Nenda kwa yaliyomo

Intaneti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Internet)
Picha ya njia mbalimbali katika sehemu ya intaneti.

Intaneti (kutoka Kiingereza Internet) ni mfumo wa kushirikiana kwa tarakilishi nyingi unaowezesha watu mbalimbali duniani kuwasiliana baina yao. Kupitia mtandao huo, watu huweza kutembelea tovuti mbalimbali, kupiga gumzo, na kuandikiana barua pepe.

Intaneti ni mfumo wa kimataifa wa mitandao ya tarakilishi inayotumia itifaki inayokubalika ya intarnet Suite (TCP/IP). Intaneti hubeba safu kubwa ya huduma na rasilimali za habari hasa hati za HyperText zilizoshikanishwa za wavuti wa ulimwengu mzima (www) na miundombinu ya kusaidia barua pepe.

Mbinu nyingi za jadi za mawasiliano ya habari, kama vile huduma za rununu na runinga, zimeundwa upya kutumia teknolojia za tovuti, na kusababisha huduma kama vile itifaki ya kupitisha sauti kwa kutumia tovuti (VoIP) na IPTV. Uchapishaji magazeti umeundwa upya katika tovuti, ubadilishanaji maoni, na kupatikana habari zinapotokea tu. Intaneti imewezesha au kuharakisha uundaji wa aina mpya za mafungamano za kibinadamu kupitia ujumbe mbashara, majukwaa ya tovuti na mitandao ya kijamii.

Kuna mawasiliano ya tarakilishi pamoja na habari zinazotunzwa kwenye mashine na kupatikana kwa programu za kutafuta wavuti (kama google) au kwa kamusi elezo kama wikipedia.

Asili ya intaneti ina mizizi katika miaka ya 1960 wakati Marekani ilifadhili miradi ya utafiti wa makala zake za kijeshi na kujenga mitandao iliyosambaa ya tarakilishi ambazo zina uwezo wa kustahimili mabadiliko na ni vumilivu kwa makosa. Kipindi hiki cha utafiti na ufadhili wa raia wa Marekani wa uti mpya wa mgongo uliofanywa kwa msingi wa kitaifa wa sayansi, ulisababisha dunia yote kushiriki katika maendeleo ya teknolojia mpya. Pia ulisababisha ufanyajibiashara wa tovuti za kimataifa katikati ya miaka ya 1990, na kusababisha kujulikana kwa zana nyingi karibu kila uwanja wa maisha ya kisasa ya binadamu. Kufikia mwaka wa 2009, wastani wa robo ya idadi ya watu duniani hutumia huduma ya tovuti.

Istilahi

Maneno intaneti[1] na mtandao wa ulimwengu mzima mara nyingi hutumika bila tofauti kubwa. Hata hivyo, intaneti na mtandao wa ulimwengu mzima si kitu kimoja, wala hazina maana sawa. Intaneti ni mfumo wa kimataifa wa mawasiliano ya data. Ni miundombinu ya vifaa na programu ambayo huwezesha mawasiliano kati ya kompyuta. Kwa kulinganisha, mtandao ni mojawapo ya huduma inayowasilishwa na intaneti. Ni mkusanyiko wa nyaraka zilizounganishwa na rasilimali nyingine, zilizoshikanishwa na viungo na URL. [2]

Historia

Uzinduzi wa Sputnik na USSR ulichochea Marekani kuanzisha shirika la utafiti wa juu wa miradi, iliyojulikana kama ARPA, katika mwezi Februari 1958 ili kuongoza kiteknolojia.[3] [4] ARPA ilitengeneza ofisi ya teknolojia za kuchambua habari (IPTO) ili kuendeleza utafiti wa programu inayojitekeleza ya mazingira ya chini (Sage), ambayo iliunganisha mifumo ya rada za nchi nzima kwa mara ya kwanza.

J. C. R Licklider alichaguliwa kuwa kiongozi wa IPTO. Licklider alihama kutoka maabara ya masomo yanayochunguza jinsi ubongo wa binadamu unavyofasiri sauti katika Chuo Kikuu cha Harvard MIT mwaka 1950, baada ya kuvutiwa na teknolojia ya habari. Akiwa MIT, alikuwa kwenye kamati iliyoanzisha Maabara ya Lincoln na kufanya kazi ya mradi wa Sage. Mwaka wa 1957 akawa Makamu wa Rais katika BBN, ambapo alinunua kompyuta ya kwanza ya PDP-1 na kuongoza maonyesho ya kwanza ya ugawanaji muda.

Akiwa IPTO, Licklider alimleta Lawrence Roberts ili aanzishe mradi wa kutengeneza mtandao, na Roberts alikita msingi wa teknolojia katika kazi ya Paulo Baran, [5] ambaye alikuwa ameandika masomo kamili kwa Wanajeshi wa waangani wa Marekani akipendekeza ubadilishaji pakiti (badala ya ubadilishaji mzunguko) ili kupata mtandao bora unaobadilika na unaoweza KUstahimili janga. Profesa wa UCLA Leonard Kleinrock alikuwa ametoa msingi wa nadharia ya pakiti za mitandao mwaka 1962, na baadaye, katika mwaka 1970, wa upitishaji wa kiviwango, dhana ambazo zimekuwa msingi wa maendeleo ya intaneti ya leo.

Baada ya kazi nyingi, sehemu mbili za kwanza ambazo zingekuwa ARPANET ziliunganishwa kati ya Shule ya Uhandisi na Sayansi Tumikizi ya UCLA na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti ya Stanford (SRI) katika bustani ya Menlo, California, tarehe 29 Oktoba 1969. ARPANET ilikuwa moja ya mitandao tangulizi ya mtandao wa intaneti ya leo. Kufuatia maonyesho kuwa ubadilishaji pakiti ulifanya kazi kwa ARPANET, kituo cha posta cha Uingereza, Telenet, TRANSPAC na DATAPAC zilishirikiana kuunda mtandao wa kwanza wa huduma ya ubadilishaji pakiti. Nchini Uingereza, hii ilikuwa inajulikana kama huduma ya kimataifa ya ubadilishaji pakiti (IPSS), mwaka 1978. Mkusanyiko wa mitandao yenye msingi wa X.25 ilikua kutoka Ulaya na Marekani na kutanda Kanada, Hong Kong na Australia kufikia mwaka 1981. Sheria ya ubadilishaji pakiti ya X.25 ilitengenezwa katika CCITT (sasa inaitwa ITU-T) mwaka 1976.

X.25 ilikuwa huru kutoka itifaki ya TCP/IP ambayo iliinuka kutokana na kuwa kazi ya majaribio ya DARPA kwenye ARPANET, mtandao wa Pakiti za Redio na Mtandao wa Pakiti ya Setilaiti wakati mmoja. Vinton Cerf na Robert Kahn walitengeneza maelezo ya kwanza ya itifaki ya TCP mwaka 1973 na kuchapisha karatasi kuhusu mada hii katika mwezi Mei 1974.

