Nenda kwa yaliyomo

Rasi ya Malay

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rasi ya Malay
Rasi ya Malay

Rasi ya Malay (Kimalay: Semenanjung Tanah Melayu) ni rasi kubwa katika Asia ya Kusini-Mashariki.[1]

Ina sehemu tatu zilizo chini ya nchi tofauti:

  • Kaskazini-magharibi yake ni eneo la kusini kabisa ya Myanmar (Burma)
  • Katikati yake ni eneo la Uthai
  • Kusini ni eneo la Malaysia ya magharibi

Kusini kabisa kwake, karibu na ncha ya rasi, iko nchi ya Singapuri kwenye kisiwa

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Rasi ya Malay iko kati ya Bahari Hindi na Pasifiki. Upande wa Pasifiki ni Ghuba ya Uthai na Bahari ya Uchina. Mlango wa Malakka unatenganisha rasi na kisiwa cha Sumatra.[2]

Rasi inaanza kwenye latitudo ya +13 na kuelekea kusini hadi latitudo ya +1. Urefu wake ni km. 1,555. Sehemu nyembamba iko katika sehemu ya Kithai yenye km 60 pekee.

Sura ya nchi ina tabia mbalimbali: milima, tambarare, maziwa, pwani na misitu minene.

Milima ya juu ni Gunung Tahan (m 2,187) na Gunung Korbu (m 2,184) nchini Malaysia. Katika tambarare za Uthai iko Khao Luang (m 1,786). Sehemu ya Myanmar kuna Recho Taung (m 1,330).

  1. The Physical Geography of Southeast Asia, Avijit Gupta
  2. Reid, Anthony (2010). Imperial alchemy : nationalism and political identity in Southeast Asia. Cambridge University Press. uk. 95. ISBN 978-0-521-87237-9.
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Rasi ya Malay kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.