Sigma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alfabeti ya Kigiriki
Herufi za kawaida
Α α Alfa 1 Ν ν Ni 50
Β β Beta 2 Ξ ξ Ksi 60
Γ γ Gamma 3 Ο ο Omikron 70
Δ δ Delta 4 Π π Pi 80
Ε ε Epsilon 5 Ρ ρ Rho 100
Ζ ζ Dzeta 7 Σ σ ς Sigma 200
Η η Eta 8 Τ τ Tau 300
Θ θ Theta 9 Υ υ Ipsilon 400
Ι ι Iota 10 Φ φ Phi 500
Κ κ Kappa 20 Χ χ Khi 600
Λλ Lambda 30 Ψ ψ Psi 700
Μ μ Mi 40 Ω ω Omega 800
Herufi za kihistoria1
Digamma 6 San 90
Stigma 6 Sho 90
Heta 8 Koppa 90
Sampi 900
1 Viungo vya Nje:
Alfabeti_ya_Kigiriki#Viungo_vya_Nje

Sigma (Σ σ ς) ni herufi ya 18 katika Alfabeti ya Kigiriki. Inaandikwa kama σ (alama ya kawaida) au Σ (alama kubwa mwanzoni mwa majina). Kama iko mwishoni mwa neno huandikwa ς. Mfano jina Ὀδυσσεύς (Odysseus) ambamo kuna σ mbili katikati na ς mwishoni.

Zamani za Kigiriki cha Kale ilikuwa pia tarakimu, ikiwa alama ya namba 200.

Asili ya sigma ni herufi ya Kifinisia ya shin 𐤔 .

Matamshi yake ilikuwa "s".

Katika alfabeti zinazofuata mfano wa Kigiriki ilipokelewa katika alfabeti ya Kilatini kama "S" na katika alfabeti ya Kikirili kama "С".