Matumizi ya neno "Internet" kuelezea mtandao mmoja wa kiulimwengu wa TCP/IP yalianza katika mwezi Desemba 1974 na uchapishaji wa RFC 675, yakiwa maelezo kamili ya kwanza ya TCP iliyoandikwa na Vinton Cerf, Yogen Dalal na Carl Sunshine, waliokuwa katika Chuo Kikuu cha Stanford. Katika miaka tisa iliyofuata, kazi iliendelea kurekebisha itifaki hizo na kuzitekeleza katika mifumo ya oparesheni ya aina mbalimbali. Mtandao wa Kwanza wenye upana mkubwa wa msingi wa TCP / IP ulikuwa ukifanya kazi kufikia tarehe 1 Januari 1983 wakati ambapo viwekaji vyote vya ARPANET vilibadilishwa kutoka itifaki za hapo awali za NCP. Mwaka 1985, Wakfu wa Sayansi wa kitaifa Marekani (NSF) uliamuru ujenzi wa NSFNET, uti wa mgongo wa mtandao wa chuo kikuu wenye kasi ya kilobaiti 56 kwa sekunde kwa kutumia kompyuta zilizoitwa "fuzzballs" na mvumbuzi wake, David L. Mills. Mwaka uliofuata, NSF ilifadhili ubadilishaji hadi mtandao wenye kasi ya juu zaidi ya megabaiti 1.5 kwa sekunde. Maamuzi muhimu kutumia itifaki za DARPA TCP/IP ulifanywa na Dennis Jennings, aliyekuwa msimamizi wa programu ya kompyuta zenye nguvu huko NSF.

Ufunguzi wa mtandao huo kwa maslahi ya kibiashara ulianza mwaka wa 1988. Baraza ya Mitandao ya Kimajimbo Marekani ilikubali ushikanishaji wa NSFNET na mfumo wa barua wa MCI katika mwaka huo, kiungo kilifanywa katika msimu wa joto wa mwaka wa 1989. Huduma zingine za kielektroniki za kibiashara zilishikanishwa zikiwemo: OnTyme, Telemail na Compuserve. Katika mwaka huo, watoaji wa huduma ya Intanet watatu waliundwa: UUNET, PSINet na CERFNET. Muhimu, mitandao tofauti iliyotoa viingilio, na baadaye kuungana na Intanet ilikuwa BITNET na Usenet. Mitandao mingine ya kibiashara na elimu kama Telenet, Tymnet, Compuserve na JANET iliunganishwa na Intanet iliyokuwa ikikua. Telenet (iliyoitwa Sprintnet baadaye ) ulikuwa mtandao mkubwa wa kompyuta wa kitaifa uliofadhiliwa kibinafsi, wenye upigaji simu ya intaneti burekatika miji, kote Marekani na uliyokuwa ukifanya kazi tangu mwongo wa 1970. Hatimaye, mtandao huu uliunganishwa na mingine katika mwongo wa 1980 wakati ambapo itifaki ya TCP / IP iliendelea kuwa maarufu zaidi. Uwezo wa TCP/IP kufanya kazi kwa karibu mtandao wowote wa mawasiliano uliruhusu ukuaji rahisi, ingawa ukuaji wa haraka wa Intanet ulikuwa juu ya upatikanaji rahisi wa safu ya vielekezi vya kibiashara kutoka makampuni mengi, upatikanaji wa vifaa vya kibiashara vya Ethanet ya mitandao ya mitaa, na kuenea kwa utekelezaji na uwekaji sheria mkali wa TCP / IP katika UNIX na karibu kila mfumo mwingine wa oparesheni.

Ingawa vifaa msingi na miongozo vinavyofanya uwezekanaji wa intanet vimekuwepo kwa karibu miongo miwili, mtandao huo haukupata kuona nyuso za umma mpaka mwongo wa 1990. Tarehe 6 Agosti 1991, CERN, shirika ya Ulaya ya utafiti wa chembe, ulieleza umma kuhusu mradi mpya wa matandao wa dunia nzima. Mtandao ulizuliwa na mwanasayansi waKiingereza Tim Berners-Lee mwaka wa 1989. Kivinjari cha mtandao kilichokuwa cha kwanza na chenye umaarufu sana kilikuwa ViolaWWW, iliyofuata mtindo wa HyperCard na kujengwa kwa kutumia mfumo wa X Window. Hatimaye ilichujwa na umaarufu wa tovuti ya Mosaic. Mwaka wa 1993, Kikao kikuu cha zana za kompyuta zenye nguvu katika Chuo Kikuu cha Illinois ilitoa aina ya kwanza 1.0 ya Mosaic, na mwisho wa mwaka wa 1994 hamu ya umma iliongezeka Intanet ambayo hapo awali ilikua ya taaluma na ufundi. Kufikia mwaka 1996 matumizi ya neno Intaneti yalikuwa kawaida, na kwa hiyo, hata matumizi yake kama kisawe cha mtandao wa ulimwengu mzima.

Muongo huo ulipoendelea, intaneti ilifanikiwa kushughulikia mitandao mingi binafsi wa awali (ingawa baadhi ya mitandao, kama FidoNet, vimebaki tofauti). Katika miaka ya 1990, ilikuwa inakadiriwa kwamba intaneti ilikua kwa asilimia 100 kila mwaka, na kipindi kifupi cha mwaka wa 1996 na 1997 ukuaji wake ulilipuka. [6] Ukuaji huo ulitokana na ukosefu wa utawala mkuu, ambao unaruhusu ukuaji wa kikaboni wa mtandao, na pia ukosaji ubinafsi na huru katika itifaki za intaneti, ambao unahamasisha ubadilishaji wauzaji na kuzuia kampuni yoyote kuwa na udhibiti mkubwa wa mtandao. [7] Makadirio ya idadi ya watumiaji wa internet ni bilioni 1.67 kufikai 30 Juni 2009. [8]

Teknolojia

Itifaki

Ugumu wa miundombinu ya mawasiliano ya Intanet unahusisha vipengele vya vifaa vyake na sehemu za mfumo wa progamu inayodhibiti tabaka mbalimbali za usanifu. Ingawa vifaa vinaweza kutumika kusaidia mifumo mingine ya programu, ni urasimu na mifumo ya sheria za usanifu wa programu zinazoainisha Intanet na hutoa msingi wa ukubwa wake na mafanikio yake. Wajibu wa urasimu wa usanifu wa mifumo ya programu za Intanet umepewa tume ya uhandis wa Intanet (IETF). [9] IETF huongoza makundi ya kuweka sheria, wazi kwa mtu yeyote, kuhusu masuala mbalimbali ya usanifu wa Intanet. Majadiliano yanayotokea na amri za mwisho huchapishwa katika mfululizo wa machapisho, iitwayo Kuomba kwa Maoni (RFC),ipatikanayo bure kwenye tovuti ya IETF. Mbinu muhimu za utengenezaji wa mitandao zinazowezesha Intanet ziko katika RFC teule yenye sheria za Intanet.

Sheria hizi hueleza msingi unaojulikana kama Itifaki ya Intanet. Hii ni kielelezo cha usanifu unaogawanya huduma kuwa visehemu katika itifaki ya mfumo(RFC 1122, RFC 1123). Visehemu hivi vina uhusiano na mazingira au upeo ambao huduma zao hufanya kazi. Sehemu ya juu ni Sehemu ya zana, nafasi iliyotengwa kwasababu ya mbinu za utenegnezaji mitandao zinazotumika katika zana za programu, mfano, kivinjari. Chini ya sehemu hii ya juu, kuna sehemu ya Usafiri iunganishayo zana katika kompyuta tofauti kupitia mtandao (mfano, client-server) na mbinu sahihi za kubadilishana takwimu. Chini ya sehemu hizi ndipo kulipo na msingi wa teknolojia ya mitandao, linalojumuisha sehemu mbili. Sehemu ya Intanet inayowezesha kompyuta kutambuana kupitia anwani za Itifaki ya internet(IP), na huziwezesha kuungana pamoja kwa kutumia mitandao zilizo karibu. Mwisho, chini ya usanifu huu, ni sehemu ya programu , na sehemu ya uunganishaji, ambayo huwezesha kuungana kwa kompyuta zilizo katika kiunganishi sawa wa mtandao ya mtaa , kama vile mtandao wa eneo(LAN) au uunganishi wa kupiga. Mfano huu, ujulikanao pia kama TCP / IP, ni iliyoundwa isitegemee vifaa inavyotumia, kwa hivyo mfano huu hauna haja ya kujishughulisha na maelezo yoyote. Mifano mingine vimeundwa, kama vile mfano wa mifumo ya kiunganishi kilichofunguka (OSI) , lakini si sawa katika maelezo ya ufafanuzi, wala utekelezaji, lakini kufanana kupo n itifaki ya TCP / IP hujumuishwa katika majadiliano ya mitandao ya OSI .

