Nenda kwa yaliyomo

Mtumiaji:Kipala/Archive 7

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Archive Hii ni ukurasa wa Hifadhi ya Majadiliano ya Awali. Usihariri ukurasa huu usiongeze wala kupunguza kitu.
Ukitaka kujadiliana upya mambo yaliyomo humo nenda kwa ukurasa wa majadiliano ya sasa.


Arusha

Kipala vipi ndugu yangu..samahani kwa makosa yangu sikuwa nimesoma wikipedia mwongozo..bado najifunza.Maneno mengine ni vigumu kupata tafsiri yake hapo ndo natumia google translate lakini kwa neno moja moja tu..tuzidi kusaidiana.


Nonkilling

Hi! I was wondering if you would help us create an entry in Kiswahili for "Nonkilling" [1]. The first paragraph would do! --Cgnk (majadiliano) 19:02, 3 Juni 2009 (UTC)

Commonwealth

You can delete it if you wish. I was trying to explain that there are four states that are called "commonwealths" instead of "states", and that by definition there really is no difference. It was a poor attempt on my part. Jhendin (majadiliano) 23:43, 21 Machi 2009 (UTC)

Kipala, salam. Eti, unaweza kunidokezea kidogo kuhusiana na hii "heroin?" Ni madawa ya kulevya ama kitu gani? Itakuwa bora zaidi endapo kama utaindikia makala ili faida wapate watu wote! Lakini kabla hujaandikia makala (au hata ukiona uandike moja kwa moja ni sawa tu). Shida yangu ni kujua hiyo heroin ni kitu gani! Kazi njema.--Mwanaharakati (Longa) 10:07, 24 Machi 2009 (UTC)

Basi umepata afyuni na heroini --Kipala (majadiliano) 09:12, 25 Machi 2009 (UTC)
MENO NJE! Kabla sijaanza kutia neno lolote lile kwanza ninatoa shukrani zangu kwako! Najisikia vibaya kwa mtu mzima kama wewe kukuomba makala hii. Haya, tatizo lililoko huku kwetu kwa sasa ni namna ya kuita madawa au dawa? Eti walikuwa wanadai ya kwamba hakuna madawa, bali kuna dawa! Lakini bado haileti maana kwa sababu hutoweza kutofautisha wingi wake kama hutoita madawa! Watajua wenyewe. Madawa ya kulevya umeadindika sahihi kabisa. Huwezi kutaja wingi wake bila kusema madawa ya kulevya, never. Hivyo upo sahihi mzee wangu. Au labda utumie dawa za kulevya?--Mwanaharakati (Longa) 10:06, 25 Machi 2009 (UTC)
Salaaam! Naomba nisaidie maana ya "Job queue lenth". Nitakuwa mwenye kushukuru endapo utanisaidia hili!--Mwanaharakati (Longa) 06:50, 26 Machi 2009 (UTC)
Sina uhakika. --Kipala (majadiliano) 08:55, 26 Machi 2009 (UTC)

Je, nikikupa kiungo husika na maelezo utanisaidia?--Mwanaharakati (Longa) 11:18, 26 Machi 2009 (UTC)

Nisipokosei niliwahi kuiangalia lakini sijaelewa. Nimekata tamaa nikaiacha. Je huwezi kuona raha bila kuielewa? --Kipala (majadiliano) 16:48, 26 Machi 2009 (UTC)
Mmhhh. Haswaaaa, sijikii raha bila kuilewa! Pia, lengo litakuwa halijatimia!! Basi nenda hapa. Ukifika utaona maelezo yaliyotajwa hapo juu!--Mwanaharakati (Longa) 16:53, 26 Machi 2009 (UTC)

Miji, kata, wilaya, na mikoa ya Kenya

Kipala, salam. Nimeona umeshaanza kuandika au kuandaa baadhi ya mikoa wilaya na... ya Kenya. Je, muundo wa majedwali yao yamekaa kirahisi? Ninauliza kwa sababu ningependa kuchangia tena! Kama inawezekana. Ni mimi kijana wako,--Mwanaharakati (Longa) 06:53, 27 Machi 2009 (UTC)

Asante - nitaanzisha ukurasa wa pekee kwa kazi hii. Nimeanza kutafuta ufafanuzi zaidi kutoka arthurbuliva yuko tayari kushauri pia. Mara naona mwanga juu ya utaratibu wa Kenya tuanze nitafurahi tukiendelea kushirikiana! --Kipala (majadiliano) 13:05, 27 Machi 2009 (UTC)
Basi tutashirikiana!--Mwanaharakati (Longa) 14:28, 27 Machi 2009 (UTC)
Mzee wangu, salaaam! Natumai ya kwamba unamwona huyo babu HBR namna anavyoanzisha makala zake bila maelezo. Akianzisha makala, basi ataweka picha tu bila elezo lolote lile. Hivi karibuni katunga makala tatu (ambazo zote zina picha tu bila maelezo!) Haivutii na wala sio vizuri! Nimeona ukijadiliana naye kwa kutumia Kijerumani - akheri uongee naye kwa Kijerumani, labda atakufahamu! Ni hilo tu, mzee wangu. Ni mimi kijana wako mpendwa,--Mwanaharakati (Longa) 06:05, 3 Aprili 2009 (UTC)
Asante kwa kunidokeza kuna tatizo. umeona nilikuwa kimya maana niko safarini. Kesho kutwa narudi nyumbani nitafuatilia jambo hili. --Kipala (majadiliano) 19:38, 3 Aprili 2009 (UTC)

Basi samahani kwa kukupa taarifa ukiwa safarini! Nitasubiri hadi hapo utakapofika nyumbani. Safari njema!--Mwanaharakati (Longa) 06:21, 4 Aprili 2009 (UTC)


Kipala, salam. A) Pole kwa kazi ya ku-undo maandiko ya waharibifu wa Wikipedia! BE) Naona ushaanza kuanzisha makala za Kenya. CHE) Ningependa kuchangia, lakini ninataka nipewe mwangaza! Kila la kheri.--Mwanaharakati (Longa) 07:44, 8 Aprili 2009 (UTC)

11,000

Mzee wangu, salaaaaam! Wikipedia yetu imefikisha makala 11,000! Ni furaha iliyoje? Basi tu, niseme tujitahidi kuendeleza na kushauriana kwa kila jambo litakalosaidia Wikipedia yetu kuwa juu! Kila la kheri.--Mwanaharakati (Longa) 15:50, 9 Aprili 2009 (UTC)

Basi ni maendeleo kwelikweli. Je unaonaje kama tutaona ngazi inayofuata ambayo ni lakhi? Nimeweka kumbukumbu ukurasa wa matukio ya hivi karibuni. Kuhusu Kenya nahangaika bado kidogo sijui tuanzishe vigezo vya kata kiwilaya au kimkoa? Kata ni chache Kenya kuliko TZ tena wameanzisha wilaya nyingi na sina takwimu ni kata gani iliyokwenda wilaya gani. --Kipala (majadiliano) 17:33, 9 Aprili 2009 (UTC)
Salam, Kipala. Kuhusu Kenya bado sina mwangaza unaonipa matumaini bila juhudi zako! Ukiona umepata sehemu yenye kurahisha habari, basi nionyeshe, nami nitatekeleza maramoja! Na hata kuhusu kuwekea vigezo - ni sawa! Basi endelea kutafuta njia mbadala itakayorahisisha kuandika makala hizo za Kenya! Ni mimi kijana wako mpendwa,--Mwanaharakati (Longa) 05:42, 11 Aprili 2009 (UTC)

Subdivisions of Tanzania

Kipala, salam! Mzee wangu, naomba nisaidie kutafsiri hilo neno la hapo juu. Maana yake, nimeshindwa kabisa kulileta kwenye Kiswahili! Jioni njema.--Mwanaharakati (Longa) 14:46, 16 Aprili 2009 (UTC)

Je siyo vitengo vya kiutawala vya TZ? --Kipala (majadiliano) 18:03, 16 Aprili 2009 (UTC)
Kwa mujibu wa Wikipedia ya Kiingereza:
    • Tanzania has country subdivision as follows:
      • 26 regions of Tanzania (mkoa).
regions are subdivided into 98 districts of Tanzania (wilaya).
district are divided into wards.

Si unadhani itakuwa mwangaza?--Mwanaharakati (Longa) 06:12, 17 Aprili 2009 (UTC)

Nadhani tafsiri ni hivi: Vitengo vikuu vya utawala nchini Tanzania ni mikoa 26. Kila mkoa una wilaya ndani yake, kwa jumla kuna wilaya 98. Wilaya hugawiwa kwa tarafa na kata (je tarafa bado ziko? Nilisikia ya kwamba serikali inataka kuzifuta). --Kipala (majadiliano) 20:23, 17 Aprili 2009 (UTC)

Wikipedia ya Kiswahili

Hallo Kipala. Im Dezember 2003 habe ich mir die damalige Suaheli-Wikipedia angeschaut, und dabei bemerkt, dass dort noch gar kein enzyklopädisches Material vorhanden war. Es gab eigentlich nur zwei-drei "Artikel", die Text von woanders kopiert hatten, sowie einige weitere "Artikel", die nur die englische Übersetzung des Titels genannt haben. Am Anfang habe ich die Wikipedia nicht eingeloggt bearbeitet, so dass es schwierig ist, meine ersten Beiträge zu finden. Unter meinen IP-Adressen waren auf jeden Fall die Adressen, die mit "163.1.209" anfangen und mit ".239" bis ".245" aufhören. Der älteste Beitrag, den ich eindeutig mir zuordnen kann, ist die Erstellung des Artikels Kiesperanto am 7. Dezember 2003. Am 5. Februar 2004 wurde ich dann aktiver: Erst habe ich die drei Artikel Lugha iliyotengenezwa, Lugha asilia und Lugha saada ya kimataifa geschaffen, und dann die erste Erklärung zum Wikipedia-Projekt auf die Hauptseite gestellt:

"Wikipedia ni mradi wa lugha nyingi wa kutengeneza kamusi elezo kamili na sahihi ya maandishi huru. Ilianzishwa kwa Kiingereza mwezi wa kwanza mwaka 2001, na mwaka 2003 imeanzishwa kamusi hii kwa Kiswahili. Kusema kwamba ni maandishi huru maana yake ni kwamba kila mtu anaweza kuikuza na kuibadilisha, hata usipofahamu mambo ya kompyuta. Uweke "Edit this page" tu, halafu badilisha au ongeza maandiko."

Dabei hatte ich mir den Ausdruck "kamusi elezo" selber ausgedacht. Das Kamusi Project hat damals nur "kamusi" als Übersetzung von "encyclopedia" angegeben, und mein Deutsch-Suaheli-Wörterbuch hatte keine Übersetzung von "Enzyklopädie". Ich wollte einer Verwechslung von Wörterbuch und Enzyklopädie entgegenarbeiten (diese Verwechslung hatte ja schon dazu geführt, dass einige Artikel einfach aus der englischen Übersetzung des Wortes bestanden), und habe dafür den Begriff "kamusi elezo" geschaffen.

Am 19. Februar habe ich das erste Mal eingeloggt gearbeitet, und dabei die Artikel Hisabati und Hesabu erstellt bzw. enzyklopädisch gemacht. In der darauf folgenden Zeit habe ich mich bemüht herauszufinden, wie ich das Interface ins Suaheli übersetzen kann. Am 31. Mai 2004 war ich dann schon Administrator geworden, und konnte die MediaWiki-Texte übersetzen. Im Juni 2004 habe ich dann noch weiter Artikel wie Historia, Jumuia und Uislamu erstellt bzw. enzyklopädisch gemacht. Im Januar 2005 hat Neno (interessanterweise auch ein Esperantist) angefangen, zur Wikipedia beizutragen (sehr stark mit MediaWiki-Übersetzung), im September 2005 Ndesanjo und im Dezember 2005 du. Seit Ende 2005 kann man das Projekt als (eingeschränkt) aktiv bezeichnen. Bis Muddy im August 2007 aktiv wurde haben im Projekt allerdings eindeutig die Nicht-Muttersprachler überwogen (mit Ndesanjo als einziger Ausnahme). Auch jetzt kommen noch ca. die Hälfte der Beiträge von Nicht-Muttersprachlern.

Wenn du noch weitere Fragen hast, beantworte ich diese gerne. Marcos (majadiliano) 13:52, 25 Mei 2009 (UTC)

