Eire Kaskazini
Eire ya Kaskazini Tuaisceart Éireann (Kieire) Northern Ireland (en) | |
---|---|
Wimbo wa taifa: "God Save the King" (Ya kifalme) | |
Lugha rasmi | Kiingereza Kigaeli cha Eire |
• Mfalme | Charles III |
• Waziri Mkuu | Michelle O'Neill |
Historia | |
• Muungano na Uingereza | 1801 |
• Mgawanyiko wa Ireland | 1921 |
• Mkataba wa Ijumaa Kuu | 1998 |
Eneo | |
• Jumla | km2 14,330 |
• Maji (asilimia) | 7% |
• Ardhi | km² 13,181 |
• Msongamano | 135/km2 |
PLT (Kawaida) | Kadirio la 2022 |
• Jumla | ▲ £56.7 bilioni |
• Kwa kila mtu | ▲ $29,674 |
HDI (2021) | ▲ 0.887 juu sana |
Gini (2017) | 33.2 |
Sarafu | Pauni ya Uingereza (£) |
Majira ya saa | UTC+0 GMT / BST (UTC+1 katika majira ya joto) |
Upande wa magari | Kushoto |
Msimbo wa simu | +44 |
Jina la kikoa | .uk |
Eire Kaskazini (pia: Ayalandi ya Kaskazini; kwa Kiingereza: Northern Ireland; kwa Kieire: Tuaisceart Éireann) ni nchi mojawapo ya Ufalme wa Muungano, iliyoko kaskazini-mashariki mwa kisiwa cha Eire. Ikiwa na idadi ya watu takriban milioni 1.9, ni taifa dogo zaidi kwa idadi ya watu ndani ya Ufalme wa Muungano na ina eneo la takriban km² 14,130. Jiji lake kubwa na mji mkuu ni Belfast. Eire Kaskazini ilijitenga rasmi na Jamhuri ya Eire mnamo Mei 3, 1921, kufuatia mgawanyiko chini ya Sheria ya Serikali ya Eire ya 1920.
Ni kwamba baada ya Vita vya uhuru vya Eire bunge la London kwa sheria ya mwaka 1920 (Government of Ireland Act 1920) liligawa Ireland katika sehemu mbili za Northern Ireland na Southern Ireland.
Wabunge waliochaguliwa katika Ireland ya Kusini walijitangaza kuwa bunge la Eire na kwa mapatano ya mwaka 1922 uhuru wa Eire ulitambuliwa. Nchi mpya ilijiita tangu 1937 "Jamhuri ya Eire" na kuendelea kama nchi ya pekee. Mikoa ya Northern Ireland iliendelea kuwa sehemu za Ufalme wa Muungano.
Ndani yake, mwaka 1999 Uskoti, Welisi na Ireland ya Kaskazini zilirudishiwa mabunge yao ya pekee.
Kadiri ya sensa ya mwaka 2021, wakazi ni 1,903,100[1]. Wengi wao ni Wazungu (96.6%), wakifuatwa na Waafrika (0.6%), Wahindi (0.5%) na Wachina (0.5%).
Kiingereza ni lugha mama kwa asilimia 95.4 za wakazi.
Upande wa dini, wengi ni Wakristo (76.6%), hasa Wakatoliki (42.3%) na Waprotestanti wa madhehebu mbalimbali (37.3%). Wenye dini tofauti ni 1.3%, wakati 17.4% hawana dini yoyote au hawakujibu swali.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Simpson, Mark (24 May 2022). "Census: Northern Ireland population just under 2m". BBC News. Retrieved 22 September 2022.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Jonathan Bardon, A History of Ulster (Blackstaff Press, Belfast, 1992), ISBN|0-85640-476-4
- Brian E. Barton, The Government of Northern Ireland, 1920–1923 (Athol Books, 1980)
- Paul Bew, Peter Gibbon and Henry Patterson The State in Northern Ireland, 1921–72: Political Forces and Social Classes, Manchester (Manchester University Press, 1979)
- Tony Geraghty (2000). The Irish War. Johns Hopkins University Press. ISBN 978-0-8018-7117-7.
- Robert Kee, The Green Flag: A History of Irish Nationalism (Penguin, 1972–2000), ISBN|0-14-029165-2
- Osborne Morton, Marine Algae of Northern Ireland (Ulster Museum, Belfast, 1994), ISBN|0-900761-28-8
- Henry Patterson, Ireland Since 1939: The Persistence of Conflict (Penguin, 2006), ISBN|978-1-84488-104-8
- P. Hackney (ed.) Stewart's and Corry's Flora of the North-east of Ireland 3rd edn. (Institute of Irish Studies, Queen's University of Belfast, 1992), ISBN|0-85389-446-9 (HB)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Angalia mengine kuhusu Northern Ireland kwenye miradi mingine ya Wikimedia: | |
![]() |
Fafanuzi za Kiingereza kutoka Wiktionary |
![]() |
picha na media kutoka Commons |
![]() |
misaada ya kujisomea kwa Kiingereza kutoka Wikiversity |
![]() |
nukuu kutoka Wikiquote |
![]() |
matini za ushuhuda na vyanzo kutoka Wikisource |
![]() |
vitabu kutoka Wikibooks |
- Northern Ireland Executive (Northern Ireland devolved government)
- Discover Northern Ireland (Northern Ireland Tourist Board)
OpenStreetMap has geographic data related to: Eire Kaskazini Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Eire Kaskazini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.