Vietnam Kaskazini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa Vietnam Kaskazini 1955-1976
Ramani ya Vietnam Kaskazini 1955-1976
Bendera ya Vietnam Kaskazini 1955-1976

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Vietnam au Vietnam Kaskazini (kwa Kivietnam: Việt Nam Dân Chủ Cộng Hòa) ilikuwa jina la dola kaskazini mwa Vietnam ya leo kati ya miaka 1946 na 1976.

Jamhuri hiyo ilitangazwa na Ho Chi Minh baada ya mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia tarehe 2 Septemba 1945 mjini Hanoi katika kaskazini ya koloni la Kifaransa ya Indochina. Tangazo lilijumlisha eneo la majimbo ya Tonking na Annan ya Indochina ya Kifaransa. Ho Chi Minh alikuwa kiongozi wa Chama cha Kikomunisti kilichotawala harakati ya Viet Minh iliyoendesha upiganaji dhidi ya Ufaransa.

Tangu mwaka 1946 Ufaransa iliyowahi kufukuzwa kutoka Vietnam na Wajapani wakati wa vita vikuu ilijaribu kurudisha utawala wake. Katika vita vya Indochina jeshi la kikoloni la Ufaransa lilishindwa mwaka 1954 na Mkutano wa Geneva juu ya Indochina ya 1954 uliligawa koloni la awali katika nchi za Laos, Kambodia na Vietnam. Vietnam iligawiwa sehemu mbili yaani Vietnam Kaskazini (rasmi: Jamhuri ya Kidemokrasia ya Vietnam) na Vietnam Kusini (rasmi: Jamhuri ya Vietnam). Mapatano ya amani yalitarajia kuwepo kwa uchaguzi wa kitaifa lakini serikali ya kusini ilikataa kura hiyo.

Hivyo Vietnam Kaskazini ilibaki kama nchi ya kikomunisti na Ho Chi Minh alikuwa rais wake.

Tangu mwaka 1960 uongozi wa Vietnam Kaskazini uliamua kujenga harakati ya Vietkong katika Vietnam Kusini kwa shabaha ya kupindua serikali ya Kusini na kuunganisha nchi yote. Hii ilisababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe ya kusini na kulazimisha kuingia kwa Marekani katika vita hivyo.

Kuanzia mwaka 1964 Vietnam Kaskazini ilituma wanajeshi wengi kwenda kusini waliofaulu kushinda vita na kuteka Saigon mwaka 1975 wakiunda serikali ya kikomunisti ya kusini. Mwaka 1976 sehemu zote mbili za Vietnam ziliunganishwa kwa jina la Jamhuri ya Kijamii ya Vietnam.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Vietnam Kaskazini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.