Nenda kwa yaliyomo

Asenia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Aseniki)


Asenia (arseniki)
Asenia yenye rangi nyeusi ndani ya madini mengine
Asenia yenye rangi nyeusi ndani ya madini mengine
Jina la Elementi Asenia (arseniki)
Alama As
Namba atomia 33
Mfululizo safu Simetali
Uzani atomia 74.9216
Valensi 2, 8, 18, 5
Densiti 1.9 hadi 5.72 kufuatana na alotropia zake
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka 1090  K (817 ° °C)
Kiwango cha kuchemka 887  K (614 °C) (mvukemango)
Asilimia za ganda la dunia 6 · 10-4 %
Hali maada mango
Mengineyo Asenia ni tahajia ya KAST, Aseniki ya ILSD, Arseniki penginepo katika mtandao

Asenia (pia: arseniki, aseniki; kutoka kigiriki αρσενικόν "arsenikon" iliyotaja kampaundi ya elementi) ni nusumetali au metaloidi yenye namba atomia 33 katika mfumo radidia. Uzani atomia ni 74.9216.

Asenia ina tabia ya alotropia kwa hiyo kuna maumbo na rangi mbalimbali. Kuna hasa maumbo yenye rangi za kijivu, nyeusi, njano na kahawia. Asenia ya kijivu ina fuwele na tabia za kimetali. Asenia nyeusi hupatikana kwa umbo hobela kama kioo.

Asenia ni sumu kali kwa binadamu.

Matumizi

[hariri | hariri chanzo]

Kampaundi za asenia hutumiwa kama madawa katika tiba ya watu lakini pia madawa ya kuua wadudu. Madawa yaliwahu kuleta hasara ya kiafya hata kuua watu.

  • Mwaka 1900 walikufa watu 70 mjini Manchester (Uingereza) kwa sababu kiwanja cha bia kilitumia nafaka iliyowahi kutiwa madawa ya asenia kwa kuua wadudu.
  • katika karne ya 20 bao za ujenzi zitiliwa mara nyingi dawa la asenia kwa kuzuia wadudu. Bao hazikuwa na hasara lakini imeonekana baadaye ya kwamba majivu ya ubao huu kama ulichomwa motoni yalikuwa hatari sana; gramu 20 za majivu ya ubao huo zikatosha kumwua mtu; maafa yalitokea baada ya watoto kucheza kwenye majivu au wanyama kulamba maji karibu na mahali pa moto baada ya mvua.

Asenia ikichanganywa na risasi (metali) (plumbi) husaidia katika kutengenezwa kwa beteri za gari ikiboresha umwagaji wa plumbi kiwandani.

Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Asenia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.