Mtumiaji:Kipala/Archive 3

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Archive Hii ni ukurasa wa Hifadhi ya Majadiliano ya Awali. Usihariri ukurasa huu usiongeze wala kupunguza kitu.
Ukitaka kujadiliana upya mambo yaliyomo humo nenda kwa ukurasa wa majadiliano ya sasa.

Samahani

Kipala, salam. Ndugu naomba niswamehe kwa kuhamisha maelezo yako ya awali katika Kumbukumbu ya Archive-2 bila ya idhini yako. Nilikuwa naona shida wakati wa kuanzisha ujumbe mpya katika kurasa yako ya majadiliano, hivyo nikaone bora niipunguze kwa njia ya kuijaladia!! Natumai utakuwa umeniswamhe kwa hili, kazi njema...--Mwanaharakati (talk) 15:45, 12 Februari 2008 (UTC)

Template:Muigizaji

Kipala, salam. Template:Muigizaji, imepatwa na matatizo kidogo. Sijui ni kwanini imekuwa vile ilivyo sasa, lakini hamna mtu aliyetia mkono wake zaidi ya siye wenyewe toka hapo awali. Labda unaweza kuitazama na kuitafutia ufumbuzi. Naomba ichunguze kisha ikinge kabisa...--Mwanaharakati (talk) 16:43, 13 Februari 2008 (UTC)

Basi. Naona kuna msiba wa template zote kwa ujumla. Huenda kukawa na tatizo huko makao makuu ya mradi mzima, maana kila template ninayoigusa naona inakasoro (sielewi na naona kuna ugonjwa wa kifafa kwa template). Tuvute subra labda kuna tatizo kwao!!--Mwanaharakati (talk) 16:51, 13 Februari 2008 (UTC)

Pole sana. Kabla sijaanza kuiangalia - labda hii: nimeona majina ya amri na maelezo mengi yamebadilika kuwa kiswahili badala ya Kiingereza. Sijui kama hapa panya amejiingiza. Ingetosha amri moja ndogo isiyoeleweka tena na basi. Unaonaje? Nitaangalia siku hizi lakini si leo.--User_talk:Kipala 17:56, 13 Februari 2008 (UTC)

KICHEKO. Si mwigizaji wala ya nchi-mto, uainishaji nk. Zote zikomatatani. Kifupi ni msiba wa kitaifa, maana hakuna kilichokaa sawa. Ndugu, hii si ni hatari isiyo na kifani? Iweje template zote ziwe lemavu pasisipo na sababu? Nakumbuka nilimpelekea Marcos baadhi ya pendekezo ya kubadilisha lugha katika sw:wiki, natumai kazi hiyo atakua kesha ianza na ndiomaana lile neno lililo andikwa "Viungo viungacho ukurasa huu" naona hamna. Labda nimwendee tena na kumweleza juu ya tatizo hili au unaonaje?--Mwanaharakati (talk) 07:27, 14 Februari 2008 (UTC)

Mimi naona templeti zote ni sawa kabisa kama kawaida. Kuna uwezekano tatizo iko kwenye mashine yako tu. Haya yanaweza kutokea. Pole. --User_talk:Kipala 09:20, 14 Februari 2008 (UTC)

Bado nabisha. Angalia Ujerumani kisha Aseniki, utaona kama kuna tatizo. Labda kwako hizi nazo zitaonyesha kasoro, endapo hizo kwako zita kaa sawa basi ujue kwangu kweli kua kasoro... nategemea jibu lako..--Mwanaharakati (talk) 11:26, 14 Februari 2008 (UTC)

Zote mbili kwangu sawa. Labda tatizo ni dogo. Nadhani tatizo ni mashine yakotu.Kwa hiyo usisikitike. Unaweza kuendelea kama awali. Ukiwa na mashaka basi nieeleze tatizo unachoona ni nini halafu nitakuambia imetokea namna gani.--User_talk:Kipala 12:51, 14 Februari 2008 (UTC)

Naomba angalia hii: Ukiitzama kwa mbali yaonysha template imekaa kulia na haina mzunguko wa kuizungushia (yaani border iko sufuri. Naomba nisaidie..

Template imekaa kushoto wakati kawaida template inakaa kulia. Inakuwaje?

Naona kwangu kama ni balaa kubwa!!--Mwanaharakati (talk) 13:17, 14 Februari 2008 (UTC)

Re:Kucheza kwa template

Salam. Naona faraja baada ya kuona na wewe umeharibikiwa (tehe tehe tehe-kicheko). Sikuwa najisikia vizuri pale nionapo kasoro zile katika Kompyuta yangu tu, na ndiomaana nilikuwa nalia kwa-kuwa ulikuwa unaniambie mashine yangu kimeo. Naona sasa tatizo lisha fika hadi huko Ujerumani uliko. Subra yahitjika. Lakini mie kuunda makala bila ya template (najihisi kama bado mtoto?? Au??) Hapendezi kwa makala ninazo changia!! Ila pole na wewe kwa ugonjwa wa kifafa cha template!! Kazi njema...--Mwanaharakati (talk) 14:18, 15 Februari 2008 (UTC)

Naomba msaada

Salam. Naomba nisaidie kutafsri neno hili (wagonload) kwa Kiswahili kilicho kizuri na kitasaidia kuleta maana nzuri. Wagonload, najua kama ni wale Farasi walio na kijumba nyuma (ama sivyo?) Kwa Kiswahili kilicho sahihi sipati maana nzuri, kwa hiyo naomba nisaidie kuswahilisha neno hili... Nategemea majibu yako.--Mwanaharakati (talk) 04:54, 16 Februari 2008 (UTC)

Neno lenyewe lataja mzigo (load) wa gari (wagon) moja. Sasa itategemea na sentensi. --User_talk:Kipala 08:39, 16 Februari 2008 (UTC)

Haya basi sentensi yenyewe hii hapa: Set in Mexico under the rule of Emperor Maximilian I, Sabata is hired by the guerilla leader Señor Ocaño to steal a wagonload of gold from the Austrian army. Kazi kwako mkubwa...--Mwanaharakati (talk) 11:12, 16 Februari 2008 (UTC)

