Dirisha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Dirisha la hewa chumbani.

Dirisha (kutoka neno la Kiajemi; kwa Kiingereza: window) ni nafasi wazi katika ukuta au paa la jengo, katika gari n.k. Lengo lake ni kuruhusu hewa na mwanga viingie, pia watu waweze kuona nje kwa njia yake.

Kunaweza kuwa na maumbo na ukubwa tofauti, ikiwa ni pamoja na mstatili, mraba, mviringo, au maumbo ya kawaida.

Kwa kawaida hujazwa na kioo ili kuzuia baridi na mavumbi kuingia. Baadhi ya madirisha yana kioo cha rangi, hasa mahali pa ibada.

Kabla ya kioo kilichotumiwa madirisha, watu wa Asia walitumia karatasi kujaza shimo kwenye ukuta. Karatasi ingeacha mwanga.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dirisha kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.