Je, huu mjadala unahusu masuala ya Wikipedia kwa Kiswahili? Ikiwa unahusu Wikipedia hii, wengine hatutofaidika na nia ya mjadala huu kwa kufuatia kutojua lugha ya Kijerumani! Huruma ni kwamba Kipala siku hizi hapatikani.. Tafakari..--Mwanaharakati (Longa) 14:20, 25 Mei 2009 (UTC)
Kipala aliniandikia kwenye Wikipedia ya Kijerumani na suala yake kuhusu historia ya Wikipedia ya Kiswahili. Nilianza kuandiku jibu katika ukarasa wake katika Wikipedia ya Kijerumani, na kwa hiyo nilitumia Kijerumani. Baadaye niliona kwamba alitaka nijibu kwenye ukarasa wake katika Wikipedia ya Kiswahili. Ili wengine waweze kuelewa niliandika nini, nitaitafsiri sasa:
Mwezi wa 12 mwaka 2003 niliangalia Wikipedia ya Kiswahili. Nikatambua kwamba yaliyomo hayakuwa habari za kamusi elezo. Kwa kweli kulikuwa na "makala" mbili au tatu tu, zilizokuwa na habari kutoka tovuti nyingine; aidha kulikuwa na "makala" chache zilizokuwa na tafsiri ya Kiingereza ya neno moja tu. Mwanzoni nilihariri bila kuingia. Kwa hiyo ni kigumu kupata hariri zangu za kwanza. Anuani za IP nilizozitumia kwa uhakika zilikuwa anuani zinazoanza na "163.1.209" na zinazokamili na ".239" hadi ".245". Hariri ya zamani zaidi ambayo ninajua kwamba ni yangu ni uundaji wa makala Kiesperanto tarehe 7 mwezi wa 12 mwaka 2003. Tarehe 5 mwezi wa pili mwaka 2004 nilianza kufanya kazi nyingi zaidi: Kwanza niliunda makala tatu Lugha iliyotengenezwa, Lugha asilia na Lugha saada ya kimataifa, baadaye nikaweka uelezaji wa kwanza kuhusu Wikipedia kwenye Ukarasa wa Mwanzo:
"Wikipedia ni mradi wa lugha nyingi wa kutengeneza kamusi elezo kamili na sahihi ya maandishi huru. Ilianzishwa kwa Kiingereza mwezi wa kwanza mwaka 2001, na mwaka 2003 imeanzishwa kamusi hii kwa Kiswahili. Kusema kwamba ni maandishi huru maana yake ni kwamba kila mtu anaweza kuikuza na kuibadilisha, hata usipofahamu mambo ya kompyuta. Uweke "Edit this page" tu, halafu badilisha au ongeza maandiko."
Msemo "kamusi elezo" niliubuni mwenyewe. Siku zile Kamusi Project ilikuwa na tafsiri "kamusi" tu kwa "encyclopedia", na kamusi yangu ya Kijerumani-Kiswahili haikuwa na tafsiri kwa "Enzyklopädie". Nilitaka kuzuia ukorogo kati ya kamusi (yaani kitabu chenye tafsiri za maneno) na kamusi elezo (yaani kitabu chenye maelezo kuhusu mambo mbalimbali; ukorogo huu tayari ilisababisha kwamba kulikuwa na makala zenye tafsiri za maneno kwa Kiingereza tu), kwa hiyo nilibuni msemo "kamusi elezo".
Tarehe 19 mwezi wa pilli nilihariri kwa mara ya kwanza kwa kutumia akaunti yangu: Nilibuni makala Hisabati na nilifanya makala Hesabu iwe na habari za kielezo. Baadaye nilijaribu kung'amua jinsi ya kutafsiri kusano (yaani "interface") kwa Kiswahili. Tarehe 31 mwezi wa 5 mwaka 2004 tayari nilikuwa mkabidhi na niliweza kutafsiri ujumbe za mfumo. Mwezi wa sita mwaka 2004 niliendelea kubuni makala au kufanya makala ziwe na habari za kielezo, kwa mfano Historia, Jumuia na Uislamu. Mwezi wa kwanza mwaka 2005 Neno (ambaye pia ni Mwesperanto) alishirikiana na Wikipedia ya Kiswahili (hasa alitafsiri ujumbe za mfumo), mwezi wa tisa mwaka 2005 Ndesanjo akaja, na mwezi wa 12 mwaka 2005 Kipala. Tangu mwisho wa mwaka 2005 mradi unaweza kuitwa mradi wenye uhai. Mpaka Muddy alishirikiana mwezi wa 8 mwaka 2007 wageni (yaani watu wasioongea Kiswahili kama lugha ya mama) walifanya sehemu kubwa ya kazi. Bado sasa karibu nusu ya hariri zinatoka kwa wageni. Marcos (majadiliano) 23:26, 26 Mei 2009 (UTC)
Hahaha. Historia safi. Hongera kwa kuweza kuwa na kumbukumbu zote hizo. Haya, mpaka sasa ni Mswahili pekee niliyebakia katika mradi huu. Wageni nao wanaanza kupotea (kwa kufuatia kuhama kikazi)! Kwa sasa ninampango wa kufanya mapinduzi ya ukurasa wa mwanzo wa Wikipedia. Ukiwa una muda, tafadhali naomba utembelee mjadala unaofanyika hapa. Nitashukuru sana kama utasaidia mawazo mawili matatu juu ya hili. Kingine: Unaonaje ukitumia historia hiyo uliyoitaja kuhusu hatua za Wikipedia hii - katika makala ya Wikipedia ya Kiswahili? Itakuwa safi sana. Kila la kheri..--Mwanaharakati (Longa) 05:41, 27 Mei 2009 (UTC)
Umeshaona ya kwamba kwa sasa nina nafasi ndogo lakini sijaacha wikipedia nimefuatilia na Marcos nikifurahia ya kwamba alijibu kwa kirefu. Naona ni kumbukumbu muhimu ya hatua za kwanza za wiki hii. Mimi mwenyewe nilipoanza kuchangia ilikuwa bado mmea mchanga mno (makala 149 pekee) lakini muundo uliwekwa tayari ilikuwa msingi mzuri kwa kujenga. Nitaangalia nafasi ya kujumlisha taarifa ya Marcos kwa makala husika. --Kipala (majadiliano) 20:30, 27 Mei 2009 (UTC)
Tutakuwa wenyekushukuru endapo utapata muda wa kukopa hayo maelezo na kuyaweka kwenye makala ile! Kila la kheri.--Mwanaharakati (Longa) 05:33, 28 Mei 2009 (UTC)

Mwanaharakati awe bureaucrat

Nimemteua Mwanaharakati achaguliwe kuwa msimamizi mkuu pamoja nasi (b'crat). Naomba upige kura kwenye ukurasa wa wakabidhi. Asante! --Baba Tabita (majadiliano) 07:13, 28 Mei 2009 (UTC)

Ningekushukuru ikiwa unaweza kuzaidia kurekebisha ukurasa wa Botswana. Niliwahi kujaribu kuongeza information walakini nikawa kufanya makosa na sahisi ukurasa huo huonekani vizuri. Nakushukuru--90.130.222.146 21:15, 11 Juni 2009 (UTC)

Translation

  • Can you translate this paragraph to Kiswahili Language?
    • Bartın Merkez, is the capital city of the Bartın County, Turkey. It located in Black Sea Region. It's population holds 121860 people.

History: Bartın's first name is Parthenios changed to Parthenia. After years, city's name changed to last situation, Bartın.
Picture:The yellow area shows Bartın Merkez.

Iko tayari nisipokosei --Kipala (majadiliano) 09:54, 17 Juni 2009 (UTC)

Ukurasa mpya wa mwanzo

Kipala, salaam! Haya, ukurasa mpya wa Wikipedia ya Kiswahili, leo hii umefikia siku yake!!! Nimebadilisha tayari. Ahsante kwa ushirikiano wako. Wako kijana, Muddyb, au,--Mwanaharakati (Longa) 14:00, 20 Juni 2009 (UTC)

Mzee wangu salaam! Labda ungetazama sehemu iliyoandikwa:

Wikipedia kwa lugha nyingine

Chini yake kuna maelezo yameandikwa "bofya hapa kwa orodha ya wikipedia zote" kama sikosei...--Mwanaharakati (Longa) 16:14, 23 Juni 2009 (UTC)

Jimbo la Ardahan

Mzee wangu, salaam! Kumradhi kwa kuchelewa kukujibu. Nilikuwa sipo kidogo. Kuhusu Jimbo la Ardahan - siyo mimi niliyehamisha kutoka mji kwenda jimbo. Kuna kijana mmoja wa Kituruki asiyejua Kiswahili kabisa alijishaua kuhamisha makala za miji na kuzipeleka jimboni ilhali zenyewe zilikuwa zikitaja miji ya majimbo ya kwao. Kwa kuwa yeye alikuwa Mturuki, bila kujua maana ya maelezo yaliyoandikwa - akahamisha makala zile! Hata hivyo, sikumezea mate, nilimweleza Oliver juu ya tendo alilolifanya, na Oliver akashauri tumwache, ila ni lazima aambiwe asihamishe ile miji kwenda jimboni. Na swali lako, ule ni mji na sio JIMBO! Mimi nitarudisha kama vile inavyotakiwa. Halafu nina swali moja, Uturuki wao hutumia majimbo au mikoa? Wako kijana mtiifu,--Mwanaharakati (Longa) 05:48, 9 Julai 2009 (UTC)

Mimi ningesema ni mikoa; nchi yote ina maeneo 81 yanayoitwa "valilik" kila moja ina mkuu anayeitwa "Vali"; chini yake kuna maeneo yanayoitwa "kaymakamlık" (pia:ilçe) chini ya mkuu ambaye ni "Kaymakan". Ngazi ya chini ni miji na kata/ vijiji chini ya viongozi wanaochaguliwa na wananchi lakini ngazi za juu wanateuliwa na serikali.
Kwa hiyo ningesema valilik ni mkoa (hata kama kwa Kiingereza wanaweza kusema pia "province" halafu hata kama kilugha "valilik" asili yake ni sawa na Kiswahili "wilaya". Ila tu jinsi tunavyozoea wilaya Afrika ya Mashariki hii valilik ni zaidi mkoa na ngazi chini yake ni kama wilaya yetu. --Kipala (majadiliano) 08:03, 9 Julai 2009 (UTC)
Sawa. Lakini ukitazama Ardahan Province utakuta kitu kama Region: Eastern Anatolia Region, Turkey. Au waseme Marmara Region, Mediterranean Region, Turkey. Je, hapo napo nita tafsiri vipi? Hii ndiyo sababu iliyopelekea mimi kuita Majimbo kwa kufuatia "mkoa" unaonekana kuwa mdogo sana kwa maelezo yaliyoandikwa kule kwenye enwiki. Naomba soma makala ya enwiki na kisha nifahamishe kabla sijaendelea zaidi!--Mwanaharakati (Longa) 08:44, 9 Julai 2009 (UTC)
Tazama hii kutoka http://en.wikipedia.org/wiki/Eastern_Anatolia_Region
"Eastern Anatolia Region (Turkish: Doğu Anadolu Bölgesi) encompasses the eastern provinces of Turkey, and it is one of the 7 non-administrative subdivisions used for census purposes"
Maana ni kama "kanda" haina maana ya kiutawala au kisiasa kama Tanzania "mikoa ya kanda ya kusini" au ya "nyanda za juu za kusini" au "mikoa ya pwani". Wanatumia "kanda" hizi kwa kusudi la sensa na takwimu tu.--Kipala (majadiliano) 14:50, 9 Julai 2009 (UTC)
Basi mzee wangu haina tabu. Nitahamisha makala zote kwenda mkoani. Sikuwa najua namna ya kutaja zile. Hasa kwa mchanganyo. Kumbe ile region kwa kule inataja kanda? Basi ahsante sana. Kila la kheri.--Mwanaharakati (Longa) 08:01, 11 Julai 2009 (UTC)

Flowerparty awe mkabidhi

Nimemteua Flowerparty achaguliwe kuwa mkabidhi pamoja nasi. Naomba upige kura kwenye ukurasa wa Wakabidhi. Ahsante! --Mwanaharakati (Longa) 10:21, 9 Julai 2009 (UTC)

Kuondoa haki za usimamizi kwa baadhi ya watumiaji

Kipala, salam! Unatakiwa utoe mawazo yako juu ya kuondoshwa kwa haki za usimamizi kwa baadhi ya watumiaji wasionekana kwa kipindi kirefu sana. Orodha hiyo unaweza kuipata hapa. Ahsante na kila la kheri.--Mwanaharakati (Longa) 16:10, 10 Julai 2009 (UTC)

Hongera ya makala 12,000

Kipala, salam! Hongera kwa kusukuma Wikipedia yetu na kufikisha makala zaidi ya 12,000! Ninatumainia kuona michango yako mengine kibao kuliko hiyo uliyoifanya hapo awali!. Siku takii lolote lile, isikuwa kheri ya maisha. Wako kijana mtiifu, MuddybA.K.A.--Mwanaharakati (Longa) 13:00, 25 Julai 2009 (UTC)

Hongera ya makala 12,000

Kipala, salam! Hongera kwa kusukuma Wikipedia yetu na kufikisha makala zaidi ya 12,000! Ninatumainia kuona michango yako mengine kibao kuliko hiyo uliyoifanya hapo awali!. Siku takii lolote lile, isikuwa kheri ya maisha. Wako kijana mtiifu, MuddybA.K.A.--Mwanaharakati (Longa) 13:00, 25 Julai 2009 (UTC)

Bangla Desh?

Hi Kipala! Nina swali: Bangla Desh au Bangladesh? Umeanzisha hivyo. Flowerparty 19:21, 28 Julai 2009 (UTC)

Asante kwa kuona tatizo. Si kitu sana ni majina yote mawili yanayoonekana lakini Bangladesh ni kawaida zaidi. Nimeisahihisha. --Kipala (majadiliano) 20:10, 28 Julai 2009 (UTC)

Ok cool, ninakubali. Pia, asante kwa ukarimu :) Flowerparty 20:26, 28 Julai 2009 (UTC)

71 Wilaya ya Kenya

Hi, just a note, I wrote mbegu for the 71 wilaya of Kenya (for instance, Wilaya ya Meru Kati). I will wait until I see information regarding the disposition of the 234 wilaya, to write an updated set of stubs. Cheers. --Mr Accountable (majadiliano) 11:10, 3 Agosti 2009 (UTC)

Eire +

Thanks for your comments on Wilaya za Eire; I have made the suggested corrections. I am setting the AWB to create the mbegu for the Wilaya now. At this time, I have some lists of mbegu to create, viz Miji ya Kanada, Majimbo ya Brazil and the like. As far as Swahili is concerned, the language is very nice, very interesting, and I am very pleased to be here working and learning. It is a little frustrating, of course, but that is only because I am taking it seriously. One problem I have is that I am not perfectly certain, on the level of encyclopedic work, as to exactly what the title of a geo list article should be. So, in the future, when I prepare a geo table, for instance the regions of the Ukraine or the states of Austria, would it be alright if I wrote a message here asking what the best title of the list or article should be, and then create the table article after I have an answer? I mean, it is easy enough to know how to speak correctly in a casual setting, but as this is an encylopedic setting, I would rather check with somoeone instead of struggling with the title and then having to move the article after it is created. .... I assume you and other administrators would think this is a good idea, so I ask if the tables of Austrian states and Ukrainian regions now at Mtumiaji:Mr Accountable/Sandbox 2 could be checked and then the proper title written here. (Then en: links to the original data are on the page.) Thanks. --Mr Accountable (majadiliano) 16:13, 6 Agosti 2009 (UTC)

Ad limina apostolorum

Ndugu, nafurahi kusikia umerudi. Kimya chako cha muda mrefu kilinitia wasiwasi juu ya afya yako. Hongera kwa ziara yako Roma. Nadhani umefurahia hasa kaburi la mtume Paulo kama mimi nilivyolifurahia mwaka huu mwezi wa 5 kuliko mara zote nilizokwenda huko. Asante kwa kukamilisha jibu la Muddyb kuhusu picha. Sasa naelewa la kufanya kwa picha ambazo ziko katika wiki fulani lakini si katika Commons. Shalom! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:39, 7 Agosti 2009 (UTC)

Serikali

Hi, thanks for helping with the geography tables of Austria and Ukraine. .. I've started with putting together a table of government ministries and a list of "Federal institutions of Tanzania", please see Mtumiaji:Mr Accountable/Sandbox 2#Tebu; it's modeled on en:Federal institutions of Brazil, as well as those of Tanzania and Cambodia (which I myself started). As the list continues to be filled out, I may need advice on Kiswahili government agency names, especially when not provided directly at the website. Thanks again for your help. --Mr Accountable (majadiliano) 00:53, 10 Agosti 2009 (UTC)

The 100 Greatest Singers of All Time

Mzee wangu, salam. Ninashida ya kutaka kueleza tafsiri ya maneno haya:

    • The 100 Greatest Singers of All Time

Wakisema "of all time" wanamaanisha "karne" (miaka 100). Ima niendelee kutafsiri kama "Waimbaji Bora wa Muda Wote" au "Waimbaji Bora wa Karne"? Ipi ni bora zaidi... Wako kijana mtiifu,--Muddyb MwanaharakatiLonga 09:42, 10 Agosti 2009 (UTC)

Wanachosema ni uwongo lakini wanamaanisha "Waimbaji bora wa karne zote" au "nyakati zote". Lakini sidhani ya kwamba ni kweli. Hakuna anayeweza kujua waimbaji bora wa karne zote maana sisi tunajua wachache tu walio wengi wa zamani hatuna habari juu ya hao hasa kama ni watu wa zamani sana au watu wa utamaduni usio na mwandishi.
Je unataka kushughulika orodha ya Rollingstone? (http://www.rollingstone.com/news/coverstory/24161972/page/103). Hii ni kitu cha kimarekani kabisa! Hawajui kitu nje ya Western Pop music (kama ni kwa Kiingereza) halafu hawana habari za muziki wa Afrika wala Ulaya bara wala Asia. . . Ukitaka kushughulika mambo haya labda kwa kichwa kama "Orodha ya waimbaji bora kufuatana na rollingstone" --Kipala (majadiliano) 16:48, 11 Agosti 2009 (UTC)
Mmmhh, shuuu! Kweli mkubwa dawa! Naona unachosema ni cha kweli kabisaaa. Wao hawataji Waafrika wala Waasia. Lakini pia wameweza kukonga nyoyo za watu na kuwasadikisha kwamba ni kweli waimbaji bora wa muda wote kama jinsi alivyokuwa Wolfgang Mozart? Basi ahsante sana kwa maelezo yako yaliyojawa na msingi wa ukweli wa mambo. Nitaita kama jinsi ulivyosema hapo juu! Kila la kheri.--Muddyb MwanaharakatiLonga 06:34, 12 Agosti 2009 (UTC)