Sabata amejiriwa na ... kupora mzigo wa dhahabu mali ya jeshi la Austria unaosafirishwa kwa gari la farasi - ingawa siamini ya kwamba ilikuwa mali ya jeshi la Austria. Kaisari Maximilian alikuwa Mwaaustria lakini aliweka huko na Wadfaransa alitegemea jeshi la Ufaransa. Sijui kosa la filamu au kosa la makala unayotafsiri. --User_talk:Kipala 12:19, 16 Februari 2008 (UTC)

Aksante. Jana ilikuwa Ijumaa, lakini huku badilisha ukurasa wa usoni, vipi hukupata muda au?..--Mwanaharakati (talk) 13:07, 16 Februari 2008 (UTC)

Daraja la Lugha

Salam. Nimevumilia nimeshindwa. Sasa nakupa pongezi kwa kuwa Mswahili huria aliye na kiwango cha mzawa wa lugha ya Kiswahili, au unaonaje? Nimebadilisha Language Status: Kutoka daraja la tatu hadi (fasaha). Kiwango ulicho nacho kimevuka daraja la tatu, hivyo nisingepnda kuona tena upo katika daraja la tatu. Katika wiki hii (na hata miezi kadhaa nyuma) nimekuwa mtu wa kushangaa vile unavyoandika Kiswahili safi na murua kuliko kile ninacho andika mie niliyezaliwa huku!! Je huoni hiyo sifa na faraja kubwa kumpita mwenye Lugha? Basi kila lakheri na hongera kwakuwa na Kiswahili bab-kubwa...--Mwanaharakati (talk) 16:20, 18 Februari 2008 (UTC)

Asante Muddy una moyo mzuri. Isipokuwa tena naona nishushe cheo hiki kidogo. Yaani bado sentensi zangu mara nyingi za Kijerumani. Makosa yako ni tokeo la kujua Kiswahili vizuri. Mimi napaswa kuchagua maneno polepole zaidi kwa sababu mara nyingi siyajui hivyo nachungulia kamusi ninapopata maneno mazuri. Halafu ombi hili: Hata ukiona sifa ukiwa sasa mkabidhi ni muhimu kukumbuka kutoingilia ukurasa wa binafsi. Kuandika kwenye ukurasa ya majadiliano sawa. Ukurasa wa binafsi kamwe. Sisi tunaelewana lakini mmtu mwingine anaweza kukushtaki na hutakuwa cha kusema. --User_talk:Kipala 19:18, 18 Februari 2008 (UTC)

Siku zote mtu hajijui bali hujuliwa!! Mie binafsi nimeona kiwango chako cha lugha ni cha juu kuliko, wewe unasema bado ni kidogo (sio kweli) kama unasema sentensi zako ni Kijerumani, mbona naona unaandika Kiswahili safi? Ama wewe mwenyewe hujiamini? Haifai kumvunja moyo mtu. Mimi kama mimi toka nije hapa nimetokea kukubali sana lugha yako wakati wa uhandishi (na hata maelekezo) yako yapo SUPERB, vipi wewe useme bado??? Basi sawa nimekuelewa!! Kazi njema...--Mwanaharakati (talk) 05:46, 19 Februari 2008 (UTC)

Tatizo la mwundo wa wiki

Salam. Naona hii sio hapa tu hata huko en:wiki na simple:wiki, pia kuna tatizo. Baada ya kucheza kwa template, kukawa na upotevu wa kifaa cha kufanyia kazi (REDIRECT button) sasa hakipo tena. Hicho hakipo katika wiki zote, sio sw:wiki, simple:wiki wala en:wiki. Nahisi ni msiba mkubwa kabisaaa... Katika en:wiki kulikuwa na vitufe kibao vya kufanyia kazi, lakini leo hii vimebaki kuwa sawa na vya sw:wiki!! Nilivyoona hivyo tu, nikagundua kwamba huu mtihani ni wa taifa zima la mradi wa wiki. Huenda wenyewe wakawa hawajui kama kuna tatizo kama hili. Huenda wakawa hawajui kama kuna mapungufu ya vitufe vya kufanyia kazi. Sasa tutafanyaje ndugu yangu? Maana habari ndio kama nilivyokeleza, tafakari!!..--Mwanaharakati (talk) 13:29, 19 Februari 2008 (UTC)

Kimbunga

Unaweza kunielezea Hurricane kwa lugha nyingine mbali na Tufani? Nina mpango wa kutafsiri makala Hurricane Wilma na Hurricane Katrina, kwa maana ya Kimbunga cha Katrina na Kimbunga cha Wilma. Nikiandika neno "Kimbunga" kwa lengo la kupata maana zaidi ya moja naona sipati, inakuja hii moja tu ya Kimbunga lugha ya wabantu!! Sasa nifanyeje? Mimi nilikuwa sijui kama Kimbunga ni lugha. Nilikuwa najua Kimbunga ni upepo mkali unaotoka usawa wa bahari na kuelekea nchi kavu. Kuna kipindi kunaweza kukawa na Kimbunga wakati wa mvua nyingi ziambatanazo na upepo mkali, pia huwa tunaita Kimbunga. Je unalipi la kusema juu ya hili?--Mwanaharakati (talk) 13:46, 19 Februari 2008 (UTC)

Nilianza makala ya "tufani" baada ya kushauriana na kamusi. Kamusi ya TUKI ina maneno haya mawili tufani na kimbunga. Nadhani wewe utajua kuliko mimi jinsi mnavyotumia maneno huko Dar. Hapa unaona udhaifu wa lugha yangu: siwezi kumwuliza mtu na kutofautisha kati ya maneno katika kamusi. Nikichungulia sasa tovuti naona kweli Kimbunga chafaa zaidi. Nikielewa vema sasa "tufani" itakuwa dhoruba yenye tabia ya kuzunguka (umbo la tufe..) kwa jumla. Kwa hiyo kimbunga ni tufani inayoanza baharini katika kanda ya tropiki (majina ya kimataifa hurikan/hurricane (Karibi), taifun/typhoon (Pasifiki), au saikloni/"cyclone" kwa jumla). Unaonaje? "Kimbunga" nimeshahamisha "Kimbunga (lugha)". Sasa usome tufani halafu uniambie kama nibadilishe makala hiyohiyo kuwa "kimbunga" . Tufani naweza kutumia kwa aina hizi za dhoruba kwa jumla ama baharini au barani. --User_talk:Kipala 20:35, 19 Februari 2008 (UTC)