Sehemu maarufu zaidi ya picha simamizi ya Intanet ni Itifaki ya Intanet (IP) ambayo hushughulikia upeanaji wa (anwani za IP) kwa kompyuta zilizo katika Intanet. IP inawezesha ushikanishaji wa mitandao na kimsingi hujenga Intanet yenyewe. Toleo ya 4 ya IP (IPv4) ni toleo lililotumiwa katika kizazi cha kwanza cha Intanet ya leo na bado yatumika vikubwa. Iliundwa kushughulikia hadi watumiaji billioni~ 4,3 (10 9) wa intanet. Hata hivyo, kulipuka kwa ukuaji wa Intanet umesababisha kuisha kwa anwani za IPv4 ambayo inakadiriwa kuingia hatua yake ya mwisho katika takriban mwaka wa 2011. [10] Toleo ya itifaki mpya, IPv6, iliundwa katikati ya mwongo wa 1990. Toleo hili linauwezo mkubwa wa kupeana anwani na mbinu bora zaidi ya uelekezaji wa trafiki ya Intanet. IPv6 kwa sasa ipo katika awamu ya kuachiliwa kibiashara duniani mashirika ya kuweka anwani za intanet(RIR) yameanza kuwahimiza mameneja wote wa rasilimali kupanga uchukuzi na uongofu wa haraka. [11]

IPv6 haishirikiani kikazi na IPv4. Kimsingi toleo la IPv6 hutengeneza toleo "sambamba" la Intanet ambalo halipatikani moja kwa moja na IPv4. Hii ina maanisha uboreshaji wa Programu au vifaa vya ukalimani ni muhimu kwa kila kifaa cha mtandao ambacho linahitaji kuwasiliana kupitia Intanet ya IPv6. Mifumo ya kuendesha kompyuta ya kompyta za kisasa tayari vimebadilishwa ili vifanye kazi na toleo zote za itifaki ya Intanet. Miundombinu ya mtandao , hata hivyo, bado yamebaki nyuma katika maendeleo hayo. Mbali na tata za viungo vinavyotengeneza miundombinu yake, Intanet imewezeshwa na mikataba ya kibiashara (mfano, mkataba wa kujitakia), na kwa ufundi maalum au itifaki zinazoeleza jinsi ya kubadilishana data kwa kupitia mtandao. Hakika Intanet ina ainishwa na viungo vyake na sheria za uelekezaji.

Muundo

Muundo wa Intanet na sifa za matumizi yake vimekuwa vikisomwa kwa undani. Imedhamiria kuwa muundo wa uelekezaji katika Intanet ya IP na viungo vya hypertext vya mtandao wa dunia nzima ni mifano ya mitandao isiyo na kipimo. Sambamba na jinsi watoa huduma, wa kibiashara za Intanet huwasiliana kwa kupitia sehemu za ubadilishanaji habari, mitandao ya utafiti kwa kawaida huunganishwa kupitia mitandao mikubwa kama GEANT, GLORIAD, Internet2 (halifa wa Mtandao wa Abilene ), na mtandao wa utafiti na kitaifa na elimu wa Uingereza, JANET. Mitandao hii imeundwa kutoka kwa mitandao mingine midogo (pia tazama orodha ya mashirika ya kiakademia ya mitandao ya kompyuta).

Wanasayansi wengi wa Kompyuta huelezea Intanet kama "mfano halisi wa mfumo uliyo mkubwa, wenye uhandisi wa hali ya juu lakini changamano zaidi.". [12] Intanet ina tofauti nyingi mno, kwa mfano, kiwango cha kuhamisha data na sifa za kiumbo za uunganishaji vinatofautiana sana. Intanet inaonyesha "tukio ibuka" linalotegemea muundo wake mkubwa. Kwa mfano, takwimu za viwango vya kuhamisha data vinaonyesha kufananakwa muda. Kanuni za mbinu za uelekezaji na utoaji anwani kwa trafiki katika Intanet zinarejelea asili yake katika mwongo wa 1960 wakati ukubwa na umaarufu wa mtandao haukuweza kutarajiwa. Kwa hivyo, uwezekano wa kujenga miundo mbadalia unachunguzwa. [13]

Utawala

Makao makuu ya ICANN huko Marina Del Rey, California, Marekani

Internet ni mtandao uliyosambaa duniani ulioundwa na mitandao mingi tofauti iliyoshikanishwa. Hufanya kazi bila kitengo cha serikali kuu. Hata hivyo, ili kudumisha uwezo wa mifumo tofauti kufanya kazi pamoja, nyanja zote za kifundi na sera ya msingi wa miundombinu na nafasi za jina kuu husimamiwa na Shirika la Intanet linalotoa majina na nambari (ICANN), lililo na makao makuu huko Marina del Rey, California. ICANN ndiyo yenye mamlaka ya kusitiri utaratibu wa utoaji wa vitambulisho vya kipekee kwa matumizi ya Intanet, pamoja na majina ya vikundi, anwani za Itifaki ya Intanet (IP), nambari ya vipenyezo katika itifaki ya usafiri, na takwimu zingine nyingi. Nafasi ya iliyounganishwa ya majina ya ulimwengu, ambapo majina na nambari za kipekee hutolewa, ni muhimu kwa mataifa katika kupata huduma za Intanet. ICANN huongozwa na halmashauri ya wakurugenzi wa kimataifa wanaotolewa kutoka jamii za, ufundi wa Intanet, biashara, elimu, na mengine yasiyo ya kibiashara. Serikali ya Marekani inaendelea kuwa na jukumu la msingi katika kuidhinisha mabadiliko katika shina la DNslililoko katika kitovu cha mfumo wa eneo la majina. Jukumu la ICANN katika kuratibu zoezi la utoaji vitambulisho vya kipekee hulitofautisha kama shirika la kipekee lenye madaraka ya kuratibu Intanet ya kimataifa. Tarehe 16 Novemba 2005, Mkutano wa Dunia juu ya Jamii ya Habari, uliofanyika Tunis, uliunda Fora ya Utawala wa Intanet (IGF) kujadili masuala yanayohusiana na Intanet.

Matumizi ya kisasa

Intaneti inaruhusu mabadiliko makubwa katika masaa na maeneo ya kufanyia kazi, hasa kwa kuenea kwa viunganishi vya kasi visivyopimwa na zana za mtandao.

Intaneti kwa sasa yaweza kupatikana karibu popote kwa njia mbalimbali, hasa kupitita vifaa vinavyobebwa mkononi. Simu za mkononi, kadi za data, michezo ya video na vielekezaji vya mkononi vinaruhusu watumiaji kujiunganisha na intanet kutoka popote pale walipo na mtandao usiotumia waya unaoruhusu teknolojia ya kifaa hiki. Ndani ya mipaka inayowekwa na skrini ndogo vifaa vingine pungufu kama vifaa vya mfukoni, huduma za Intanet, pamoja na barua pepe na mtandao, huweza kupatikana. Watoa huduma za Intanet huweza kuzuia huduma zinazotolewa na malipo ya usafirishaji wa data bila kutumia nyaya yaweza kuwa ya juu zaidi kuliko mbinu zingine za kupata intanet.

