Ipsilon

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Upsilon uc lc.svg
Alfabeti ya Kigiriki
Herufi za kawaida
Α α Alfa 1 Ν ν Ni 50
Β β Beta 2 Ξ ξ Ksi 60
Γ γ Gamma 3 Ο ο Omikron 70
Δ δ Delta 4 Π π Pi 80
Ε ε Epsilon 5 Ρ ρ Rho 100
Ζ ζ Dzeta 7 Σ σ ς Sigma 200
Η η Eta 8 Τ τ Tau 300
Θ θ Theta 9 Υ υ Ipsilon 400
Ι ι Iota 10 Φ φ Phi 500
Κ κ Kappa 20 Χ χ Khi 600
Λλ Lambda 30 Ψ ψ Psi 700
Μ μ Mi 40 Ω ω Omega 800
Herufi za kihistoria1
Digamma uc lc.svg Digamma 6 San uc lc.svg San 90
Stigma uc lc.svg Stigma 6 Sho uc lc.svg Sho 90
Heta uc lc.svg Heta 8 Qoppa uc lc.svg Koppa 90
Sampi uc lc T-shaped.svg Sampi 900
1 Viungo vya Nje:
Alfabeti_ya_Kigiriki#Viungo_vya_Nje

Ipsilon (pia: Ypsilon au kigiriki Ύψιλον "i fupi") ni herufi ya 20 katika alfabeti ya Kigiriki ikawa baadaye herufi ya 25 katika alfabeti ya Kilatini. Iliandikwwa kama Y ya Kiswahili lakini ilikuwa vokali si konsonanti.

Katika Kigiriki cha Kale ilitaja pia namba 400.

Waroma waliipokea mara mbili katika alfabeti ya Kilatini:

  • mwanzoni katika karne za KK kupitia Kietruski kwa umbo la V lililomaanisha mara sauti ya "u" mara ya "w/v".
  • baada ya kuenea kwa utawala wao hadi Ugiriki katika karne ya 1 KK na kupokea maneno mengi ya Kigiriki.

Ipsilon ya kigiriki ilitaja vokali iliyokuwa kati ya "u" na "i" (kama Kijerumani "ü"); katika Kigiriki cha kisasa ni "i" pekee.

Asili yake ilikuwa Waw ya Kifinisia.