Kimbunga ni lugha zoefu katika jamii yetu. Tufani ni jina geni sana midomoni mwa watu. Labda watu wa pwani wanaweza wakawa wanajua kama tufani ni kimbunga. Turahisishe: tuweke maana zaidi ya moja katika makala ya "Kimbunga" na mtu atakuwa na hiari yake ya kwenda katika makala ya Kimbunga (lugha) au katika Katrina-Wilma. Au waona vipi?--Mwanaharakati (talk) 06:00, 20 Februari 2008 (UTC)

Majibu ya tatizo la format ya template

Salam. Ndugu, ushapitia kule katika MetaWiki? Basi angalia majibu haya hapa...--"Mwanaharakati" (talk) 18:05, 20 Februari 2008 (UTC)

Basi imerudishwa - template ni sawa (nilipaswa kufyeka kumbukumbu ya mashine kwa "ctrl-shft-r" hadi kuiona). Nimemwomba Malanagli aeleza kusudi lake la kuondoa data hii nadhani alitaka kuswahilisha amri zetu. --User_talk:Kipala 18:46, 20 Februari 2008 (UTC)

Hongera kwa kazi yako.. Tumejikwamua na tatizo hili la kucheza kwa template.. Una-stahili pongezi kwa kazi yako ulioifanya..--"Mwanaharakati" (talk) 05:47, 21 Februari 2008 (UTC)

Ziwa nyassa

Kipala, salam. Husika na kichwa cha habari hapo juu ni makala au kurasa ya kuelekeza, yaani, REDIRECT? Naona imetokea katika sehemu ya kurasa mpya!! Labda niulize ili nipate kujua, a)(b. Je ni sahihi ulivyoandika Ziwa Nyassa? Yaani, kwa-kuweka SSA badala ya SA tu. Nauliza tu, sijui lolote juu ya Nyasa au Nyassa!! Siku njema..----"Mwanaharakati" (talk) 11:13, 23 Februari 2008 (UTC)

Muddy, swali ni zuri ingawa sijaelewa sehemu a). Kuhusu b: Nyasa ni sawa. Redirect hii ni uwivu upande wangu. Nje ya Kiswahili tahajia "nyassa" ni kawaida. Nikiandika makala naona makosa kama haya huingia. Hapa naona mara kwa mara niweke redirect kwa umbo sahihi nikihofia nitarudia kosa lilelile. Katika wikipedia kubwa yenye wachangiaji wengi makosa huondolewa haraka. Hapa kwetu tukiwa wachache kosa linaweza kukaa kwa miaka na miaka. Pia mazingira ya wasomaji wetu tahajia labda si nguvu hasa. Basi ni haya tu, sijui kama njia inafaa. --User_talk:Kipala 11:27, 23 Februari 2008 (UTC)

Hiyo kurasa nimeikuta umeiandika: redirect halafu [[Ziwa Nyassa]], badala ya #REDIRECT kurasa... Basi kurasa haija-redirectiwa, badala yake imekuwa kurasa mpya!! Nilivyoona hivyo nikaweka zile alama za kuifanya kurasa ielekezwe kule sehemu husika!! Natumai umeelewa ama sivyo?--"Mwanaharakati" (talk) 11:44, 23 Februari 2008 (UTC)

Sielewi namna gani imetokea lakini asante kwa kusahihisha. --User_talk:Kipala 12:05, 23 Februari 2008 (UTC)

Vitufe vya kufanyia kazi

Kipala, salam. Nimejaribu kumwuliza bwana Pathochilds kuhusu kuongeza baadhi ya vitufe katika wiki yetu. Hapo awali kulikuwa na vitufe kadhaa, lakini kwa sasa naona hamna. Jamaa akatoa ushauri wake namna ya kufanya ili vitufe virudi na vitaongezeka baadhi kama zilivyo wiki zingine zilizo kubwa. Katika jaribio hilo naona nilifeli kwakuwa jaribio la taka mtu aliyemkabidhi ndio afanye kazi hiyo!! Je unaweza ukapata kajimuda kidogo ili uweze kuifanya hiyo shughuli? Endapo utakuwa na muda, basi fungua hapa!! Siku njema.....--"Mwanaharakati" (talk) 12:04, 25 Februari 2008 (UTC)

Salam. Naona nimeshafanikisha swala la vitufe vya kufanyia kazi. Naona sasa idadi ya vitufe imeongezeka! Kile kitufe kilichopotea (kitufe cha redirect) naona kimerudi na wenzake tele. Ni mimi na Steward Nick kutoka meta tulioshrikiana pamoja kuongeza vifaa hivyo. Vilevile signature. Hapo awali, hapa kwetu kulikuwa hamna ule mwundo wa mtu akimaliza kuandika ujumbe wake katika user-talk page ya mtu halafu ionyeshe ukurasa wa majadiliano wa mhusika, ilikuwa haiji sehemu yake ya majadiliano! Lakini sasa tushaweka sawa. Hamna haja ya kuweka chochote kile kwani kila kitu kisha kaaa sawa! Basi kila lakheri....--Muddyb Blast Producer (majadiliano) 06:29, 12 Machi 2008 (UTC)

Map of Tanzania

Please excuse the English, but I do not know Swahili.

