Renaissance

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Shule ya Athens ni mchoro wa Raphael. Haya ni maonyesho ya michoro ya kipindi cha Renaissance picha ya eneo kutoka katika Ugiriki ya Kale, ambao kume shehena wanafalsa maarufu kedekede wa Kigiriki, waandishi, wasanii na wanamahesabu. Raphael alitumia sura za watu mashuhuri wengi kutokana na kipindi chake. Alimtumia Leonardo da Vinci kama mfano wake wa kutengenezea Plato.

Renaissance (pia: zama za mwamko, mwamko-sanaa) ni kipindi cha kihistoria cha Ulaya kilichoanza kunako miaka ya 1400, na kikafuatiwa na kipindi cha Zama za Kati, ambacho pia kinajulikana kwa jina maarufu kama Middle Ages.

Neno "Renaissance" linatokana na neno la Kifaransa lenye maana ya "kuzaliwa upya". Sababu zilizopelekea kipindi hiki kuitwa hivyo ni kwamba, wakati huo, watu walianza kuwa na shauku ya kujifunza kuhusu mambo ya kale, kwa namna moja au nyingi walijufunza kuhusu mambo ya Ugiriki ya Kale na Roma ya Kale.

Kwa masomo hayo Renaissance ilionekana kama "kuzaliwa upya" kwa masomo hayo. Renaissance mara nyingi ilisemwa kama ndiyo mwanzo wa "modern age".

Wakati huo wa Renaissance, kuliwa na wasanii wengi sana, wengi wao walikuwa waandishi na wengi wao walikuwa wanafalsafa. Watu walijifunza mabo ya hisabati na sayansi mbalimbali. Mtu aliye mjanja wa kujua vitu vingi huitwa "Mtu wa Renaissance". Leonardo da Vinci, ambaye alikuwa mchoraji, mwasayansi, mwanamuziki na pia mwanafalsafa, huyu ni Mwana Renaissance mashuhuri.

Awali Renaissance ilianzia nchini Italia, lakini punde ikaenea katika Ulaya nzima. Katika Italia kipindi hiki kimegawanyika katika makundi matatu:-

  • Renaissance ya Awali.
  • Renaissance ya Juu
  • Renaissance ya Mwisho ambayo pia huitwa kipindi cha Mannerist.


Kipindi kilichofuata baada ya Mannerist kilikuwa kinaitwa Baroque pambacho pia kilienea Ulaya nzima kunako 1600. Nje ya Italia, ni vigumu kuelezea wapi kipindi cha Renaissance kiliishia na wapi kipindi cha Baroque kilianza.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Hourglass.svg Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Renaissance kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.