Nenda kwa yaliyomo

Funguvisiwa la Karolini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Eneo la funguvisiwa hilo.

Funguvisiwa la Karolini (kwa Kiingereza: Caroline Islands) ni funguvisiwa la Mikronesia lililosambaa sana katika Bahari ya Pasifiki hadi umbali wa kilomita 3,540[1]. Ni visiwa vidogo 500 hivi vyenye asili ya matumbawe.

Sehemu kubwa ni ya Shirikisho la Mikronesia, ila Palau ni nchi huru ya pekee.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Visiwa vimekaliwa na watu tangu miaka 4,000 iliyopita, hasa kutoka Rasi ya Malay na visiwa vya Indonesia. Wengine wametokea visiwa vya Polinesia.

Kisiwani Yap kulitokea dola na utawala wa kifalme.

Tangu kufika kwa Wahispania katika karne ya 16 visiwa vilikuwa chini ya ubwana wa nje lakini maisha ya kawaida yaliendelea bila mabadiliko makubwa kwa muda mrefu.

Mwisho wa karne ya 19 Hispania iliuza koloni hilo kwa Ujerumani; utawala wa Kijerumani ulikwisha katika Vita vikuu vya kwanza ukachukuliwa na Japani hadi mwisho wa Vita vikuu vya pili.

Japani ilifuatwa na Marekani iliyoendelea kutawala kwa niaba ya UM hadi uhuru (mwaka 1986 kwa shirikisho na 1994 kwa Palau).

  1. "Distance from Tobi Island to Kosrae". Google. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-01-06. Iliwekwa mnamo 2021-11-15.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.