Edinburgh

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Princes Street mjini Edinburgh

Edinburgh (Kigaeli: Dùn Èideann) ni mji mkuu pia mji mkubwa wa pili wa Uskoti mwenye wakazi 435,790 (2005). Mji uko kwenye pwani la mashariki wa Uskoti kwenye mdomo wa mto Forth baharini.

Boma la Edinburgh liko katikati ya mji kwenye kilima kikali.

Edinburgh imejulikana kote Ulaya kwa sababu ya sherehe yake ya maigizo inayofanyika kila mwaka na washiriki maelfu.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Boma lilianzishwa kabla ya karne ya 7 BK. Mji ulianza kukua kando la boma. Mwaka 1437 umekuwa mji mkuu wa Uskoti badala ya Perth. Ilikuwa pia mahali pa kukutana kwa bunge la Uskoti liliopata jengo lake la pekee mwaka 1639. Baada ya maungano ya Uingereza na Uskoti mwaka 1707 hapakuwa tena na serikali au bunge la pekee hadi 1999 mwaka wa kurudishwa bunge na serikaliya kijimbo kwa Uskoti. Edinburgh imekuwa tena mji mkuu wa angalau wa jimbo linalojitawala katika mambo ya ndani.

Picha za Edinburgh[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Europa Mapa.png Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Edinburgh kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Mji wa Edinburgh