Nenda kwa yaliyomo

Risasi (metali)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

kwa risasi kama ramia ya bunduki au bastola tazama risasi (silaha)


Risasi au Plumbi (plumbum; kiing. lead)
Vipande vinene vya risasi huleta kinga dhidi ya Caesi nururifu chini yake.
Vipande vinene vya risasi huleta kinga dhidi ya Caesi nururifu chini yake.
Jina la Elementi Risasi au Plumbi (plumbum; kiing. lead)
Alama Pb
Namba atomia 82
Mfululizo safu Metali
Uzani atomia 207.2
Valensi 2, 8, 18, 32, 18, 4
Densiti 11.34 g/cm³
Ugumu (Mohs) 1.5
Kiwango cha kuyeyuka 600.61 K (327.46 °C)
Kiwango cha kuchemka 2022 K (1749 °C)
Asilimia za ganda la dunia 2 · 10-3 %
Hali maada mango
Mengineyo Risasi ni elementi nzito isiyo nururifu

Risasi (kutoka Kiarabu: رَصاص rasas; jina la kisayansi: plumbi linatokana na Kilatini "plumbum") ni elementi. Namba atomia yake ni 82 kwenye mfumo radidia na uzani atomia ni 118.710.

Ni metali nzito na laini yenye rangi ya buluu-kijivu. Huyeyuka mapema kwenye kiwango cha halijoto cha 327 °C. Ni babaikaji kirahisi na kwa sababu hii ilikuwa kati ya metali za kwanza zilizotumiwa na binadamu katika historia. Ikiingia katika mwili wa binadamu ni sumu. Haimenyuki kirahisi.

Kama metali nzito ina pia densiti kubwa.

Matumizi

[hariri | hariri chanzo]

Sehemu kubwa ya risasi hutumiwa kwa ajili ya betri za magari. Nyingine hutumiwa kwa ajili ya aloi mbalimbali.

Risasi huyeyushwa haraka na hivyo kuna mbinu ya kuitumia kwa kazi ya kushika mabati ya kufunika nyumba. Matumizi mengine ni katika vioo vya madirisha ambapo vipande vya kioo cha rangi huunganishwa kuwa dirisha linaloonyesha picha. Hapo vipande vya kioo hushikwa kwa risasi.

Zamani risasi ilitumiwa pia kwa mabomba ya maji lakini hii imeachwa kutokana na tatizo la metali hii kuwa sumu. Kazi ya fundibomba kwa Kiingereza hadi leo huitwa "plumber" kutokana na "plumb" ambalo ni jina la Kilatini la risasi.

Risasi katika silaha

[hariri | hariri chanzo]

Kihistoria risasi ilikuwa muhimu tangu kupatikana kwa silaha kama ramia au kiasi cha bunduki na bastola. Ramia zilitengenezwa kwa muda mrefu kwa kutumia metali ya risasi pekee. Leo hii risasi peke yake ni laini mno kwa teknolojia mpya ya silaha zenye kanieneo (shindikizo) kubwa. Bado risasi hutumiwa kwa sababu ya uzito wake lakini siku hizi hufunikwa na koti la aloi ya shaba inayozuia kubadilishwa kwa umbo lake wakati wa kurushwa katika silaha.

Risasi kama kinga ya mnururisho

[hariri | hariri chanzo]

Densiti kubwa ya risasi ni kinga nzuri dhidi ya mnururisho. Hivyo kuna mavazi ya kinga yanayovaliwa na waganga wanaotumia eksirei mara kwa mara. Hata wagonjwa wanaochunguzwa hupewa mifuniko yenye risasi kwa kinga ya viungo vya uzazi dhidi ya mnururisho wa eksirei.

Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Risasi (metali) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.