Majadiliano ya mtumiaji:Jonny Frosty

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Taarifa ya kukuzuia!

Ndugu, imenibidi kukuzuia kwa sababu zinazotajwa chini. Wakati unapokuwa umezuiwa huwezi kuhariri isipokuwa penye huu ukurasa wako wa majadiliano. Unaweza kunijibu kwa kutumia “Email this user”.

Sababu ni kuwa umeingiza matini iliyopatikana kwa njia ya tafsiri ya kompyuta ikiwa na kasoro nzito ya lugha. Umearifiwa kwamba ni marufuku kumwaga matokeo ya google translate katika makala zetu. Wachangiaji wanaopuuza utaratibu huu wanasababisha hasara kubwa kwa Wikipedia yetu na kuwapa wengine kazi kubwa mno ya kusafisha makosa yao.

Bila shaka una nia nzuri kuchangia katika Wikipedia. Tutafurahi kushirikiana nawe lakini ni lazima ufuate utaratibu. Kazi yetu kama wakabidhi ni kulinda mradi huu.

Ukiwa tayari kufuata utaratibu pamoja na kupitia upya matini ulizozileta tayari, naomba uwasiliane nami kwa kufungua ukurasa wangu (bofya jina langu chini) na kuniandikia baruapepe kwa kubofya “Email this user” upande wa kushoto. Hapo nitaweza kukuruhusu tena. Hapo lazima uwezeshe njia kwa kufuata maelezo katika Wikipedia:Email.

Ndugu umeonywa tayari kuhusu matumizi ya tafsiri ya kompyuta. Baada ya kuona kazi yako ya Cynthia E. Rosenzweig nimeona umemwaga tena tafsiri ya kompyuta bila masahihisho ya kutosha. Umeacha sentensi ambazo hazieleweki kama msomaji hajui matini ya Kingereza. Nimefuta makal hiyo. Maudhui yake nimehamisha Mtumiaji:Jonny Frosty/Cynthia E. Rosenzweig. Ilhali unazuiliwa kuhariri kwenye nafasi za makala, utaweza kusahihisha matini hiyo iliyopo kwenye nafasi yako ya mtumiaji na kuiswahilisha. Ninakushauri kuvunja sentensi za kiingereza na kueleza yale yasieleweka. Ukimaliza tafadhali niandikie Email nitaangalia kazi. Kipala (majadiliano) 19:00, 23 Mei 2023 (UTC)[jibu]

Habari, najaribu kurekebisha makala hio kwa njia ya mtumiaji lakini inashindikana bado nimezuiliwa kuhariri kwenye Mtumiaji:Jonny Frosty/Cynthia E. Rosenzweig Jonny Frosty (majadiliano) 11:44, 29 Mei 2023 (UTC)[jibu]
@Kipala Jonny Frosty (majadiliano) 13:04, 30 Mei 2023 (UTC)[jibu]
Tafadhali jaribu hapa: Majadiliano ya mtumiaji:Jonny Frosty/Cynthia E. Rosenzweig

Nipe taarifa kama unaweza kuhariri hapa. Kipala (majadiliano) 20:10, 2 Juni 2023 (UTC)[jibu]

@Kipala Hapana bado nashindwa kuhariri, ninaweza kutazama na kunakili tu. Jonny Frosty (majadiliano) 21:20, 2 Juni 2023 (UTC)[jibu]