Vita ya Marekani dhidi Hispania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uchoraji wa Kimarekani wa 1898 ulionyesha himaya mpya yenye upanuzi wa maili 10,000 kati ya Ufilipino na Kuba

Vita ya Marekani dhidi ya Hispania ilitokea mwaka 1898. Ilianza kwa shambulizi la Marekani tarehe 25 Aprili dhidi ya Puerto Rico iliyokuwa koloni la Hispania na kuishia tarehe 12 Agosti 1898, jeshi la Hispania katika Manila (Ufilipino) lilipojisalimisha.

Hivyo Marekani ilitwaa makoloni ya Hispania ya Puerto Rico, Kuba na Ufilipino.

Vita hii ilikuwa mwanzo wa Marekani kufuata siasa ya nje ya upanuzi hata katika maeneo ya mbali. Kabla ya vita hii Marekani ilishughulika kupanua eneo lake kwenye bara la Amerika ya Kaskazini dhidi ya wakazi asilia na dhidi ya Mexiko.

Marekani ilitumia nafasi ya ghasia ya wenyeji wa Kuba dhidi ya utawala wa kikoloni wa Hispania. Baada ya mlipuko kwenye manowari ya Marekani USS Maine katika bandari ya Havana, Marekani ilitangaza vita dhidi ya Hispania ingawa sababu ya mlipuko haijajulikana hadi leo ilikuwa nini.

Hispania haikuweza kushindana na manowari na silaha za Marekani zilizokuwa zimeendelea kiteknolojia. Pia Marekani ilikuwa karibu na mahali pa vita na Hispania ilishindwa kuongeza wanajeshi na silaha.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vita ya Marekani dhidi Hispania kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.