Kiswahili wikilugha ya kwanza ya Afrika

Ndugu, hongera kwako na kwa wenzetu wengine kwa kuchangia kufanya Kiswahili kuwa lugha ya Afrika yenye kurasa nyingi zaidi! Tumepiku Afrikaans! Tuendelee hivi kukuza lugha yetu! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 04:47, 16 Agosti 2009 (UTC)

13,000

Kipala, salam. Mzee wangu, si umeiona hiyo namba? Hongera kwa kutusukuma na kutushauri kwa muda wote.--Muddyb MwanaharakatiLonga 07:13, 18 Agosti 2009 (UTC)

Jamani, nashangaa! Hongera kwako na sisi sote!--Kipala (majadiliano) 08:39, 18 Agosti 2009 (UTC)

14,000

Kipala, salaaaam! Ninapenda kukutaarifu kwamba Wikipedia yetu imefikisha zaidi ya makala 14,000! Ni matumaini yangu kwamba tutafika elfu 15,000? Mmmh, ni safari ndefu! Labda hii kidogo inakukumbusha enzi zako za kusukuma gurudumu hili kutoka 140 hadi 1,000? Haikuwa kazi rahisi, lakini uliweza! Basi hongera kwa kuliwezesha na kila la kheri katika maisha! Ni mimi kijana wako mtiifu,--Muddyb MwanaharakatiLonga 14:42, 11 Septemba 2009 (UTC)

mradi wa Google kwa ajili ya wikipedia yetu

Mzee Kipala, salaam!
Nimepata mawasiliano kutoka Christine Moon huko Palo Alto, California. Yeye anafanya kazi kwa shirika la Google, nao wameanza kupanga mradi au huduma kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Tanzania na Kenya ili waelimishwe kuandika makala kwa wikipedia ya Kiswahili. Kumbe!
Christine sasa ametualika kumwandikia maoni yetu, angalia tovuti hiyo:
http://docs.google.com/Doc?docid=0AbIPJ9Nv6udZZGd6MndwcGdfMzFkODNzOG0zYw&hl=en
Bahati mbaya yeye haelewi Kiswahili, kwa hiyo itakuwa lazima kumwandikia kwa Kiingereza. Asante kwa michango yako!
Ni wako katika ujenzi wa lugha yetu, --Baba Tabita (majadiliano) 08:00, 10 Oktoba 2009 (UTC)

Alleluya na Alhamdulillah! Basi hoja zuri, nitachangia google.docs karibuni (sasa hivi bado tuko nyumba ya wageni hapa Tehran tukisubiri kuingia nyumba). Asante ---Kipala (majadiliano) 20:36, 10 Oktoba 2009 (UTC)
Nafurahi kusikia uko wapi. Nilikuogopea tena. Kazi njema!--Riccardo Riccioni (majadiliano) 21:12, 10 Oktoba 2009 (UTC)

mkutano wa Skype kesho kutwa

Mzee, salaam! Jumatatu tarehe 19, saa kuminamoja za mchana/jioni (yaani saa za Nairobi) tutajaribu kukutana kwenye Skype kwa ajili ya majadiliano kuhusu kuwahamasisha wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Kenya na Tanzania kutumia na kuichangia makala wikipedia ya Kiswahili. Mpaka sasa tupo wanne: Christine wa Google (mooncheech), Sj (metasj), Muddyb (mohammed.lupinga) nami (stegling). Ni tumaini langu kuwa utakuwepo. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 18:56, 17 Oktoba 2009 (UTC)

majadiliano kuhusu utafsiri wa istilahi

Mzee Kipala, salaam! Nimeanzisha majadiliano mapya kuhusu utafsiri wa istilahi ya wikipedia yetu hapa. Naomba uyaangalie na kuchangia maoni yako. Asante! --Baba Tabita (majadiliano) 09:36, 23 Oktoba 2009 (UTC)

Uingereza

Nimeongeza pendekezo lingine kwenye makala ya Uingereza, na kutoa mawazo kwenye ukurasa wa majadiliano. Ni kweli kwamba hii si jambo rahisi! Lloffiwr (majadiliano) 18:13, 7 Novemba 2009 (UTC)

Wikipedia:Makala ya wiki

Mzee Kipala, salam! Kumradhi kwa usumbufu. Ningependa uendelee kwa sababu kuna kesho! Nenda kwa Wikipedia:Makala ya wiki na mambo yatakuwa mazuri kabisaaa! Kila la kheri.--Muddyb MwanaharakatiLonga 14:24, 10 Novemba 2009 (UTC)

Kigezo cha jaribio

Salaam kutoka Ulaya. Nimejaribu kuongeza kigezo cha jaribio kama nilivyoeleza kwenye ukurasa wa jumuia. Sijapata 'feedback' kwa hiyo siwezi kumaliza shughuli. Umewahi kutoa mawazo kuhusu mada hii kwa hiyo nimeona vyema nikuulize unisaidie kwa kutoa mawazo tena. Lloffiwr (majadiliano) 13:58, 21 Novemba 2009 (UTC)

Usaidizi katika shindano

Kipala, salam. Ni tumaini langu kwamba umeona mabadiliko na maongezeko kadha wa kadha yaliyofanywa na wanafunzi hawa. Swali ni kwamba, tunaruhusiwa kuchangia au kusawazisha makala walizotunga? Au tuendelee kuwaacha tu wenyewe wafanye-wafanyavyo? Wako,--Muddyb MwanaharakatiLonga 09:18, 27 Novemba 2009 (UTC)

Swali zuri. Nimesahihisha makala ile moja ya Maungano ya Afrika kwa sababu nilishindwa kuisoma. Bado naona ni makala mabaya. Je nimefanya kosa nilipobandika kigezo cha FUTA? Sijafuatalia kwa undani je tunawapata hawa wanafunzi kwenye orodha fulani?
Au unaonaje kama si vile tuwape kigezo (Mshiriki wa mashindano....) ila tu baadaye tunahitaji kusafisha igezo hivi vyote?
Je ni sawa kuweka mapendekezo ya ufutaji kama kwa makala mengine (yaani nisipojua yeye ni mmoja wa mashindano??)
Eti Muddy unajua wewe kupeleka maswali haya kwa wenzetu wengine? Mimi nabanwa sana muda; kuna shughuli; katikati dakika tano ninaposubiri tu halafu naangalia wikipedia kama sasa ila sijui baada nukta mtu anakuja --Kipala (majadiliano) 10:06, 27 Novemba 2009 (UTC)
Haya, nitamwuliza SJ. Yeye ndiye mkuu na mratibu wa vigezo na kila kitu kwenye shindano hili! Pia, nimekuwa nikifuta makala mbalimbali pindi nionapo haziko sawa. Hofu yangu ni kwamba endapo zitakuwa nyingi na hatutakuwa na uwezo tena wa kuchunguza mojamoja, basi futa ukiona siyo. Pia, hawajui hata namna ya kujibu ujumbe kwa mtu aliyemwandikia - hii nayo shida na haitakuwa rahisi tena kuendelea kuwashauri ilhali wajibu! Pole na kazi. Ni yuleyule kijana wako,--Muddyb MwanaharakatiLonga 10:12, 27 Novemba 2009 (UTC)

Uchaguzi Mpya

Salam, Kipala. Unaombwa upige kura katika ukurasa wa wakabidhi wa Wikipedia. Mmoja kati ya wachangiaji wenzetu (Mr Accountable) amejiteua kuwa mkabidhi! Ili kumpgia kura, tafadhali fungua hapa. Ahsante sana.--Muddyb MwanaharakatiLonga 18:27, 28 Novemba 2009 (UTC)

Mwongozo

Wow, the tutorial looks great. --Mr Accountable (majadiliano) 00:13, 6 Desemba 2009 (UTC)

Yeah. lets wait if the "looks" help some reader. As long as the guys keep on dumping unfinished google-translate as articles... hmmm.

Miti

Salaam nafurahia kuona ya kwamba siku hizi umeangalia hata mahali ambako ndege hulala au kutafuta kivuli! --Kipala (majadiliano) 07:31, 10 Desemba 2009 (UTC)

Salaam. Nafurahi kama unapenda vile ninafanya. Nafikiri mimi ni mwanabiolojia wa pekee ambaye anaandikia wikipedia ya Kiswahili makala. Kwa hivyo lazima niandike kuhusu mada yoyote ya biolojia. ChriKo (majadiliano) 21:53, 10 Desemba 2009 (UTC)
Na kwanini tusijivunie kuwa na mwanabiolojia pekee kwenye wikipedia yetu? Basi hongera!!! Na ni tegemeo letu kuona mengi.--Muddyb MwanaharakatiLonga 06:41, 11 Desemba 2009 (UTC)
Asante sana Muddyb. ChriKo (majadiliano) 22:03, 11 Desemba 2009 (UTC)

Learning to use Submission pages

Many people need to be reminded to a) put the badge on their userpage, and b) follow the link from that badge!

See for instance Ogeya bphase's contribs. None of them are on his submissions page... On the "All submissions" page, try clicking on the "contribs" link next to the name of each participant, especially the ones with empty contributions - many of them are contributing but not taking credit. We can help them do it right the first time, then they will get it the second time. Sj (majadiliano)

Uhabeshi

Salaam, mzee wangu. Naomba uangalie tofauti hizi katika historia ya ukurasa wa Uhabeshi (yaani Ethiopia). Bahati mbaya, makala nzuri imefutwa na makala nyingine nzuri ikaingizwa. Je, utaweza kuunganisha miswada hiyo miwili? Nimeangalia nikashindwa. Pole! Hii KWC inaanza kunihangaisha saaana. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 09:51, 29 Desemba 2009 (UTC)