Kufuli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kufuli iliyopatwa na kutu.

Kufuli ni kifaa cha madini kinachotumika kufungia vitu mbalimbali kama vile mlango, sanduku au hata sefu ya kuhifadhia pesa au vitu vya maana.

Kufuli huwekwa kwa ajili ya ulinzi, ili kuepukana na uhalifu wa wizi au hata kupotea kwa vitu.

Kando ya aina hii ya kufuli, ambayo ni madini au chuma, kuna pia kufuli za aina nyingine ambazo hutumia njia tofauti kuhifadhi vilivyo ndani. Njia hizi ni kama neno la siri au mwambatanisho wa batoni za kubofya.

Historia za kufuli[hariri | hariri chanzo]

Mfumo wa kwanza kabisa wa kufuli ulipatikana Ninawi. Kufuli za aina hiyo zilipatikana baadaye nchini Misri ambazo zilikuwa na komeleo, kipande cha mbao na ufunguo wa kufungulia kufuli.

Kufuli ya kwanza ya chuma ilitengenezwa na mvumbuzi Theodoros wa Samos (karne ya 6 KK).

Waroma wa hapo jadi pia walikuwa na mazoea ya kuweka bidhaa zao za maana katika visanduku na baadaye kuning'iniza funguo shingoni. Hili lilikuwa na madhumuni mawili. Kwanza, liliweza kuhifadhi bidhaa zake kutokana na wizi na pili liliwaambia watu kuwa yeye alikuwa tajiri mwenye vitu vya maana.

Kufuli za leo[hariri | hariri chanzo]

Kwa sababu ya teknolojia, kufuli za leo zinatofautiana sana na kufuli za hapo kale. Haya yaliletwa na mabadiliko katika sekta ya viwanda (Mapinduzi ya Viwandani) katika karne ya 18.

Kufuli za leo ni kama vile

  • Kufuli za kieletroniki ambazo hufunguliwa kwa kawi za umeme
  • Kufuli za rimoti zisizo na ufunguo
  • Kufuli za kufungua baada ya kubofya kwa kibodi.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.