Kabari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kabari
Kupasua ubao kwa kabari na nyundo

Kabari (kwa Kiingereza wedge) ni chombo kinachotumiwa kwa kupasua kitu au gimba, pia kwa kutenganisha vitu viwili vilivyoshikamana. Umbo lake linafanana na pembetatu nyembamba.

Kifizikia inatumia kanuni za bapa betuko, hivyo inaitwa pia "mashine sahili".[1]

Matumizi ya kila siku ni kupasua shina la mti kuwa kuni au kupasua jiwe. Kimsingi hata uwezo wa kisu au shoka wa kukatia unafuata mfano wa kabari maana vyote hutegemea kanuni za bapa betuko.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Simple Machines. Georgia State University. Iliwekwa mnamo 12 January 2016.