Kupatwa kwa Mwezi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Picha za kupatwa kwa Mwezi tarehe 16 Juni 2011 kuanzia saa 4:41 usiku hadi saa 7:37

Kupatwa kwa Mwezi (en:lunar eclipse) ni hali ya Mwezi kutoonekana kisehemu au kabisa kwa muda mfupi hadi kuonekana tena kama mwezi mpevu. Badiliko hili linaweza kudumu kati ya saa moja hadi masaa matatu na nusu.

Sababu ya kupatwa kwa Mwezi[hariri | hariri chanzo]

Kupatwa kwa Mwezi kihatua ukiingia katika kivuli cha Dunia

Kupatwa kwa Mwezi kunasababishwa na kivuli cha Dunia kinachomwaga giza juu ya Mwezi kabisa au kisehemu. Hali hii inatokea wakati Mwezi - Dunia na Jua zinakaa katika mstari mmoja, ikiwa Dunia iko katikati ya Jua na Mwezi. Hapo kivuli cha Dunia inagusa Mwezi. Inatokea tu wakati wa mwezi mpevu. Hali hii ni kinyume cha kupatwa kwa Jua ambako Jua, Mwezi na Dunia ziko pia kwa mstari mmoja lakini hapo Mwezi uko kati ya Jua na Dunia na hapo ni Mwezi unaosababisha giza kenye uso wa ardhi pale ambako kivuli chake kinapita juu ya Dunia.

Kupatwa kwa Mwezi

Tofauti kati ya aina za kivuli wakati wa kupatwa kwa Mwezi[hariri | hariri chanzo]

Mara nyingi kupatwa kwa Mwezi si rahisi kutambua kwa sababu si kupatwa kikamilifu. Hapo Mwezi unapita katika nusukivuli cha Dunia tu. Nusukivuli ni hali ambako sehemu ya nuru inazuiliwa lakini sehemu nyingine bado inafika. Tofauti ya uangavu si kali sana.

Hali tofauti inatokea kama Mwezi unapita kwenye kitovu cha kivuli cha Dunia. Hapa tofauti ya uangavi ni kubwa na kuonekana kabisa. Mara nyingi kitovu cha kivuli kinafunika sehemu tu ya Mwezi na hapo tofauti inaonekana kwenye uso wa Mwezi jinsi tunavyouuna.

Wakati Mwezi wote umeingia katika kiini cha kivuli bado unaonekana kidogo, mara nyingi kwa rangi nyekundu. Sababu yake ni ya kwamba nuru ya Jua inapita katika angahewa ya Dunia na hapo inatawanywa. Kwa hiyo nuru ambayo bado inakisiwa na uso wa Mwezi si nuru inayofika moja kwa moja kutoka Jua bali sehemu ndogo ya nuru tu iliyotawanywa na angahewa. Hapo masafa ya mawimbi marefu hayatawanywi katika angahewa kirahisi kama masafa mafupi na hapo ndipo sababu ya rangi nyekundu.

Marudio[hariri | hariri chanzo]

Kupatwa kwa Mwezi kunatokea kila mwaka, angalau mara mbili hadi mara tano. Lakini mara nyingi mwezi hufunikwa kisehemu tu.[1] Kwa jumla 12,063 marudio ya kupatwa kwa Mwezi yamekadiriwa kwa kipindi cha miaka 5,000 kuanzia mwaka 1999 KK hadi 3000 BK.[2]


Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Matokeo ya kupatwa kwa Mwezi kati ya 2011 hadi 2020, tovuti ya NASA, iliangaliwa Julai 2012
  2. Periodicity of Lunar eclipses, tovuti ya NASA

Angalia pia[hariri | hariri chanzo]


Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: