Nikaragua
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Pro Mundi Beneficio (Kilatini: Kwa salama ya dunia) | |||||
Wimbo wa taifa: Salve a ti, Nicaragua (Usalimiwe Nikaragua) | |||||
Mji mkuu | Managua | ||||
Mji mkubwa nchini | Managua | ||||
Lugha rasmi | Kihispania (kitaifa) (Kiingereza, lugha 6 za kienyeji kimahali kwenye pwani ya Karibi) | ||||
Serikali | Jamhuri Daniel Ortega | ||||
Uhuru Imetangazwa Imetambuliwa |
15 Septemba 1821 25 Julai 1850 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
130,000 km² (ya 97) 14.01 | ||||
Idadi ya watu - Julai 2012 kadirio - Msongamano wa watu |
6,071,045 (ya 108) 51/km² (ya 155) | ||||
Fedha | Cordoba (NIO )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC-6) (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .ni | ||||
Kodi ya simu | +505
- |
Nikaragua (pia Nikaragwa) ni nchi ya Amerika ya Kati yenye wakazi 6,071,045 (2012). Imepakana na Honduras na Kosta Rika; upande wa magharibi ni pwani ya Pasifiki na upande wa mashariki kuna pwani ya Bahari ya Karibi.
Jina la nchi linasemekana kuwa mchanganyiko wa jina la wakazi asilia walioitwa "Nikarao" na neno la Kihispania la "agua" (=maji) kutokana na maziwa makubwa mawili nchini yanayoitwa Lago Managua na Lago Nicaragua. Maelezo mengine yanamtaja chifu wa wazalendo wakati wa kufika kwa Wahispania aliyeitwa "Nikarao".
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Nikaragua ina volkeno nyingi; nyororo ya milima ya kivolkeno hufuata mstari wa pwani ya Pasifiki.
Sehemu ya juu ni mlima Mogoton wenye kimo cha mita 2,438 juu ya UB.
Maziwa makubwa mawili ya maji matamu ni Lago Managua na Lago Nicaragua.
Eneo upande wa Karibi lina wakazi wachache sana: ni hasa eneo la misitu minene.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Nchi ilikuwa koloni la Hispania tangu mwaka 1524.
Mwaka 1821 iliachana na utawala wa Hispania pamoja na nchi jirani na kuingia katika Shirikisho la Amerika ya Kati.
Tangu mwaka 1854 imekuwa nchi ya kujitegemea kabisa.
Wakazi
[hariri | hariri chanzo]Wakazi walio wengi sana hukalia maeneo ya mji mkuu Managua na pwani ya Pasifiki.
Sehemu kubwa (69 %) ni machotara kati ya wakazi asilia na Wazungu. 7% ni Wazungu. 9% wana asili ya Afrika, wakikaa hasa kwenye pwani Ya Bahari ya Karibi. Waindio ni asilimia 5.
Lugha rasmi na kubwa zaidi ni Kihispania, lakini si lugha pekee.
Upande wa dini, walio wengi ni Wakatoliki (61.5% kadiri ya sensa ya mwaka 2005) na Waprotestanti (30.6%). 15.1% hawana dini yoyote.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Visit Nicaragua
- Nicaragua Spanish Language Schools NSLS
- Nicaragua Economy Ilihifadhiwa 5 Machi 2016 kwenye Wayback Machine.
- Taarifa za jumla
- Nicaragua entry at The World Factbook
- Nicaragua Corruption Profile Ilihifadhiwa 24 Machi 2014 kwenye Wayback Machine. from the Business Anti-Corruption Portal
- Nicaragua Ilihifadhiwa 7 Juni 2008 kwenye Wayback Machine. at UCB Libraries GovPubs
- Nikaragua katika Open Directory Project
- Nicaragua profile from the BBC News
- Wikimedia Atlas of Nicaragua
- Maps from WorldAtlas.com
- Nicaraguaportal Ilihifadhiwa 7 Novemba 2014 kwenye Wayback Machine.: Official information of the Honorary Consulate of Nicaragua
- Key Development Forecasts for Nicaragua from International Futures
- Sanaa na utamaduni
- Nicaraguan Art Ilihifadhiwa 13 Juni 2019 kwenye Wayback Machine. Art and Literature by Nicaraguans
- Mengineyo
- The State of the World's Midwifery – Nicaragua Country Profile Ilihifadhiwa 12 Mei 2013 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika ya Kati bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Nikaragua kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |