Tianjin
天津市 | |
---|---|
Nchi | China |
Jimbo / Mkoa | (chini ya serikali kuu) |
Anwani ya kijiografia | 39°08′N 117°11′E / 39.133°N 117.183°E |
Eneo | km2 11,946 |
Wakazi | 15,621,200 |
Msongamano wa watu | 1,300/km2 |
Simu | 22 |
Tianjin (kwa Kichina: 天津), ni mji mkubwa katika China kaskazini.
Idadi ya wakazi ni 11,760,000 wanaoishi kwenye eneo la kilomita za mraba 11,917.
Mji huu ulianzishwa mwaka 1403 na kaisari Yongle kilomita 137 kutoka Beijing karibu na mdomo wa Mto Hai katika Bahari ya Bohai.
Tasnia ya kisasa ya mitambo na nguo ya China ilianza hapa. Tangu mwanzo wa Sera ya Mlango Wazi mwaka 1984, Tianjin iliongezwa maeneo mengi ya viwanda. Tangu 1994 hadi 2008, kiwango cha pato la taifa cha Tianjin kiliongezeka asilimia 12.5 kwa wastani kila mwaka.
Tianjin ni pia mahali pa kuanzishwa kwa chuo kikuu cha kwanza nchini China kwenye mwaka 1895. Mji huo una taasisi karibu zaidi ya elfu za sayansi na teknolojia, pamoja na wataalamu zaidi ya elfu 600 katika fani tofauti. Inayo idadi kubwa ya wataalamu maarufu na wasomi.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]Tianjin travel guide kutoka Wikisafiri
- Tianjin Government website
- China (Tianjin) Pilot Free Trade Zone Ilihifadhiwa 2 Novemba 2019 kwenye Wayback Machine.
- Economic profile for Tianjin at HKTDC
- Official Tianjin Media Gateway Ilihifadhiwa 20 Oktoba 2018 kwenye Wayback Machine.
- Historic US Army map of Tianjin, 1945
- Official promotional video of Tianjin City
Makala hii kuhusu maeneo ya China bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Tianjin kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |