Vietnam Kusini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Ramani ya Vietnam Kusini
Wanajeshi wa Marekani katika Vietnam Kusini

Vietnam Kusini au Jamhuri ya Vietnam (Việt Nam Cộng Hòa) ilikuwa nchi katika nusu ya kusini ya Vietnam ya leo kati ya 1954 na 1976. Mji mkuu ulikuwa Saigon (leo: Mji wa Ho-Chi-Minh).

Uhuru wa koloni ya Kifaransa[hariri | hariri chanzo]

Koloni ya kifaransa ya Vietnam iligawiwa mwaka 1954 wakati wa kuondoka kwa Wafaransa. Katika kaskazini ya nchi wanamigambo Wakomunisti chini ya Ho Chi Minh waliwahi kuwafukuza Wafaransa katika vita ya Indochina. Wakimbizi wengi waliohofia Wakomunisti walikimbilia kusini.

Wafaransa waliwahi kuunda serikali ya kienyeji na kumkabidhi madaraka Kaisari Bao Dai kwa sehemu ya kusini walipobaki na uwezo. Mkutano wa Geneva juu ya Indochina ya 1954 uliomaliza vita uliamua ya kwamba serikali ya Bao Dai itawale kusini na kanda la eneo lisolo na jeshi ligawanye sehemu mbli za nchi.

Udikteta wa Diem[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa kundoka kwa Wafaransa Bao Dai alipinduliwa na waziri mkuu Ngô Đình Diệm. Diem alikataza uchaguzi kwa Vietnam wote uliopangwa kwa 1956. Akaendesha utawala kama rais vikali akawa dikteta. Mwenyewe alikuwa Mkatoliki akashindwa kujenga uhusiano na Wabuddha waliokuwa wakazi wengi. Farakano hili kati ya Wakristo na Wabuddha lilisaidia upanuzi wa Wakomunisti.

Vita ya Vietnam[hariri | hariri chanzo]

1963 Diem alipinduliwa na jeshi na nchi iliendelea chini ya kamati za kijeshi. Wakomunisti kutoka kaskazini walipeleka silaha kusini na kuanzisha maeneo waliotawala kwa umbo la chama cha Vietkong. Vita ya wenyewe kwa wenyewe ilipanua. Marekani ilijiunga katika vita hii kwanza kwa kutuma wanajeshi kama washauri na wasaidizi kwa jeshi la Vietnam Kusini na baadaye pia kwa vikosi vilivyoshiriki katika vita ya msituni dhidi ya wakomunisti wa Vietkong.

Kuingilia kwa Marekani[hariri | hariri chanzo]

Jeshi la Vietnam Kusini iliongozwa vibaya na viongozi wake walijushughulisha zaidi na ufisadi kuliko vita. Wanajeshi wa kawaida hawakuwa na hamu kuwafuata wakubwa ambao walijali pesa kuliko maisha ya watu wao. Hivyo Marekani ilichukua sehemu kubwa zaidi za mapigano na mwaka 1968 wanajeshi 543,000 Wamarekani walikuwepo Vietnam Kusini.

Huko Marekani watu wengi walianza kupinga mchango wa nchi yao katika vita hii na serikali ilianza kupunguza idadi ya wanajeshi wake ikijaribu kuimarisha jeshi la Vietnam Kusini.

Kwa jumla majarabio haya yalishindikana. Vietnam Kaskazini iliendelea kutuma wanajeshi wengi kupitia Laos na Mareakani ilishindwa kuwazuia.

Mwisho wa Vietnam Kusini[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1975 Vietkong pamoja na jeshi la Vietnam Kusini iliteka mji mkuu Saigon. Kwa mwaka moja serikaliy a kikomunisti ilitawala kusini na mwaka 1976 sehemu mbili za Vietnam ziliunganishwa.

Takriban milioni na nusu ya wakazi wa kusini walikimbia baada ya 1976 wakitumia maboti na mashua ya kila aina wakajaribu kuvuka bahari na kufikia nchi pasipo na ukomunisti. Wengi wao walikufa.