I would be happy to create a map of Tanzania. However, I am not quite sure what you want. I am not sure, for example, why you don't like the map that you marked up (the sketch that you showed me). Perhaps you could show me a map similar to what you would like to see, or more thoroughly describe it. Thanks, MapMaster 03:00, 28 Februari 2008 (UTC)

I have replaced your map at Usafiri wa Tanzania with one that I created and uploaded to Commons. It looks very much like your map. I hope you like it. Let me know if you would like something changed.
By the way, how does one say "map" and "new map" in Swahili? They would be useful when I add maps here.
And finally, it would help me if you could add a few words in Swahili to my user page, letting people know that I am a mapmaker. Thanks, MapMaster 05:28, 5 Machi 2008 (UTC)
I have added the tarmac roads as you requested. Is there anything else amiss? Thanks, MapMaster (majadiliano) 17:31, 11 Machi 2008 (UTC)

Uteuzi kwa bureaucrat

Rafiki yangu, nimekuteua uwe bureaucrat mwenzangu. Nimerudi nyumbani jana jioni tu baada ya wiki nne bila kuweza hata kuingia mtandaoni. Vizuizi hivyo havimsaidii bureaucrat. Tukiwa wawili tutasonga mbele vizuri zaidi. Wikipedia nyingi zina mabureaucrat wengi zaidi kuliko mmoja tu. Naomba msaada wako. Uangalie ukurasa wa wakabidhi. Asante, na ubarikiwe! --Oliver Stegen 09:22, 1 Machi 2008 (UTC)

Pole ukiwa na hisia ya kuadhibiwa. Haikuwa lengo langu. Kwa kweli nadhani unastahili, na bora kuwa wawili kuliko mmoja. Tusaidiane kazini :-) Nitasubiri siku chache ili kuwapa wengine nafasi ya kutoa maoni yao halafu nitakubureaucratisha. --Oliver Stegen 09:14, 5 Machi 2008 (UTC)

Anahisi kama umemkulupusha kumchagua yeye awe bureaucrat. Kila sifa anazo za kuwa bureaucrat, pia anazoefu na madudu yote yaliyomo katika Wikipedia hii. Yampasa aridhie uteuzi huo uliompatia, ingawaje anaonyesha kutotaka lakini hivyo ndivyo hali ilivyo. Kwa kazi za Oliver, yeye kaona haitakuwa rahisi kushughulikia watu wote au mabot yote yatakayojiri kwa kipindi ambacho yeye hatopatikana. Ni uamuzi wa busara kwa kumchagua Kipala awe bureaucrat. Tafadhali Nd. waombwa uridhie uteuzi huu. Kila lakheri....--"Mwanaharakati" (talk) 11:49, 5 Machi 2008 (UTC)

Category za Waliokufa / -fariki

Salaam! Naomba tuendelee na jina la Category 'Waliofariki' mwaka fulani badala ya 'Waliokufa'. Asante! Wasalaam, --Oliver Stegen 18:42, 2 Machi 2008 (UTC)

Re:Makala za msingi

Salam. Naam, nimeona tofauti kubwa baina ya sisi na wa yoruba. Ni kweli kabisa kwamba wao vimakala vyao vya kihuni. Haitoleta maana kama tutakaza mwendo wa kuandika makala fupi kama zile. Kuhusu filamu na muziki: Kusema kweli mimi sijui wanamuziki-waigizaji wengi wa nchi tofauti kuliko vile ninavyojua wa Kimarekani.

Maranyingi nikiwa naangalia filamu-muziki huwa naona tu watu na kuhifidhi majini yao kisha nakuja katika yahoo search na kuanza kumtafuta huyo niliyemuona amecheza vizuri na kuukonga moyo (bila kujua kama Mwamerika ama Mjerumani). Ikitokea huyo niliyemchagua akawa Mmarekani, basi sina budi kumwandika, awe Mswizaland Mwaustralia na wengine wote.

Tukienda mbele na kurudi nyuma, film industry zilizo-kubwa, nyingi zinatoka Marekani na ndiyomaana na shindwa kuapata waigizaji wengine waliowakali na wengi kuliko Marekani. Makala za msingi: Nikiangalia mule, naona nitaweza kumaliza wanamuziki wote na waigizaji pia.

Ni kiasai cha kutulia ili niweze kupambana na makala zile za waigizaji-wanamuziki. Shukrani: Ni vyema pia kukumbushana katika ujenzi huu wiki hii (namna ya kuandika na kufikia lengo), sikujisikia vibaya eti kwanini uliniambia niende katika ukuara wa makala za msingi la. Naona ni njia moja wapo ya kutaka kuikuza wiki yetu. Basi nashukuru kwa ujumbe wako!! Ubarikiwe!--"Mwanaharakati" (talk) 07:21, 3 Machi 2008 (UTC)

Hongera kwa bureaucrat

Hongera kwa kuchaguliwa kuwa mmoja wa mabureaucrat kwa wikipedia yetu ya Kiswahili. Sina wasiwasi yoyote kuhusu kufanya kazi pamoja nawe. Ukihitaji kumsajilisha mtumiaji kama akaunti ya kikaragosi, tumia ukurasa wa kumfanya mtumiaji awe bot. Kwa sasa sina shauri lingine. Haya, twende tukaendelee na kazi. Kila la kheri, --Oliver Stegen 18:49, 9 Machi 2008 (UTC)

Pakia Faili

Salam. Sijajua tatizo ni lipi. Sisi hatujafika huko katika sehemu ya kupakizia mafaili. Lakini ngoja niangalie mafuto maalum kisha nitakujibu..--Mwanaharakati (majadiliano) 14:15, 13 Machi 2008 (UTC)

Labda utumie hii http://sw.wikipedia.org/wiki/Special:Upload kwa sasa halafu baada ya muda tutafute namna ya kuirudisha! Naona hata katika simple wikipedia nao pia wameondosha kitufe hicho cha kupakizia faili. Basi mambo ndiyo kama unavyoyaona. Kuhusu sie, hatujafanya lolote linahusiana na kiungo hiki cha kupakizia faili. Labda tutafakari kwa pamoja ili tutatue tatizo, Wasalaaaam,--Mwanaharakati (majadiliano) 15:11, 13 Machi 2008 (UTC)