Intaneti pia imekuwa soko kubwa kwa makampuni; baadhi ya makampuni makubwa leo yamekua kwa kuchukua faida ya gharama nafuu ya matangazo na biasharakwa kupitia Intanet, pia inajulikana kama biashara kupitia intaneti (e-commerce). Ni njia ya haraka sana katika kueneza habari kwa idadi kubwa ya watu kwa ujumla. Intaneti pia imebadilisha ununuzi - kwa mfano, mtu anaweza kuagiza CD kupitia intaneti na kuipokea katika barua baada ya siku kadhaa, au kuitoa kwa mtandao moja kwa moja katika baadhi ya kesi. Intaneti pia imewezesha uuzaji wa kibinafsi ambao unaruhusu kampuni kuuza bidhaa kwa mtu fulani au kundi maalum la watu, zaidi ya njia zingine za matangazo. Mifano ya uuzaji binafsi hujumuisha jamii zilizo katika Intanet kama vile MySpace, Friendster, Orkut, Facebook, na nyingine yznye maelfu ya watumizi wa Intanet ambao hujiunga kujitangaza wenyewe na kufanya urafiki kupitia Intanet. Wengi wa watumiaji hawa ni vijana na waliobaleghe wenye kati ya miaka 13-25. Kwa upande mwingine, wakati wanapojitangaza wao wenyewe hao pia hutangaza maslahi na mazoea yao, ambayo makampuni ya uuzaji katika Intanet yanaweza kutumia kama habari ili kujua kile ambacho watumiaji hawa watanunua kupitia Intanet, na kutangaza bidhaa za makampuni kwa watumiaji hao.

Gharama ya chini na ubadilishanaji wa haraka wa mawazo, maarifa, na ujuzi vimefanya kazi shirikishi kuwa rahisi sana, kwa msaada wa programu shirikishi. Makundi hayawezi tu kuwasiliana kwa bei ya chini, bali upana wa Intanet unaruhusu makundi kama hayo kujiunda kwa urahisi. Mfano wa makundi hayo ni harakati ya programu za bure, ambazo zimetengeneza, miongoni mwa programu nyingine, Linux, Mozilla Firefox, na OpenOffice.org. "Kuongea" kupitia intaneti, iwe katika fomu ya vyumba vya kuongea vya IRC, au kupitia mfumo wa ujumbe wa moja kwa moja , kunaruhusu mfanyikazi na wenzake kuwasiliana kwa njia rahisi sana wakati wanapofanya kazi katika kompyuta zao wakati wa mchana. Ujumbe unaweza kubadilishwa kwa njia ya haraka na inayofaa zaidi kuliko barua pepe. Maongezo katika mifumo hii huweza kuruhusu ubadilishanaji wa faili, michoro ya "ubao mweupe" au mawasiliano ya sauti na video kati ya wanachama wa timu moja.

Mifumo ya kudhibiti toleo unaruhusu timu zinazoshirikiana kufanya kazi kwa seti za hati zenye umiliki mmoja, bila ajali ya kufuta kazi za timu nyingine au wanachama kusubiri hadi kupata hati "zilizotumwa" ili kuweza kutoa michango yao. Biashara na timu za miradi zinaweza kushirikiana katika kalenda vilevile nyaraka na taarifa nyingine. Ushirika kama huo hutokea katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na utafiti wa kisayansi, maendeleo ya programu, kupanga mikutano , wanaharakati wa kisiasa na uandishi wa bunifu. Ushirikiano wa kijamii na kisiasa pia unaenea wakati upatikanaji wa Intanet na idadi ya watu waliosoma kompyuta inapoongezeka. Kutoka 'matukio' ya makundi yanayoundwa haraka na watu mwanzo wa miaka ya 2000 na matumizi ya mitandao ya kijamii katika maandamano ya uchaguzi wa 2009 huko Iran, Intanet inaruhusu watu kufanya kazi pamoja kwa ufanisi zaidi na kwa njia nyingi zaidi kuliko iwezekanavyo bila Intanet.

Intanet inaruhusu watumiaji wa kompyuta kufikia kompyuta zingine, na habari huhifadhiwa kwa urahisi, popote walipo duniani. Wanaweza kufanya hivi pamoja na, au, bila matumizi ya usalama, kujitambulisha na teknolojia za kuficha, kutegemea na mahitaji yao. Hii inahimiza njia mpya ya kufanya kazi kutoka nyumbani, kushirikiana na kubadilishana habari katika viwanda vingi. Mhasibu aliyeketi nyumbani anaweza kukagua vitabu vya kampuni iliyo katika nchi nyingine, kupitia kitumishi kilicho katika nchi nyingine ya tatu, ambayo inahifadhiwa na wataalamu wa IT katika nchi ya nne. Akaunti hizi zinaweza kuwa ziliundwa na waweka vitabu wafanyao kazi nyumbani, katika maeneo mengine, kwa kuzingatia habari-e waliyopata kupitia barua pepe waliyotumiwa kutoka ofisi za duniani kote. Baadhi ya mambo haya yalikuwa yanawezekana kabla ya kuenea kwa matumizi ya Intanet, lakini gharama ya laini binafsi ya kukodisha ingefanya mamboo hayo yasiweze kufanyika. Mfanyakazi wa ofisi akiwa mbali na dawati lake, labda upande mwingine wa ulimwengu katika safari ya kibiahsara au likizo, anaweza kufungua kikao katika kompyuta yake binafsi iliyoko ofisini mwake kwa kupitia mtandao binafsi wenye usalama (VPN) kwa kupitia Intanet. Hii inampa mfanyakazi upatikanaji kamili wa faili zake zote za kawaida na data, pamoja na barua pepe na zana nyingine za matumizi , wakati akiwa mbali na ofisi. Dhana hii pia inajulikana na baadhi ya watu wa usalama wa mitandao kama mtandao binafsi wa kidhahania wenye ndoto za kutisha, kwa sababu inapeleka mzunguko salama wa mtandao wa shirika ndani ya nyumba za wafanyakazi wa shirika hilo.

Huduma

Habari

Watu wengi hutumia maneno Intaneti na mtandao wa ulimwengu mzima (au Web tu ) kama visawe, lakini, kama tulivyojadiliana awali, maneno haya mawili yana maana tofauti. Mtandao wa Dunia Nzima ni seti ya nyaraka, picha na rasilimali nyingine, zinazotazamwa na kushikanishwa na kitafuta rasilimali sawa (URL) na viungo. URL hizi huruhusu watumiaji kuvipatia anwani vijakazi vya mtandao na vifaa vingine vinavyohifadhi rasilimali hizi na kuvipata vinapohitajika kwa kutumia HyperText Transfer itifaki ya kupelekea hati (HTTP). HTTP ni itifaki ya kipekee ya mawasiliano inayotumika katika mtandao wa Intanet. Huduma za mtandao huweza pia kutumia HTTP kuruhusu mifumo ya programu kuwasiliana ili kuweza kushiriki na kubadilishana mantiki ya biashara na data.

Bidhaa za programu zinazoweza kupata rasilimali za Mtandao mara nyingi huitwa ajenti wa matumizi. Katika matumizi ya kawaida, tovuti za mtandao, kama Internet Explorer, Firefox, Opera, Apple Safari, na Google Chrome, huwaruhusu watumiaji kuvuka kutoka kurasa ya mtandao mmoja hadi nyingine kupitia viungo vya hyper. Hati kwenye mtandao huweza kuwa na mchanganyiko wowote wa data ya kompyuta, zikiwemo, picha, sauti, maandishi, video, mchanganyiko wa picha na sauti na mambo yanayomhusisha mtumiaji wa Intanet kama michezo, zana ofisi na maonyesho ya kisayansi. Kupitia utafiti wa Intanet unaoendeshwa na maneno maalum kwa kutumia mitambo ya utafutaji kama Yahoo! na Google, watumiaji duniani kote huweza kupata habari nyingi, kwa urahisi na moja kwa moja kutoka kwa Intanet. Ikilinganishwa na kamusi elezi zilizochapishwa namaktaba za kawaida, Mtandao wa Dunia Nzima umewezesha kusambaa ghafla kwa habari na data.

Kwa kutumia mtandao, pia ni rahisi kuliko awali kwa watu binafsi na mashirika kuchapisha mawazo na habari kwa watazamaji wengi wanaotarajiwa. Kuchapisha kurasa ya mtandao, kibadilishanaji maoni - blogu, au kujenga tovuti inahusisha gharama ndogo za awali na huleta kupatikana kwa huduma nyingi zisizo na gharama. Kuchapisha na kudumisha idadi kubwa ya, mitandao ya kitaalamu yenye kuvutia, habari tofauti na ya moja kwa moja bado ni swala gumu na ghali, hata hivyo. Watu wengi na baadhi ya makampuni na vikundi-vitumizi hutumia mitandao ya ubadilishanaji maoni au blogu ambayo hutumika kama jarida zenye urahisi wakati wa kuongeza habari. Baadhi ya mashirika ya kibiashara huwahimiza wafanyakazi kuwasilisha ushauri katika maeneo yao maalum katika matumaini ya kuwa wageni watafurahishwa na maarifa ya mtaalam na habari za bure, na kuvutiwa kwa shirika hilo kama matokeo. Mfano mmoja wa zoezi hili ni Microsoft, ambayo watengenezaji bidhaa zake huchapisha mitandao ya ubadilishanaji binafsi katika blogu ili kuvutia umma kwa kazi zao. Mikusanyo ya kurasa binafsi za mtandao zilizochapishwa na watoa huduma wakubwa hubakia maarufu, na imeendelea kuwa ya kipekee. Ingawa oparesheni kama vile Angelfire na GeoCities zimekuwepo tangu siku za mwanzo wa Tovuti, oparesheni mpya, kwa mfano, Tovuti Facebook na MySpace kwa sasa vina wafuasi wengi. Oparesheni hizi mara nyingi hujionyesha kama mtandao ya huduma za kijamii kuliko viwekaji vya kurasa za mtandao.

Kuweka matangazo katika kurasa za tovuti pendwa huwa na faida, biashara-e (biashara ya mtandao)(e-commerce) au uuzaji wa bidhaa na huduma moja kwa moja kupitia tovuti inaendelea kukua. Katika siku za mwanzo, kurasa za mtandao kwa kawaida zilitengenezwa kama seti za faili za nakala kamilifu na zilizo peke za HTML zikihifadhiwa kwenye tovuti ya huduma. Hivi karibuni, tovuti hutengenezwa kwa kutumia kisimamizi cha yaliyomo au kifaa ororo cha wiki, ambacho huwa na maudhui machache sana mwanzoni. Wachangiaji wa mifumo hii, ambao wanaweza kuwa wafanyakazi wanaolipwa, wanachama wa klabu au shirika zingine au wanachama wa umma, hujaza vihifadhi-data na maudhui kutumia kurasa zilizoundwa kwa kusudi hilo, ilhali wageni huangalia na kusoma yaliyomo katika ombo lake la mwisho la HTML. Kuna uwezekano wa kuwa au kutokuwa na mifumo ya uhariri, kibali na mifumo ya usalama iliyojengwa katika mchakato wa kuchukua maudhui mpya iliyoingizwa na kuifanya ipatikane na wageni wanaolengwa.

Mawasiliano

Barua pepe ni huduma muhimu ya mawasiliano inayopatikana kwenye Intanet. Dhana ya kutuma ujumbe wa kielektroniki wa maandishi kati ya wahusika kwa njia iliyosawa na kutuma barua au memo ilitangulia utengenezaji wa Intanet. Leo inaweza kuwa muhimu kutofautisha kati ya Intanet na mifumo ya kindani ya barua pepe. Barua pepe ya Intanet inaweza kusafiri na kuhifadhiwa kimaandishi katika mitandao mingine mingi na mashine zilizo nje ya udhibiti wa mtumaji na mpokeaji. Kwa wakati huu kunauwezekano wa yaliyomo kusomwa na kubadilishwa na mhusika wa tatu, ikiwa kuna mtu yeyote anayefikiri kuwa una umuhimu wa kutosha. Mifumo ya barua za kindani, ambapo habari haipaswi kamwe kutoka nje ya mtandao wa kampuni au shirika , ni salama zaidi, ingawa katika shirika lolote kutakuwa na wafanyikazi wa IT na wafanyakazi wengine ambao kazi yao inahusu ufuatiliaji, na mara chache kufikia, barua pepe za wafanyikazi wengine ambazo hawajatumiwa hao. Picha, nyaraka na faili nyingine zinaweza kutumwa kama viungo vya barua pepe. Barua pepe zinaweza kutumwa kwa anwani nyingi za barua pepe.

Telefoni ya intaneti ni huduma nyingine la mawasiliano ya kawaida iliyowezekana kwa uundaji wa a Intanet. VoIP husimamia itifaki ya kupitisha sauti kupitia Intanet, ikirejelea itifaki msingi ya mawasiliano ya Intanet. Wazo hili lilianza mwanzo wa mwongo wa 1990 na zana zilizofanana na simu za polisi za kompyuta binafsi. Katika miaka ya hivi karibuni mifumo mingi ya VoIP imekuwa rahisi kutumia na kuwa na manufaa kama simu ya kawaida. Faida ni kwamba, Intanet inapobeba trafiki ya sauti, VoIP inaweza kuwa bure au kuwa na gharama ndogo sana kuliko upigaji simu wa jadi, hasa juu ya umbali mrefu na hasa kwa wale wenye viunganishi vinanvyowaka wakati wowote kama vile Cable au ADSL. VoIP inapevuka na kujitokeza kama mshindani mbadalia wa huduma za simu za jadi. Uwezo wa kubadilishana ujumbe kati ya watoa huduma mbalimbali imeboreshwa na uwezo wa kupiga au kupokea simu kutoka kwa simu ya jadi unapatikana. Vibadilisha mtandao vya VoIP ambavyo ni rahisi na vya bei nafuu vinapatikana na vinaondoa haja ya kuwa na kompyuta binafsi.

Ubora wa sauti unatofautiana kutoka wito moja hadi mwingine lakini mara nyingi ni sawa, na huweza hata kuzidi ule wa simu za jadi. Matatizo yaliyobakia kwa VoIP hujumuisha upigaji simu kwa nambari ya dharura na utumainikaji. Hivi sasa, watoa VoIP wachache hutoa huduma ya dharura, lakini haipatikani na wote. Simu za jadi huwezeshwa na nguvu za laini na hufanya kazi wakati stima zinapopotea; VoIP haifanyi hivyo bila chanzo kingine cha nguvu kwa vifaa vya simu na vifaa vya upatikanaji wa Intanet. VoIP pia imekuwa maarufu kwa zana za michezo , kama njia ya mawasiliano kati ya wachezaji. Wateja wa VoIP wanaojulikana katika michezo ni kama vile Ventrilo na Teamspeak. Wii, PlayStation 3, na Xbox 360 pia hutoa sifa za VoIP za kuongea kupitia mtandao .

Kuhamisha data

Kugawana failini mfano wa uhamishaji wa kiasi kikubwa cha data kupitia Intanet. Faili ya kompyuta inaweza kutumwa kwa kutumia barua pepe kwa wateja, waenzi na marafiki kama kiungo. Inaweza kuwekwa kwenye tovuti au tumishi ya FTP kwa upakuaji rahisi na watu wengine. Inaweza kuweka ndani ya "eneo lenye wamiliki wengi" au ndani ya tumishi ya failikwa ajili ya matumizi ya haraka na washikadau. Mzigo wa upakuaji mzito kwa watumiaji wengi unaweza kupunguzwa na matumizi ya "vioo" vya huduma au mitandao ya viwango aina moja. Katika hali hizi zote, upatikanaji wa faili unaweza kudhibitiwa na kujitambulisha kwa watumiaji, usafiri wa faili katika ya Intanet unaweza kuborongwa kwa kupewa maana fiche, na hongo ya pesa yaweza kutumiwa ili kuzipata faili. Bei inaweza kulipwa kutoka eneo tofauti kwa njia isiyokuwa wazi, kwa mfano, kutoka kwa kadi ya deni(krediti) ambayo maelezo yake hupitishwa pia - kwa kawaida hupewa maana fiche kabisa- kupitia Intanet. Asili na dhibitisho la faili iliyopokewa inaweza kuangaliwa kupitia saini za dijitali au kwa MD5 au aina nyingine ya ujumbe. Sifa hizi rahisi za intanet, juu ya msingi wa dunia nzima, zinabadilisha uzalishaji, mauzo, na usambazaji wa kitu chochote ambacho kinaweza kupunguzwa na kuwa faili ya kompyuta kwa usafirishaji. Hii ni pamoja na kila namna ya machapisho ya magazeti , bidhaa za programu, habari, muziki , filamu, video, picha, grafiki na sanaa zingine. Hili kwa upande mwingine limesababisha mabadiliko katika kila moja ya viwanda ambavyo awali vilidhibiti uzalishaji na usambazaji wa bidhaa hizi.

Utabakishaji wa vyombo vya habari unahusu kitendo ambacho watangazaji wengi wa redio na televisheni wanatumia kukuza lishe ya Intanet ya habari za moja kwa moja kutumia sauti, na tabaka za video (kwa mfano, BBC). Wanaweza pia kuruhusu maonyesho na usikilizaji kulingana na mabadiliko ya wakati kama kuangalia mbele, picha klasiki na sifa za kusikiliza tena. Watoaji huduma hawa wameungwa na anuwai ya "watangazaji" halisi wa Intanet ambao kamwe hawakuwa na leseni za kutoa habari moja kwa moja. Hii ina maanaisha kuwa kifaa kilichounganishwa na intanet, kama vile kompyuta au kitu kingine maalum, kinaweza kutumika kupata vyombo vya habari vilivyounganishwa na Intanet kwa njia ile ile kama ilivyowezekana tu na mpokezi wa televisheni au redio. Aina ya matini ni pana sana, kutoka kwa ponografia hadi tovuti za ufundi na utaaluma wa juu. Podcasting ni aina fulani katika mada hii, ambapo - kwa kawaida ni sauti- matini zinapakuliwa na kuchezwa tena kwenye kompyuta au kubadilishwa kwenye chombo cha habari kinachobebeka ili kisikilizwe matu anapotembea. Hizi mbinu za kutumia vifaa rahisi vinaruhusu mtu yeyote, aliye na udhibiti ufichaji au udhibiti wa leseni, kutangaza picha , muziki na video kote ulimwenguni.

Kamera za mtandao zinaweza kuonekana kama ongezeko ya chini ya bajeti ya jambo hili. Ingawa baadhi ya kamera za mtandao zinaweza kutoa video za kiima kizima, picha huwa ndogo au hujiongeza pole pole. Watumiaji wa intanet wanaweza kuangalia wanyama waliyozunguka kidimbwi cha maji huku Afrika, meli katika kipisho cha Panama, trafiki katika mzunguko wa barabara za mtaa au kufuatilia wanapoishi katika muda halisi. Vyumba vya kuongea vya video na mikutano ya video pia ni maarufu, matumizi mengi yakipatikana ya kamera kibinafsi za mtandao, zilizo na, au zisizo na sauti inayotamba pande zote mbili. YouTube ilianzishwa tarehe 15 Februari 2005 na sasa ni tovuti inayoongoza kwa maonyesho ya video za bure pamoja na idadi kubwa ya watumiaji. Inatumia mtandao wenye msingi wa kichezaji cha flashi kuonyesha faili za video. Watumiaji waliojiandikisha huweza kuongeza idadi isiyo na kipimo ya video na kutengeneza vitambulishi vyao binafsi. YouTube inadai kuwa watumiaji wake hutazama mamia ya mamilioni, na huongeza mamia ya maelfu, ya video kila siku. [14]

Upatikanaji

Lugha ya iliyoenea katika mawasiliano ya Intanet ni Kiingereza. Hii inayotumika zaidi katika intaneti ni Kiingereza. Hili latokana na kuwa ndiyo lugha asilia ya intanet na pia nafasi yake kama lingu-franca = lugha sambazi. Pia inaweza kuhusiana na upungufu wa utendaji wa kompyuta za awali, kiasi kikubwa zikitoka Marekani, kushughulikia maandishi mengine kuliko yale ya lahaja ya Kiingereza ya alfabeti ya Kilatin. Baada ya Kiingereza (asilimia 29 ya wageni wa Tovuti) lugha zilizohitajika zaidi katika Tovuti ya Dunia Nzima ni Kichina (asilimia 22), Kihispania (asilimia 8), Kijapani (asilimia 6), Kifaransa (asilimia 5), Kireno na Kijerumani (kila moja asilimia 4 ), Kiarabu (asilimia 3) na Kirusi na Kikorea (kila moja asilimia 2 ). [15] Katika kanda, asilimia 42 ya watumiaji wa intaneti duniani wana makao Barahindi, asilimia 24 Ulaya, asilimia 15 Amerika ya Kaskazini, asilimia 11 Amerika Kusini na Caribbean zikichukuliwa kwa pamoja, asilimia 4 Afrika, asilimia 3 Mashariki ya Kati na asilimia 1 Australia / Oceania. [16] Teknolojia za Intanet zimeendelea ya kutosha katika miaka ya hivi karibuni, hasa katika matumizi ya Unicode, kwamba vifaa vizuri vinapatikana kwa maendeleo na mawasiliano katika lugha zinazotumiwa kwa wingi. Hata hivyo, baadhi ya matatizo kama mojibake (uonyeshaji usiosahihi wa maandishi ya lugha za kigeni , pia inajulikana kama kryakozyabry) bado hubakia.

