Mwandiko wa kikabari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Maendeleo ya mwandiko wa kikabari
safu 1: picha asilia;
safu 2: mwandiko uliorahisishwa wakati wa Hammurabi;
safu 3: wakati wa Ashuri;
safu 4: wakati wa Babeli Mpya mnamo 600 KK;
safu 5: maelezo ya picha asilia na maana ya silabi iliyopatikana baadaye

Mwandiko wa kikabari ni kati ya aina za mwandiko wa kale sana duniani ilikuwa kawaida katika Mesopotamia ya kale ukitumiwa na Wasumeri, Wababeli, Waashuri na wengine hata katika nchi jirani.

Ilianzishwa na Wasumeri mnamo mwaka 3,000 KK ikaishia baada ya mwaka 400 KK na mfano wa mwisho unaojulikana uliandikwa mwaka 75 BK.

Mwandiko picha mwanzoni[hariri | hariri chanzo]

Chanzo chake ilikuwa mwandiko wa picha zilizotumiwa kuandika habari. Mwandiko picha huu ulirahisishwa na kuonyeshwa baadaye kwa mistari mbalimbali badala ya kila picha.

Udongo wa ufinyanzi badala ya karatasi[hariri | hariri chanzo]

Mistari hii ilipatikana kutokana na njia ya kawaida ya kuandika: hapakuwa na karatasi lakini waandishi walitumia vipande vya udongo wa ufinyanzi kama ubao mdogo. Hapo waliandika kwa kijiti na mbinu huu ulileta alama zinazofanana na mistari yenye vichwa au "kabari". Vipande vya udongo wa ufinyanzi vilikaushwa na kuchomwa kama tofali. Kwa njia hii ziliweza kudumu katika mazingira pakavu kwa maelfu ya miaka.

Kwa matumizi ya haraka udongo haukukaushwa. Iliwezekana pia kufuta mwandishi yote kwa kusliba kipande cha udongo na kuandika upya kwa mfano kwa matumizi ya dukani na kadhalika.

Maandishi maalumu kama sheria za mfalme Hammurabi wa Babeli ziliandikwa pia cha kuchonga alama katika jiwe au mwamba lakini hii haikuwa njia ya kawaida.

Mabadiliko ya mwandiko[hariri | hariri chanzo]

Katika muda wa miaka 2000 ya matumizi yake mwandiko huo uliendelezwa jinsi inavyoonekana katika picha kwenye makala hii. Baada ya kuacha picha yenyewe alama zilitumiwa kama silabi hivyo mwandiko wa silabi ulijitokeza. Maana watu hawakuangalia tena maana asilia ya picha bali sauti yake tu jinsi ilivyo na herufi za alfabeti yetu.

Babu wa alfabeti yetu[hariri | hariri chanzo]

Baadaye mwandiko huu uliendelezwa kuwa mwandiko wa Wafinisia uliokuwa asili ya alfabeti ya Wagiriki iliyo mama ya alfabeti yetu ya Kilatini. Katika alfabeti ya Kilatini herufi ya "A" yaonekana hadi leo ya kwamba asili yake ilikuwa picha cha kichwa cha ng'ombe iliyogeuzwa.

Globe of letters.svg Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwandiko wa kikabari kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.