Graviti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mwendo wa maji yanayotoka kwenye nozeli kuelekea juu unabadilishwa mwelekeo wake kwa umbo la parabola kutokana na nguvu ya graviti ya dunia

Graviti (pia: nguvu za uvutano, nguvu mvutano) ni kani ya uvutano iliyopo kati ya magimba yote ya ulimwengu. Kila gimba lenye masi linavuta magimba yote mengine yenye masi.

Hii ni sababu ya kwamba tunatembea duniani badala ya kuelea kwa sababu masi ya dunia inatuvuta kuelekea kitovu chake. Sisi tuna uvutano wa dunia pia lakini hali halisi kani hii ni ndogo mno kulingana na nguvu ya masi kubwa ya dunia. Wakati huohuo dunia yetu inavutwa na jua na hii ni sababu ya kwamba dunia inazunguka jua katika obiti na haiwezi kukimbia mbali nayo.

Tukitupa jiwe hewani itaanguka tena chini. Hii ni kwa sababu kani ya mkono ilipeleka jiwe kwa njia ya kwenda juu lakini kani ya uvutano wa dunia inairudisha.

Tabia ya kuvutana inaonekana vema kati ya dunia na mwezi. Dunia ni kubwa inauvuta mwezi na kuushika kwenye njia yake ya kuzunguka. Lakini wakati huohuo mwezi unavuta pia dunia na hii inaonekana baharini katika mabadiliko ya maji kupwa na maji kujaa. Maji ya bahari inavutwa na mwezi kiasi cha kwamba sehemu ya bahari iliyo moja kwa moja chini ya mwezi iko nusu mita juu ya wastani wa uso wa bahari yote.

Isaac Newton anajulikana kama mtaalamu aliyeweza kueleza graviti mara ya kwanza kama utaratibu wa kimsingi wa kisayansi.

Science.jpg Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Graviti kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.