Salam. Ndugu, nimejaribu kuielekeza Wikipedia:upload kwa Special:upload, lakini haelekei moja kwa moja. Inakwenda hadi katika kurasa husika kisha inasimama. Kwa-kuwa wote sasa tupo hewani, Oliver mie na wewe, ni vyema tutafakari namna ya kutatua tatizo hili. Unasemaje?--Mwanaharakati (majadiliano) 09:33, 15 Machi 2008 (UTC)

Sijui. Lakini asante kwa kujaribu. Naona kuna mahali ambako fremu ya kurasa zetu imeandikwa lakini sijui hii ni wapi. Kama umewasiliana na watu wa Meta je unapata nafasi ya kuwauliza tena? Naona kwa badiliko fulani (ninahisi ilikuwa kazi ya kutafsiri majina kwenye menu yetu) hapa "wikipedia:upload" imeingizwa badala ya "special:upload". Lakini sijui wapi na na nani? --User_talk:Kipala (majadiliano) 09:51, 15 Machi 2008 (UTC)
Samahani kwa kuchelewa kukujibu. Kulikuwa na tatizo la umeme kwa takriban masaa mawili na zaidi. Nafasi ya kuwauliza tena ipo. Lakini hili sijamwuliza yeyote kutoka meta. Labda nikaulize sasa. Huenda akawa ndugu yetu anaendeleza shughuli zake za utafsiri wa viungo vya wiki hii. Labda tumwandikie Malangali juu hili kisha atueleze ana lipi la kusema au ushauri gani juu hili, huku nikiwa naache ujumbe katika ukurasa wa majadiliano wa Nick1915 na Pathoschild juu ya hili. Natumai nitakuwa nimeeleweka, kazi njema....--Mwanaharakati (majadiliano) 11:52, 15 Machi 2008 (UTC)
Haya, jamaa namwona kaingia si-muda mrefu sana na akasema kwamba tatizo lishaisha, lakini naona bado mambo yapo kama awali. Lakini nimekwisha mjibu juu ya hili. Naomba tuvute subra kidoogo..--Mwanaharakati (majadiliano) 14:50, 15 Machi 2008 (UTC)
Tayari. Kazi njema..--Mwanaharakati (majadiliano) 14:52, 15 Machi 2008 (UTC)
Safi, asante. Si kitu sana kwanga kwa sababu umenionyesha njia ya panya ila tu ni sharti isahihishwa. --User_talk:Kipala (majadiliano) 14:55, 15 Machi 2008 (UTC)

Samahani kidogo. Ninataka kuuliza swali. Hivi sasa ni saa ngapi huko kwenu? Ingaje swali laonekana kama si la msingi sana. Samahani lakini...--Mwanaharakati (majadiliano) 15:07, 15 Machi 2008 (UTC)

Si kitu. 16:06 yaani saa kumi alasiri na dakika sita. --User_talk:Kipala (majadiliano) 15:08, 15 Machi 2008 (UTC)

Hehe. Hata mimi nilifikiria hivyo kama itakuwa kwenye saa kumi hivi, ila nilikuwa nataka uhakika. Ahksante sana..--Mwanaharakati (majadiliano) 16:02, 15 Machi 2008 (UTC)

Salam

Hujambo bwana Kipala. Ninafurahi kupata nyayo zako na ninataka kukusalimu katika jina la Bwana na Mwokozi wangu Yesu Kristo. --213.219.135.57 16:11, 14 Machi 2008 (UTC)

Asante - sema wewe u nani?? --User_talk:Kipala (majadiliano) 16:13, 14 Machi 2008 (UTC)

Mimi ni Stefano Kaisavira, muzaliwa wa DR Congo. Kwa Kifaransa naitwa Etienne Kaisavira. Kiswahili ni lugha yangu tangu utoto. Na ninapendelea sana kuongea na watu katika hii lugha tukufu ya Kiswahili. Ninakaa hapa Brussels Belgium kwa muda wa zaidi ya miaka 12. Email yangu ni etienne.kaisavira@gmail.com na simu yangu ni +32474315897.--Stefano Kaisavira (majadiliano) 16:20, 14 Machi 2008 (UTC)

Sasa wewe unakaa wapi? Kwa Africa ama huku Ulaya? Namna gani ninaweza kukutana na wewe? Tafadhali, nitafurahi kupokea ujumbe wako katika email box yangu.--Stefano Kaisavira (majadiliano) 16:30, 14 Machi 2008 (UTC)

Swali

Salaaam! Naomba niulize kidooogo, maana huku kwetu Afrika bado hali ni tete katika teknolojia ya filamu. Swali ni hivi: Zile bastola wanazotumia katika kuigizia filamu ni za kweli? Na kama ni za uongo mbona zinatoa moto kama ulivyoelezea katika makala ya "Silaha za moto". Naomba nifumbue macho....--Mwanaharakati (majadiliano) 10:14, 18 Machi 2008 (UTC)

Wanatumia ramia bila risasi yaani ganda na baruti pekee. Subiri ninaongeza ramia.--User_talk:Kipala (majadiliano) 10:27, 18 Machi 2008 (UTC)
Sasa mbona vioo, magari, miti na kadharika huwa vinavunjika au hata kupasuka? Hapo je?--Mwanaharakati (majadiliano) 13:10, 18 Machi 2008 (UTC)

Sijaeleweka vizuri. Nauliza wakati pale mtu anapotumia silaha huku ndani yake kukiwa kuna ramia, mbona vitu huharibiwa? Inakuwaje!!! Au hii inaumiza....--Mwanaharakati (majadiliano) 14:07, 18 Machi 2008 (UTC)