Njia za kawaida za kupata Intaneti nyumbani ni kwa kupiga, laini za broadband (kupitia waya za koax, nyuzinyuzi za optiki au waya za shaba), Wi-Fi, setilaiti na teknolojia ya rununu ya 3G. Maeneo ya umma kwa matumizi ya Intaneti ni maktaba na mikahawa ya Intaneti, ambamo kompyuta zilizounganishwa na Intaneti hupatikana. Pia kuna sehemu za kupata Intaneti katika maeneo mengi ya umma kama vile kumbi za uwanja wa ndege na maduka ya kahawa, katika baadhi ya sehemu hizi kwa matumizi mafupi wakati umesimama. Maneno mbalimbali hutumiwa kama vile "kiosk za umma za interneti", "pahala pa upatikanaji intaneti pa umma", na "simu za kulipia za Mtandao". Hoteli nyingi sasa pia huwa na pahala pa umma, ingawa hizi hulipiwa kulingana na matumizi. Sehemu hizi hutumika kwa matumizi mbalimbali kama ununuzi tiketi , amana za benki, malipo kupitia mtandao nk. Wi-Fi hutoa upatikanaji usiotumia waya wa mitandao ya kompyuta, na kwa hiyo yaweza kufanya hivyo kwa Intanet yenyewe. Sehemu moto zinazotoa upatikanaji kama huo hujumuisha mikahawa ya Wi-Fi, ambapo watumiaji hupaswa kuleta vifaa vyao visivyotumia waya kufikia Intaneti kama vile Kompyuta za pajani au PDA. Huduma hizi huweza kuwa bure kwa wote, bure kwa wateja tu, au waliolipishwa. Eneo moto halina haja ya kuwa finyu katika eneo ndogo. Kampasi nzima au bustani, au hata mji mzima unaweza kuwezeshwa. Juhudi za mashinani zimesababishamitandao ya kijamii isiyotumia waya. Huduma za Wi-Fi za kibiahsara zinazofunika maeneo ya miji mikubwa zinapatikana London, Vienna, Toronto, San Francisco, Philadelphia, Chicago na Pittsburgh. Intanet huweza kupatikana kutoka sehemu hizo kama kiti cha bustani.[17] Mbali na Wi-Fi, kumekuwa na majaribio na mitandao ya simu ya kibiashara isiyotumia waya kama Ricochet, huduma mbalimbali za kasi za data kupitia mitandao ya simu za mkononi na, huduma zisizotumia waya zisizobadilika. Simu za mkononi za hali ya juu kama vile smartphone kwa ujumla huja na upatikanaji wa Intaneti kwa kupitia mtandao wa simu. Vivinjari cha mitandao kama vile Opera hupatikana katika simu hizi za mkononi zilizoendelea, ambazo pia huweza kutekeleza aina nyingie tofauti ya programu za Intaneti. Simu nyingi za mkononi huweza kupata Intanet kuliko PC ingawa hii haitumiki kwa upana. Kinachotoa huduma za upatikanaji wa Intaneti na muundo wa mfanyiko wa itifaki hutofautisha mbinu zinazotumika kupata Intaneti.

Taathira za kijamii

Intaneti imefanya kuwe na uwezekano mkubwa kabisa wa aina mpya za mahusiano ya kijamii, shughuli na upangaji, kutokana na sifa zake msingi kama vile kuenea katika matumizi na upatikanaji. Tovuti za kijamii kama vile Facebook na MySpace vimetengeneza aina mpya ya ufahamianaji na mwingiliano. Watumiaji wa tovuti hizi huweza kuongeza vitu mbalimbali kwa kurasa zao binafsi, kuonyesha maslahi yao ya kawaida, na kuungana na watu wengine. Inawezekana kupata mzunguko mkubwa wa marafiki, hasa kama tovuti inaruhusu watumiaji kutumia majina yao halisi, na kuruhusu mawasiliano kati ya makundi makubwa ya watu waliomo. Tovuti kama meetup.com zipo ili kuruhusu matangazo mapana ya makundi ambayo yanaweza kuwepo hasa kwa mikutano ya ana-kwa-ana, lakini ambayo inaweza kuwa na mahusiano mbalimbali madogo katika tovuti ya kundi lao katika meetup.org, au tovuti zingine zenye kufanana.

Kizazi cha kwanza kwa sasa kinakuzwa na upatikanaji ulioenea wa kujiunga na Intaneti, unaosababisha utovu wa faragha, utambulisho, na wasiwasi wa kimiliki. "Wenyeji wa dijitali" hukumbwa na wasiwasi tofauti ambao haukuwa na vizazi vya mwanzoni.

Katika jamii za kidemokrasia, mtandao umepata uhusiano mpya kama chombo cha kisiasa, kupelekea udhibiti wa Intaneti na baadhi ya nchi. Kampeni ya urais wa Howard Dean mwaka 2004 huko Marekani ulikuwa mashuhuri kwa uwezo wake wa kutoa michango kupitia Intaneti. Makundi mengi ya kisiasa hutumia interneti ili kufanikisha utaratibu mpya wa kujiandaa , ili kutimiza wanaharakati wa Intaneti. Baadhi ya serikali, kama zile za Iran, Korea ya Kaskazini, Myanmar, Jamhuri ya Watu wa China, na Saudi Arabia, zinaudhibiti wa juu wa yale watu katika nchi zao wanayoweza kupata kwenye Intanet, hasa maudhui ya kisiasa na kidini. Hii inakamilishwa kwa kupitia programu inayoficha makundi na maudhui ili yasipatikane kwa urahisi bila mbinu ya kitaaluma zaidi.

Nchini Norway, Denmark, Finland [18] na Uswidi, watoa huduma za Intaneti kwa hiari yao(pengine kuepuka mpangilio kama huo kuwa sheria) walikubali kudhibiti upatikanaji wa tovuti zilizotajwa na polisi. Ingawa orodha hii ya URL haramu inapaswa kuwa na anwani za tovuti zinazojulikana zenye kuonyesha ponografia ya watoto, yaliyomo katika orodha hii ni siri. Nchi nyingi, ikiwemo Marekani, zimepitisha sheria zinazofanya umiliki au usambazaji wa nyenzo fulani, kama vile ponografia ya watoto, iliyoharamu, lakini hazitumii programu ya kuficha. Kuna programu nyingi za bure na zinazouzwa ziitwayo, programu za udhibiti wa maudhui, na ambazo mtumiaji anaweza kuchagua kuzuia tovuti zinazokera katika kompyuta binafsi au mitandao, kama kuzuia uwezekano wa mtoto kupata habari za kimapenzi au vurugu.

Intaneti imekuwa chanzo kikuu cha burudani tangu kabla ya mtandao wa dunia nzima, kukiwa na majaribio ya kijamii yanayofurahisha kama vile MUD na MOOyaliyofanywa katika vitoa nhuduma vya vyuo vikuu, ambapo makundi ya Usenetya vichekesho yalipokea kiasi kikubwa cha trafiki kuu. Leo, majukwaa mengi ya Intaneti yana sehemu ya michezo na video za kuchekesha; katuni(vibonzo) fupi katika mfano wa sinema za flashi pia ni maarufu. Zaidi ya watu milioni 6 hutumia vibadilishanaji maoni (blogu) au mbao za ujumbe kama njia ya mawasiliano na kwa ajili ya kubadilishana mawazo. Viwanda vya sinema za watu wazima na kamari vimechukua faida kamili ya mtandao wa dunia nzima, na mara nyingi hutoa chanzo muhimu ya mapato ya matangazo kwa tovuti zingine. Ingawa serikali nyingi zimejaribu kuweka vikwazo katika matumizi ya Intaneti katika viwanda hivi, zilishindwa kupunguza kuenea umaarufu wa viwanda hivi.

