Mwandiko wa Kichina

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mwandiko wa Kichina

Mwandiko wa Kichina ni jumla ya alama zinazotumiwa kuandika lugha za Kichina. Mwandiko huu hutumia alama moja kwa neno lote kwa hiyo kila mtu anaelewa mwandiko hata akisoma na kutamka tofauti katika lahaja mbalimbali.

Kichina huandikwa kwa alama zinazomaanisha neno moja si sillabi au herufi tu. Lakini maneno mengi ya Kichina yana silabi moja tu. Kamusi kubwa ya lugha ina alama zaidi ya 40,000- Wachina wasomi wenye elimu nzuri hujua takriban alama 6,000 hadi 7,000. Gazeti la kawaida hutumia alama 3,000. Serikali inasema mtu ajua kuandika na kusoma kama ameshika angalau alama 2,000.

Tangu mapinduzi ya Kichina ya 1949 serikali imesambaza alama zilizorahisishwa. Kuna pia mipango ya kulatinishi lugha yaani kuendeleza namna ya kuandika lugha kwa herufi za Kilatini.

Mwandiko wa Kichina ulikuwa pia msingi wa mwandiko wa Korea na Japani.