Ninavyoelewa ni mambo mawili. Wakitumia bastola mbele ya kamera wanaweka ramia kila kitu inonekana sawa lakini ramia hazina risasi ni ya mazoezi tu. Inaonekana na kusikika kama pigo la risasi lakini si vile. Kitu kingine ni wakionyesha matokeo ya kufyatulia na kadhalika. Kama chombo kinaharibika wanafanya haya mara nyingi kando halafu kazi kubwa ni kukata piach na kuziunganisha, siku hizi mara nyingi kwa kompyuta. Nimeona kwenye TV jinsi gani Petersen anatengeneza mambo yake. Wachazaji huiga kwenye studio mbele ya kitambaa kikubwa cha buluu (blue screen). Kazi ya pekee ni kupiga picha za nyumba inayopasuka au kuchoma moto n.k. Baadaya wanaunganisha yote kwenye deski yaani kompyuta. Sisi tunaona jinsi gani shujaa anapita kwenye moto na milipuko hali halisi alicheza tu kwenye jukwaa ndogo ndani ya ukumbi mbele ya blue screen. --User_talk:Kipala (majadiliano) 16:32, 18 Machi 2008 (UTC)
Duh! Safari ni ndefu ya kufika huko. Lakini inastaajabisha kabisa yaani. Haya, tuombe Mungu labda na sisi tutafika huko kwa miaka hii ya karibuni... Ahksante kwa maelezo yako...--Mwanaharakati (majadiliano) 04:24, 19 Machi 2008 (UTC)

Re:Kiwashio

Upo sahihi kabisa. Unaweza kutumia hata swichi, kwani hata huku pia huwa tunatumia swichi. Ukisema kiwashio, ni bora zaidi kwani utakuwa umetumia Kiswahili. Na ukisema Swichi, hapo inakuja ile kitu ya kusema unaandika neno la Kiingereza kwa maneno ya Kiswahili! Naona yote ni sawa tu. Na pia samahani kwa kuchelewa kukujibu swali lako... Kazi njema..--Mwanaharakati (majadiliano) 14:43, 19 Machi 2008 (UTC)

Re:Bombom

Bombom ni maneno ya kizamani sana. Tumia "Bomu". Kiwashio: Ni sawa kabisa kwamba ni "kidude kinachowashia ramia" hili liko sawa wala usitie shaka. Kuna la zaidi?--Mwanaharakati (majadiliano) 16:07, 19 Machi 2008 (UTC)

Angalia balaa hilo. Nikiwa na angalia taarifa za habari zinahusu juu ya ujambazi uliotokea huwa wanasema: Majambazi hao walikuwa wakitumia "Bunduki" aina ya "SMG" yaani, sub machine gun (sina uhakika kama kirefu chake ndiyo hicho). Sasa kuhusu machine gun sijui ila nasikia wakiita kama bunduki na kuitaja aina gani ya bunduki hiyo. Mengineyo sijui, je unalipi la kusema?--Mwanaharakati (majadiliano) 16:16, 19 Machi 2008 (UTC)
Kazi njema. Naona nikuage kidooogo. Kesho ni sikukuu ya "Mtume Muhammad S.W.A". Kesho kutwa ni Siku kuu ya Ijumaa Kuu, hivyo hatutokuja kazini kwa muda wa siku mbili. Tukijaaliwa Jumamosi! Ushauri wa mwisho: Usitumie sana maneno ya kamusi, kwani huku Bongo hayatumiki mara nyingi! Hivyo ukiandika, upo uwezekano wakuwa unaelewa mwenyewe tu. Labda mtu awe na kamusi, na sio wengi wenye nazo (mimi sina kabisaaa). Ni mfano tosha.. Siku Kuu njema....--Mwanaharakati (majadiliano) 16:34, 19 Machi 2008 (UTC)
Nawe pia!--Mwanaharakati (majadiliano) 16:38, 19 Machi 2008 (UTC)

Watunzi au Watungaji wa muziki?

Ndugu, nimegundua jamii mbili ambako moja ingetosha - angalia majadiliano ya ukurasa wa jamii hii. Pole na usumbufu! Nitasubiri oni lako kabla sijasawazisha hizo mbili ziwe moja. Asante! --Oliver Stegen (majadiliano) 21:05, 22 Machi 2008 (UTC)

Sawazisha tu jinsi unavyoona. Waulize Waswahili huko kipio kinaeleweka. Heri ya Pasaka! --User_talk:Kipala (majadiliano) 21:17, 22 Machi 2008 (UTC)
Kheri ya pasaka! Nina swali kidogo. Nini maana ya Documentary?--Mwanaharakati (majadiliano) 09:25, 25 Machi 2008 (UTC)
Asante, kuhusu documentary: ni filamu (kwetu Kijerumani hata kitabu) ya taarifa juu ya tukio fulani. Yaani si hadithi tu iliyotungwa na mtu. Kamusi ya TUKI inasema: filamu inayoonyesha maisha halisi, filamu ionyeshayo hali halisi. Maana yake hawakubuni neno bado yale ni maelezo. --Kipala (majadiliano) 09:30, 25 Machi 2008 (UTC)

Heheh. Nilikuwa nikiita "makala" lakini za katika televisheni, hapo je?--Mwanaharakati (majadiliano) 09:36, 25 Machi 2008 (UTC)

Sijui tunga jina kwa muda au andika maelezo. Hali halisi ni kitu kama taarifa. Kwenye kipindi cha habari za TV taarifa ni kitu kifupi tu ya nusu dakika hadi labda dakika mbili. Kwenye "documentary" ni taarifa ndefu kidogo. Inaonyesha habari kwa undani, sababu na historia ya tukio au tatizo, watu mbalimbali wanaohusika na kadhalika. Kwa mfano filamu za taarifa ni zile za Michael Moore (kuhusu mauaji kwenye shule ya Columbine High, pamoja na habari za biashara ya silaha katika Marekani, matangazo ya makampuni yanayouza silaha, matamko ya wanasiasa wanaosema kuwa na silaha ni haki ya kila mtu, maduka yanayouza kwa mtuy eyote, majadiliano na polisi na kadhalika..). Moja kuhusu Afrika ni Darwin's nightmare iliyokasirisha wanasiasa huko Dodoma. Alijaribu kuonyesha mazingira ya biashara ya samaki huko Ziwa Viktoria.... --Kipala (majadiliano) 09:59, 25 Machi 2008 (UTC)
Basi tuiite hivyo hivyo Documentary-Kiswahili Dokumentari! Ama namna gani...--Mwanaharakati (majadiliano) 10:20, 25 Machi 2008 (UTC)

Mzungu

Mambo vipi! Mkubwa, naomba umwelezee kwa kirefu "Mzungu" (na hata kutaja asili ya wazungu) maana mie nimejaribu kuelezea kidogo tu. Sasa naomba uchungue makala ile ya Mzungu! Nitashukuru kama utapata kajimuda hiko, Wasalaam,--Mwanaharakati (majadiliano) 14:18, 25 Machi 2008 (UTC)

Nashukuru kwa itikio lako. Ubarikiwe!--Mwanaharakati (majadiliano) 04:32, 26 Machi 2008 (UTC)

Re:Mzungu na interwiki

Salaam! Naona mkubwa umekuja kwa mkwala mzito kabisaa (Usidharau kamusi tena!) Furaha teeele! Sawa mkubwa wangu. Ila nasikitika kwa kukosa kukuona tena kama awali. Hata hivyo katika wiki hizi moja-mbili naona ulikimbiza ajabu. Mimi nipo kama mlinzi katika wiki yetu! Mara nyingi huwa naangalia "mabadiliko ya karibuni" na kujua mengi yaliyojiri katika wiki hii! Basi kila lakheri mkubwa wangu. Kingine: Waweza kufuatilia habari za Checkuser? Hapa kwetu naona hamna checkuser na sisi pia twaitaji checkuser. Tafadhali naomba ufuatilie hili kama inawezekana!--Mwanaharakati (majadiliano) 10:01, 26 Machi 2008 (UTC)

Swali

Salaam. Kuna kajimchezo nataka nikajue jina lake kanaitwaje. Niliona katika TV wakionyesha Wazungu wa Ulaya wakicheza mchezo wa kupigiza viatu huku wakiwa wanalukaluka, yaani wanavyocheza viatu ndiyo vinasikika sana kuliko chochote katika mchezo huo. Je huo mchezo unaitwaje?--Mwanaharakati (majadiliano) 11:55, 31 Machi 2008 (UTC)

Kuna ngoma kadhaa zinavyochezwa hivyo. Nchi mbalimbali. Kama wanapiga mapaja pia ni Wabavaria kutoka kwetu kusini au majirani Waaustria. Wengine ni Wahispania. Ukiangalia picha hizi utaona vikundi vinavyocheza ngoma za kienyeji sehemu mbalimbali. Kama wamevaa kiutamaduni ni rahisi zaidi kusema ilikuwa nini. --Kipala (majadiliano) 13:08, 31 Machi 2008 (UTC)

Kwa hiyo hamna jina rasmi la mchezo huo?--Mwanaharakati (majadiliano) 13:41, 31 Machi 2008 (UTC)
Bila shaka kuna jina ila tu kuna aina mbalimbali katika nchi tofautitofauti hivyo majina yatatofautiana. Unavyoeleza ni aina ya ngoma zinazoitwa "folk dance" kwa Kiingereza. Lakini hii ni jina la kujumlisha aina zote za ngoma za kiutamaduni na aina unazoeleza ni za pekee kati ya hizi. Bila kujua inatokea wapi hatutapata jina. --Kipala (majadiliano) 20:12, 31 Machi 2008 (UTC)
Habari za asubuhi Bw. Kipala. Leo ni siku yangu ya furaha kwa kufikisha mwaka tangu kuanza kazi katika sekta ya uhasibu hapa kazini. Nilianza mnamo tar. 02-04-07 hadi leo hii 02-04-08, nimefikisha mwaka bila tabu hivyo namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunifikisha leo hii! Nimefurahi kukujulisha juu ya hili, kazi njema!--Mwanaharakati (majadiliano) 09:26, 2 Aprili 2008 (UTC)
La. Sio katika Wikipedia. Ni sehemu ninayofanya kazi! Katika Wikipedia, mpaka tarehe 18 ya mwezi wa nane ndiyo nitafikisha mwaka! Basi nashukuru kwa hongera yako! Ubarikiwe.--Mwanaharakati (majadiliano) 10:29, 2 Aprili 2008 (UTC)

Salam. Kuna neno nimeshindwa kutafsiri. Naomba nisaidie maanake halisi:

  • "Mighty Handful"

Wakati najaribu kuandika makala ya César Cui. Naomba nisaidie!--Mwanaharakati (majadiliano) 09:29, 3 Aprili 2008 (UTC)

"Handful" inamaanisha hapa watu wachache - "mighty" ya kwamba ni wenye uwezo sana, kazi yao ni bora. --Kipala (majadiliano) 18:47, 3 Aprili 2008 (UTC)
Ndugu khari yako. Kuna ujumbe nimetuma katika mailbox yako! Naomba uungalie na unijibu kulekule katika E-mail....--Mwanaharakati (majadiliano) 12:14, 4 Aprili 2008 (UTC)

Re:Vyakula

Salam. Hapa sipati picha iliyo kamili. Labda uiite "Jamii za nafaka" kwani kunde hutaja jina moja tu! Kunde ni kunde tu kama kunde. Na kunde ipo ndani ya nafaka, nafaka ni maharagwe, njegele, njugumawe, dengu, choloko na kadhalika. Jaribu kutunga jina lolote lile la kutaja vitu hivyo vyote mbali na "Jamii kunde". Unaonaje?--Mwanaharakati (majadiliano) 12:00, 5 Aprili 2008 (UTC)

Nafaka? Sidhani lakini sina uhakika. Ninavyoelewa hadi sasa matumizi ya nafaka inalingana na "grain" - yote mbegu za aina manyasi. Jinsi unavyoelewa wewe ni kingine. "Jamii kunde" inatakiwa kutafsiri "legume". Nimebadilisha kidogo sentensi ya kwanza; sijui kama ni sawa. Maana ya jina ni ya kwamba ni kundi la mbegu za kuliwa, na zote zafanana na kunde. Nadhani wangeiita pia "jamii maharagwe" hapa nimefuata TUKI. Nisingeandika kama siyo kumaliza majina yale ya orodha inayotaka "legume".

