Kichapishi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kichapishi cha IBM
Kichapishi cha IBM

Kichapishi (kutoka kitenzi "kuchapa"; pia: printa, kutoka Kiingereza "printer") ni kifaa kimojawapo cha kompyuta. Inaruhusu mtumiaji kuchapisha[1] maandishi kwenye karatasi, kama vile barua na picha.

Kwa kawaida kichapishi kipo chini ya udhibiti wa kompyuta yaani, inaendeshwa na kompyuta.

Wengi wanaweza pia kuifanya kazi kama mashine ya kutoa nakala kwa kutumia kichapishi au kwa kutumia kamera ya kidijiti ili kuchapisha moja kwa moja bila kutumia kompyuta.

Aina[hariri | hariri chanzo]

  1. Vichapishi vya mgongano (impact printers) hutumia vifaa mbalimbali vinavyopiga riboni inayopeleka wino kwenye karatasi. Vimepitishwa na vichapishi vya kisasa zaidi havitumiwi sana tena. Isipokuwa vichapishi vya sindano (dot-matrix printers) bado hutumiwa katika ofisi kwa sababu zinaweza kutoka nakala ya pili mara moja au kujaza fomu zilizochapishwa tayari. Kichapishi cha sindano huchora nukta nyingi zinazounda umbo la herufi.
  2. Kichapishi cha wino (inkjet printer) huwa na nozeli inayosogezwa haraka juu ya karatasi na kupuliza matone madogo ya wino kwene uso wake. Kwa njia hiyo inachora haraka herufi na pia picha. Mashine hizo ziapatikana kwa matumizi na rangi moja -kwa kawaida nyeusi- au rangi nne zinazounganishwa kuunda rangi nyingi. Vichapishi vya wino hupatikana kwa bei nafuu lakini mara nyingi wino yake huuzwa ghali. Sokoni kuna wino mbadala kwa bei nafuu lakini kuna uwezekano kwamba wino fulani haulingani na kifaa chenyewe.
  3. Kichapishi cha leza (laser printer) hutumia silinda yenye chaji ya umeme na wino ya unga. Mwanga wa leza hupita juu ya silinda na kubadilisha chaji kwenye uso wake hivyo kuchora picha ya matini au uchoraji. Wino yenye umbo la unga hupulizwa kwenye silinda na kushika kwenye sehemu zilizoathiriwa na leza. Karatasi hupitishwa kwenye silinda na kupokea wino ya unga. Karatasi inapita kwenye silinda ya joto ambako wino huwa imara. Mtindo huu kimsingi ni sawa na mfumo wa fotokopi.
  4. Kichapishi cha 3D kinatengeneza nakala ya vitu vyenye pandeolwa tatu. Mara nyingi hutumia plastiki na kujenga matokeo yake tabaka baada ya tabaka. Vichapishi vya 3D vya kiwandani hutumia pia metali au mata nyingine. Mashine kubwa huchapisha vitu vikubwa hadi nyumba.
  5. Printamtandao huweza kufikiwa na yeyote kupitia mtandao
  6. Printashiriki hupokea maagizo ya tarakilishi zaidi ya moja, ingawa kwa wakati mmoja huchapa kazi ya mojawapo tu.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Kuchapisha kulingana na Merriam Webster Dictionary ni mchakato ambapo mawazo ya kibinadamu yameandikwa kwa maneno kwenye karatasi
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.