Eneo moja kuu la burudani kwenye interneti ni Michezo yenye wahusika wengi. Aina hii ya burudani inajenga jamii, kuwaleta watu wa umri fofauti na asili zote kufurahia mwendo wa kasi wa ulimwengu wa michezo ya wahusika wengi. Hii inaanza kutoka MMORPG hadi mfyatua risasi wa kwanza , kutoka michezo ya kusawiri mhusika hadi kamari ya Intaneti. Hii imebadilisha njia ambayo watu wengi huweza kuingiliana na jinsi wao wanvyoweza kutumia muda wao wa bure katika Interneti. Wakati michezo ya Intaneti imekuwapo tangu mwongo wa 1970, aina ya kisasa ya michezo ya Intaneti ilianza na huduma kama GameSpy na MPlayer, ambayo wachezaji wa michezo kwa kawaida walijiunga nayo. Wasiyojiunga walikubaliwa kucheza baadhi ya aina za mchezo iliyochezwa au baadhi ya michezo. Wengi hutumia Intaneti kwa kupata na kuchukua muziki, sinema na vitu vingine kwa starehe zao na utulivu. Kama ilivyojadiliwa hapo awali, kuna vyanzo za kulipia na vya bure kwa haya yote, kwa kutumia vitoa huduma vikuu na teknolojia za viwango vinavyolingana. Baadhi ya vyanzo hivi hujali zaidi haki za wasanii wa awali na juu ya sheria za kimiliki kuliko wengine.

Wengi hutumia mtandao wa dunia nzima kupata habari, taarifa za michezo na hali ya hewa na, kupanga likizo na kujua zaidi kuhusu mawazo na maslahi yao. Watu hutumia maongezi kupitia mtandao, utumaji wa ujumbe na barua pepe kuwasiliana na marafiki duniani kote, wakati mwingine kwa njia sawa na jinsi baadhi ya watu awali walivyokuwa na marafiki ambao walifahamiana kwa barua tu. Mitandao ya kijamii kama MySpace, Facebook na mingineo, pia huwasaidia watu kuwasiliana kwa starehe zao. Intaneti imeshuhudia kuongezeka kwa idadi ya kopyuta binafsi za mtandao, ambapo watumiaji wanaweza kupata faili zao, folda, na masharti kupitia Intaneti. Matumizi ya Intaneti yamesababisha upungufu mkubwa kwenye rasilimali ya kampuni; mfanyikazi wastani wa Uingereza hutumia dakika 57 kwa siku akipitia mtandao wa dunia nzima wakati akifanyakazi, kulingana na utafiti wa mwaka wa 2003 uliofanywa na Huduma za Kibiashara za Peninsula. [19]

Hatari za Intaneti

Wavuti wa Webmd umesema kuwa mtu aliyepatwa na ashiki ya kuwa kwa mitandao kila wakati (addicted) huenda akawa na maswala mengine ya kiafya kwa ubongo (mental health issues).

Wavuti pia umefanya watu wawe na uchu wa kuangalia filamu za ponografia kwa sababu hili hufanyika kwa urahisi.

Vijana wengi pia wamejipata kwa hatari baada ya jumbe katika vyombo vya habari vya kijamii (social media) baada ya kutapeliwa au hata kutekwa nyara na watu waliojifanya marafiki.

Kumekuwa pia na michezo mibaya iliyowafanya vijana kujiua kama vile Blue Whale challenge ambapo wachezaji walikuwa wakishawishiwa wajitoe uhai baada ya kushiriki katika mchezo.

Kumekuwa pia na michezo ya kamari (online betting) ambapo watu wapoteza pesa na hata kugeukia kuwa wezi ili waweze kuendelea kucheza michezo ile.

Jinsi ya kudhibiti intaneti kama mzazi

Wazazi wana jukumu la kuhakikisha kuwa wanao hawaingii katika wavuti baya za ponografia, ugaidi, zinazofunza itikadi kali au zinazohimiza au kuwashawishi watoto kushiriki katika tabia mbovu. Wanaweza kufanya hivi kwa kuweka "rotating proxies" ambazo hudhibiti kinachoonwa kwa wavuti ile. Pia wanafaa waongee na watoto na kuwaambia madhara ya mitandao.

Kama una uraibu wa Intaneti, inafaa uchukue likizo usitumie mitandao ili uweze kuongea na watu moja kwa moja.

Tazama pia

Tanbihi

 1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-01-16. Iliwekwa mnamo 2021-04-23.
 2. "Links". HTML 4.01 Specification. World Wide Web Consortium. HTML 4.01 Specification. Iliwekwa mnamo 2008-08-13. [T]he link (or hyperlink, or Web link) [is] the basic hypertext construct. A link is a connection from one Web resource to another. Although a simple concept, the link has been one of the primary forces driving the success of the Web. {{cite web}}: Check date values in: |date= (help)
 3. "ARPA/DARPA". Defense Advanced Research Projects Agency. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-04-07. Iliwekwa mnamo 2007-05-21.
 4. "DARPA Over the Years". Defense Advanced Research Projects Agency. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-04-07. Iliwekwa mnamo 2007-05-21.
 5. Baran, Paul (1964). On Distributed Communications.
 6. Coffman, K. G; Odlyzko, A. M. (1998-10-02). "The size and growth rate of the Internet" (PDF). AT&T Labs. Iliwekwa mnamo 2007-05-21. {{cite journal}}: Cite journal requires |journal= (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
 7. Comer, Douglas (2006). The Internet book. Prentice Hall. uk. 64. ISBN 0132335530.
 8. "World Internet Users and Population Stats". Internet World Stats. Miniwatts Marketing Group. 2009-06-30. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-06-23. Iliwekwa mnamo 2009-11-06.
 9. "IETF Home Page". Ietf.org. Iliwekwa mnamo 2009-06-20.
 10. Huston, Geoff. "IPv4 Address Report, daily generated". Iliwekwa mnamo 2009-05-20.
 11. "Notice of Internet Protocol version 4 (IPv4) Address Depletion" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2010-01-07. Iliwekwa mnamo 2009-08-07.
 12. Walter Willinger, Ramesh Govindan, Sugih Yamini, Vern Paxson, na Scott Shenker (2002). Scaling phenomena in the Internet, katika Proceedings of the National Academy of Sciences, uk.99, suppl. 1, 2573-2580
 13. "internet Makeover?Some Urge its time ". Gazetti la Seattle Times, tarehe 16 Aprili 2007.
 14. "YouTube Fact Sheet". YouTube, LLC. Iliwekwa mnamo 2009-01-20.
 15. internet World Stats, Archived 26 Aprili 2012 at the Wayback Machine. zilizichapishwa upya tarehe 30 Juni 2009
 16. World Internet Usage Statistics News and Population Stats Archived 23 Juni 2011 at the Wayback Machine. zilizoandikwa upya 30 Juni 2009
 17. "Toronto Hydro to Install Wireless Network in Downtown Toronto". Bloomberg.com. Ilichukuliwa tarehe 19-Mar-2006.
 18. "Finland censors anti-censorship site". The Register. 2008-02-18. Iliwekwa mnamo 2008-02-19.
 19. "Scotsman.com News - Net abuse hits small city firms". News.scotsman.com. Iliwekwa mnamo 2009-08-07.

Marejeo

 • Rehmeyer, Julie J. 2007. Mapping a medusa: Intaneti inasambaza mizizi yake Science News 171 (23 Juni) :387-388. Inapatikana http://www.sciencenews.org/articles/20070623/fob2.asp Archived 19 Aprili 2008 at the Wayback Machine..
 • Castells, M. 1996. Rise of the Network Society. 3 vols. Vol. 1. Cambridge, MA: Wachapishaji wa Blackwell .
 • Castells, M. (2001), “Lessons from the History of Internet”, in “The Internet Galaxy”, Ch. 1, ukurasa 9-35. Uchapishaji wa Chuo Kikuu cha Oxford.
 • RFC 1122, Requirements for Internet Hosts—Communication Layers, IETF, R. Braden (Ed.), Oktoba 1989
 • RFC 1123, Requirements for Internet Hosts—Application and Support, IETF, R. Braden (Ed.), Oktoba 1989

Viungo vya nje

Kwa Kiingereza