Kingine kuhusu "mboga" ni "vegetable". Hapa nimeona tangu muda mrefu kamusi zinataja mboga lakini watu huwa na maana pana zaidi ndani ya mboga ama majani ama nyama. Sijui yale yanaoitwa vegetable unaita nini? --Kipala (majadiliano) 13:19, 5 Aprili 2008 (UTC)

Mboga za majani. Ndiyo hizo nilizokuwa nikisema hapo mwanzo kabisa ni kwamba matembele, majani ya maboga, kisamvu na kadhalika. Hapo vipi?--Mwanaharakati (majadiliano) 13:25, 5 Aprili 2008 (UTC)
Sasa naenda zangu! Na sinto kuwa hewani hadi siku ya Jumanne, kwasabau huku Bongo kutakuwa na Siku kuu ya Karume, yaani Karume Day. Endapo utakuwa swali uliza sasa!--Mwanaharakati (majadiliano) 13:33, 5 Aprili 2008 (UTC)
Haya basi kwa kheri! Tukijaaliwa tutaonana Jumanne!--Mwanaharakati (majadiliano) 13:58, 5 Aprili 2008 (UTC)

Television Soap Opera

Salama nyingi zikufikie Nd. Kipala. Nilikuwa naomba msaada wa kutafsri baadhi ya maneno kutoka hapa, nitashukuru kama utanipatia msaada huo! Kazi njema....--Mwanaharakati (majadiliano) 06:58, 14 Aprili 2008 (UTC)

Utofauti katika logo ya Wikipedia kwa Kiswahili

Salam. Mkubwa samahani kidogo. Naona kuna tatizo la kuelekea katika ukurasa wa mwanzo, yaani ile logo yenye kuonyesha kama hii ni Wikipedia (Kamusi elezo huru) naona hakuna na badala yake imekaa picha ya askari wa doria. Je ni mimi tu ndiyo ninayoona hivyo au hata wewe mwenzangu waona hivyo?--Mwanaharakati (majadiliano) 15:07, 16 Aprili 2008 (UTC)

Ahksante kwa pole! Naona bado hujanipata. Labda angalia hii:
Faili:Mfano a.JPG
Fananisha hizi. Kushoto ni sw:wiki na kulia ni en:wiki.

Sasa huyo askari anafanya nini katika hiyo sehemu ya logo ama kwako huoni?--Mwanaharakati (majadiliano) 15:30, 16 Aprili 2008 (UTC)

Huku kwangu ni balaa tupu. Kila kitu kimekaa hovyo. Na katika wikipedia chini - sehemu ya kutajia: "Sera ya faragha", Kuhusu Wikipedia na Kanusho! Kulikuwa na picha zinazoonyesha Wikimedia logo na MediaWiki logo, navyo vyote hamna. Naona hii ni "another victim" katika Wikipedia hii! Sasa nifanyaje?--Mwanaharakati (majadiliano) 15:44, 16 Aprili 2008 (UTC)

Navuta subira huenda na kwako ikawa! Na mara itakapofika kwako ndiyo tutachukua hatua lakini kwa sasa bado ni mapema mno. Au wewe unaonaje nikifanya subra kwanza....--Mwanaharakati (majadiliano) 05:49, 17 Aprili 2008 (UTC)

Kama uji na mgonjwa. Yaani ipo kama jana ilivyokuwa na bado haijabadilika kuwa sawa kama awali. Lo, tabu tupu. Lakini nakubmuka hata lile swala la mwanzo nilianza kuona mimi kisha baadaye wewe ama sivyo?--Mwanaharakati (majadiliano) 09:22, 17 Aprili 2008 (UTC)

Salam. Naona isharudi kama awali. Vipi umefanya maarifa? a)(b Piano kumbe ni nini kama sio Kinanda?--Mwanaharakati (majadiliano) 06:45, 18 Aprili 2008 (UTC)

Kinanda

Ahsante kwa ushauri wako. Lakini kulikuwa na tatizo la kuingiliana kwa IP address yetu na mtu mwingine, yaani IP moja tunatumia watu wawili hivyo ilileta mgogoro. Lakini kwa sasa wesha weka sawa! Kuhusu piano: Hapa bado naona kizungumkuti kabisaa, organ, piano na keybord. Labda nikupe tofauti ndogo:

1. Piano: mara nyingi tunaamini kwamba ni kinanda kile cha Kanisani (hasa wakatoliki) na kile cha Wazungu wanachoweka majumbani mwao!

2. Organ: ni kinanda cha wapiga taarab, yaani hutumia kupiga kwa kushika mkononi huku akiwa wima. Ni hasa wale wapigaji wa kale (zilipendwa)

3. Keybord: ni kinanda cha wapiga muziki wa kawaida, yaani wapiga muziki wa taarab, mabendi, makanisa ya kilokole n.k.

Pamoja na kuwa na mlolongo mrefu wa maelezo kuhusiana na hayao, lakini bado vyote tunaviita vinanda bila kubagua namna vilivyo! Unaonaje?--Mwanaharakati (majadiliano) 08:42, 18 Aprili 2008 (UTC)

Hongera ya makala 7,000

Kipala na Oliver, hongereeni kwa kusukuma wiki yetu juu ya kiwango cha makala 7,000! Nafurahia kuona tumefikia makala elfu saba. Naona kama naota kufikia kiwango hicho, ingawaje si nyingi hivyo lakini tumefika!. Basi tuendelee kushauriana na kuvumiliana!--Mwanaharakati (majadiliano) 07:28, 21 Aprili 2008 (UTC)

CD ya Wikipedia. Sijafahamu namna gani au inakuwaje kuhusu CD?--Mwanaharakati (majadiliano) 11:51, 22 Aprili 2008 (UTC)

Ualimu

Ndugu Kipala, asante kwa mawasiliano. Nakubali kichwa Ualimu kibadilishwe kiwe Ualimu wa Kanisa, ila sijui namna ya kukibadilisha... Pia ningependa Klara kiwe Klara wa Asizi. Fanya wewe!