Baobonye

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Baobonye ya kawaida kwa mfumo wa Marekani

Baobonye (keyboard) vilevile Bodidota/Bodi ya dota[1] (Kiswahili cha sasa) ni kifaa muhimu kinachomwezesha mtu kuweka maandishi na namba kwa tarakishi (kompyuta).

Kwa tarakishi nyingi ni kifaa kikuu cha kuingiza habari mashineni.

Kuna mifumo mbalimbali za baobonye kulingana na lugha.

Muundo wa kawaida kwa lugha zinazotumia alfabeti ya Kilatini ni QWERTY (hizi ni herufi 6 za kwanza).

Muundo huu unaweza kuchosha mikono na vidole. Ulianzishwa zamani za mashine za kupiga chapa na mfumo wa herufi ulilenga kutovurugisha mikono ya taipu. Siku hizi hakuna taipu tena lakini watu waliozoea muundo umebaki vile.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Kamusi ya Karne ya 21, UK: 40, EMAC BAKITA na KIE. ISBN: 998-702-097-6