Ufunguo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Ufunguo wa Waviking wa Uingereza (900 hivi BK)
Kufuli za karne za kati huko Kathmandu (Nepal).

Ufunguo (kutoka kitenzi "kufunga", kinyume chake "kufungua") ni kifaa kinachotumika kufungulia au kufungia mlango au kufuli.

Kwa sababu hiyo, mara nyingi huchukuliwa kama ishara ya kumiliki nyumba, sanduku n.k. Mwambatanisho wa kufuli na ufunguo huchangia katika ulinzi kwa maana ni mwenye ufunguo peke yake anayeweza kufungua kufuli.

Historia ya ufunguo[hariri | hariri chanzo]

Historia ya ufunguo yafanana na ile ya kufuli maana zote zilitengenezwa kwa pamoja. Kufuli na ufunguo wa kwanza zilipatikana kule Ninawi. Baadaye, mwambatanisho huo ulipatikana nchini Misri.

Baada ya mfumo huu wa ulinzi kuitikiwa na wote, uvumbuzi uliendelezwa na teknolojia pia kutumika katika kuboresha kufuli na funguo.

Leo, funguo za kisasa zahitilafiana sana na zile za zamani. Hata hivyo, minajili ni ilele: ulinzi.

Funguo za kisasa[hariri | hariri chanzo]

Funguo za leo zina ulinzi mwingi kuliko ule wa zamani. Wezi waliweza kufungua na kuingia kwenye nyumba za kufuli za kitambo maana zilitengenezwa kwa teknolojia dhaifu. Hivi leo, teknolojia ni nzuri na ni vigumu (hata kama bado lafanyika) kufungua kufuli kwa ufunguo usiodhaminiwa kufanya hivyo.

Pia kumekuwa na kufuli zisizohitaji ufunguo wa kawaida bali tu kubofya kwa nambari. Milango hii ni kama ile ya karakana za gari, ya milango ya nyumba na kampuni.

Kuna milango pia ambayo hufunguliwa kwa njia ya kieletroniki baada ya kutambua anayejaribu kufungua.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]