Majadiliano:Majira ya kupukutika majani

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sijui kama inafaa kweli kutumia "masika" kwa ajili ya majira nje ya tropiki. Nikielewa vema tabia kuu ya masika ni mvua, na katika tropiki mvua inamaanisha kipindi cha kuotea kwa mimea. Lakini jambo kuu ni mvua, nisiopokosei. Nikiangalia kamusi ya Madan-Johnson, huko wamelinganisha masika na "autumn" kwa sababu inafuata kipindi cha joto. Kipala (majadiliano) 19:48, 8 Mei 2015 (UTC)[jibu]

Umejijibu tayari. Ni kweli majira ya Ulaya na huku kwetu ni tofauti, ndiyo maana nimeyataja kwa mzunguko, lakini kamusi nyingine zinalinganisha masika na autumn. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:07, 13 Mei 2015 (UTC)[jibu]
Ninakubali na ninyi nyote. Majira ya hapa na ya huko Ulaya ni tofauti. Na ukitumia masika kwa majira ya Ulaya haieleweki ni gani. Wengine wanasema ni autumn, wengine ni spring. Wengi wanasema kwamba autumn ni sawa na demani. Kwa hivyo, katika makala hii, tutatumia demani au masika? ChriKo (majadiliano) 14:00, 21 Desemba 2022 (UTC)[jibu]