Nenda kwa yaliyomo

Halmashauri ya Kiekumeni ya Makanisa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Halmashauri ya Kiekumeni ya Makanisa (kwa Kiingereza: World Council of Churches, kifupi WCC) ni muundo wa kimataifa unaokusudiwa kuunganisha madhehebu ya Ukristo. Ilianzishwa mwaka 1948.

Makao makuu yako Geneva, Switzerland.[1]

Halmashauri hiyo ni tunda la juhudi za ekumeni na kauli yake ya msingi ni kwamba: "Halmashauri ya Kiekumeni ya Makanisa ni jumuia ya makanisa yanayomkiri Bwana Yesu Kristo kuwa Mungu na Mwokozi kadiri ya Maandiko, na kwa sababu hiyo yanajitahidi kutekeleza pamoja wito unaoyaunganisha yote kwa utukufu wa Mungu pekee: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu".[2]

Kati ya wanachama 349 kuna Makanisa mengi ya Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki, Wakatoliki wa Kale, Ushirika wa Kianglikana, Waprotestanti kama vile Walutheri, Wamenno, Wamethodisti, Wamoravian na Wapresbiteri, Wabaptisti na badhi ya Wapentekoste.[3] Kumbe Kanisa Katoliki si mwanachama, ingawa linatuma wawakilishi wake katika mikutano.[4]

Kwa jumla yanawakilisha Wakristo milioni 590 katika nchi 150 na jumuia 520,000 zinazohudumiwa na mapadri na wachungaji 493,000.[5]520,000 local congregations served by 493,000 pastors and priests, in addition to elders, teachers, members of parish councils and others.[6]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. World Council of Churches — World Council of Churches. Oikoumene.org (2013-08-04). Retrieved on 2013-08-09.
  2. "About us — World Council of Churches". oikoumene.org. 2013. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-10-14. Iliwekwa mnamo 2013-10-12.
  3. "Member list — World Council of Churches". oikoumene.org. 2014. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-12-25. Iliwekwa mnamo 2014-11-12.
  4. Cross & Livingstone The Oxford Dictionary of the Christian Church OUP(1974) art.
  5. "Who are we?". World Council of Churches. 2003. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-01-07. Iliwekwa mnamo 2007-04-10.
  6. "Who are we?". World Council of Churches. 2003. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-01-07. Iliwekwa mnamo 2007-04-10.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • W. A. Visser 't Hooft, The Genesis of the World Council of Churches, in: A History of The Ecumenical Movement 1517–1948, R. Rose, S. Ch. Neill (ed.), London: SPCK 1967, second edition with revised bibliography, pp. 697–724.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Halmashauri ya Kiekumeni ya Makanisa kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.