Hindu Kush

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Ramani ya Hindu Kush, ikionyesha mpito wa Dorah
Sehemu za milima

Hindu Kush ni safu ya milima ya kunjamano katika Asia ya Kati. Inaenea kuanzia Afghanistan upande wa magharibi hadi Pakistan na kuishia katika China na Tajikistan.

Mlima wa juu ni Tirich Mir wenye kimo cha mita 7,708.

Njia za kuvuka milima hiyo ziko kwenye mipito ya Mintaka, Kilik, Chilinji na Kuramber zikiunganisha Kashmir na nchi za Asia ya Kati.

Mito mingi pamoja na Chapursan, Ishkuman, Ghizar, Gilgit na Shandur hutoka kwenye mabonde ya Hindu Kush na mwishowe hujiunga na Mto Indus. Upande wa kaskazini maji ya Hindu Kush hutiririka kuingia katika mto Amu Darya. Kigezo:Mbeg-jio-Asia