya wikipedia yetu hapa. Naomba uyaangalie na kuchangia maoni yako. Asante! --Baba Tabita (majadiliano) 09:43, 23 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]

Uchaguzi Mpya[hariri chanzo]

Salam, Dada. Unaombwa upige kura katika ukurasa wa wakabidhi wa Wikipedia. Mmoja kati ya wachangiaji wenzetu (Mr Accountable amejiteua kuwa mkabidhi! Ili kumpgia kura, tafadhali fungua hapa. Ahsante sana.--Muddyb MwanaharakatiLonga 18:30, 28 Novemba 2009 (UTC)[jibu]

Uso mpya[hariri chanzo]

Salaam nikielewa vema unazoea kule Meta, sawa? Naomba usaidizi nikijaribu kujua nani ni mhusika katika badiliko la uso wa wikipedia. Yaani hatujaulizwa , tatizo kubwa ni inabatilisha sehemu za mwongozo na kurasa za msaada kwa watumiaji wapya. Picha si sahihi tena, muundo wa ukursa ni tofauti wa hiyo maelezo kama "dirisha upande wa kulia/kushoto - juu/chini" mara nyingi si sahihi tena. Hii tatizo hasa sasa kwa sababu tunayo tena madi wa kuandika makala za afya kwa kukusanya wauguzi huko Kenya na TZ, wote ambao hawakutumia wikipedia bado. Unamjua mtu anayeweza kusaidia? Kipala (majadiliano) 19:45, 17 Septemba 2010 (UTC)[jibu]

Nimeuliza taratibu ya usability project walioweka uso mpya katika kila wiki wa WikiMedia Foundation kule meta, kwa mtu ninayemfahamu kidogo. Lakini sidhani kwamba watakuwa tayari kurudisha katika uso ulivyokuwa. Nafikiri kwamba ni nzuri kutokuwa tofauti sana na wiki zingine, kwa sababu utengenezaji wa wiki utakuwa vigumu kama tupo tofauti sana na wengine. Ukitaka kuwasiliana na usability project wenyewe wako hapa. Tatizo hasa ni kuzoea uso mpya na kuandika kurasa za msaada haraka shauri ya mradi mpya, sivyo? Nitauliza kama wataweza kuandika mwongozo fupi kwa ajili ya watumiaji wapya kule usability project, itusaidie kuandika upya Kiswahili. Lloffiwr (majadiliano) 12:23, 22 Septemba 2010 (UTC)[jibu]

Naona umeweka ilani kwenye mwogozo. Lakini kwa bahati mbaya si kweli jinsi unavyoandika ya kwamba unaweza kuchagua uso wa mono ya awali. Hii naona u nikiingia katika de.wikipedia. Kwetu tunapata mchanganyiko wa mono na vetor. Sijui kwa nini. Nimedokeza tatizo hili kwa watu mbalimbali lakini sikupata jibu wala kutoka kwako! Pamoja na hayo unaamini ya kwamba mtumiajimpya ataelewa maneno kam "mono" na "vektor"? Hali halisi badiliko hililimeleta fujo tu kwetu. Naogopa hatuna uwezo wa kubadilisha lakini ni wazi hapa kuna kitu kinachofanana na ufalme au udikteta kidogo basi ni kuvumilia tu. Kipala (majadiliano) 20:04, 26 Septemba 2010 (UTC)[jibu]
Tafadhali ubadilishe ilani tena kama unavyoona ni vyema - nakubali kwamba maneno kama mono na vector ni vigumu kuvielewa. Nafasi ya kusaidia kuandika kurasa za msaada sina wakati huu. Umesema kwamba tuna mchanganyiko wa mono na vector - hii sijaelewa; labda unaweza kueleza kwa ndani? Lloffiwr (majadiliano) 22:06, 26 Septemba 2010 (UTC)[jibu]


Kura ya kuamua juu ya wakabidhi waliopotea[hariri chanzo]

Karibu kutembelea ukurasa wa wakabidhi na kuamua juu ya wenzetu waliopewa haki za wakabidhi lakini hawakuonekana tangu miezi mingi: Wikipedia:Wakabidhi#Kura_ya_kuondoa_wakabidhi_waliopotea. Tuliwahi kujadili swali hili mwaka uliopita (tazama kwenye ukurasa unaotajwa, juu ya pendekezo) ; sasa njia imeonekana. Kipala (majadiliano) 05:27, 1 Oktoba 2010 (UTC)[jibu]

Pendekezo kuhusu utaratibu wa kuanzisha makala kwa watumiaji waliojiandisha pekee[hariri chanzo]

naomba usome hapa na fanya uamuzi wako: Wikipedia:Jumuia#Pendekezo:_Utaratibu_wa_kuanzisha_makala Kipala (majadiliano) 14:57, 26 Novemba 2012 (UTC)[jibu]

Wiki Indaba conference[hariri chanzo]

Salaam, Lloffiwr. Kuna mpango wa mkutano mjini Johannesburg mwezi wa pili mwakani, angalia http://wikiindaba.net/index.php?title=Main_Page - pia, umeombwa kujibu maswali yao kwenye tovuti la Google docs: https://docs.google.com/forms/d/1zEk6hw4IiQYVrdJGYphPhQHOQFi4wdOIXvzVj9vy_gU/viewform Asante kwa msaada wako. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 11:05, 5 Novemba 2013 (UTC)[jibu]

Salaam. Umejaribu kujibu maswali yao?--MwanaharakatiLonga 15:19, 9 Novemba 2013 (UTC)[jibu]

Harakati zipo?[hariri chanzo]

Salaam, dada. Kimya sana. Je, harakati zinaendelea kama zamani?--MwanaharakatiLonga 15:19, 9 Novemba 2013 (UTC) [jibu]

Umelala, dada.. Haya, tuongee baadaye!--MwanaharakatiLonga 15:36, 9 Novemba 2013 (UTC)[jibu]

Naomba ushirikiano wako![hariri chanzo]

Mpendwa, nakuomba uangalie baada ya siku 2,3 kurasa hizi mbili:

1. Wikipedia:Wakabidhi#Kusafisha_orodha_ya_Wakabidhi_mwaka_2014
2. Wikipedia:Ukurasa_wa_jumuia#Wiki_Indaba_2014

Kuhusu 1) napendekeza kuwachagua wakabidhi wapya na kuondoa wale waliomo katika orodha ya wakabidhi lakini hawakuwepo tangu miaka 2.

Kuhusu 2): nahitaji msaada na mawazo yenu. Nitashiriki kwenye mkutano wa Wikimedia mwezi wa Juni. Inaonekana mimi ndipo mchnagiaji wa pekee kutoka Wikipedia yetu. Ninajitahidi kupeleka mawazo ya jumuiya yetu. Naomba michango!

Nitaongeza karibuni mawazo yangu kuhusu mambo ninayoona kuwa na maana kwa mtazamo wangu. Ujumb huu natuma kwa wachangiaji wanaoonekana katika orodha ya wachangiaji hai waliochangia zaidi ya mara 3 katika siku 30 zilizopita!

Ndimi wako Kipala (majadiliano) 20:25, 13 Mei 2014 (UTC)[jibu]

Kupakia mafaili, Sogora ya kupakia?[hariri chanzo]

Wikimedia Commons logo

Hello! Sorry for writing in English. As you're an administrator here, please check the message I left on MediaWiki talk:Licenses and the village pump. Thanks, Nemo 19:22, 18 Septemba 2014 (UTC)[jibu]