Nenda kwa yaliyomo

Familia takatifu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Familia Takatifu)
Familia takatifu, mchoro wa Juan Simón Gutiérrez.
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
Yesu
Yesu Kristo na Ukristo

Umwilisho  • Utoto wa Yesu  • Ubatizo
Arusi ya Kana • Utume wa Yesu • Mifano ya Yesu  • Miujiza ya Yesu
Kugeuka sura • Karamu ya mwisho • Msalaba wa Yesu  • Maneno saba
Kifo cha Yesu  • Ufufuko wa Yesu
Kupaa mbinguni  • Ujio wa pili
Injili  • Majina ya Yesu katika Agano Jipya  • Yesu kadiri ya historia  • Tarehe za maisha ya Yesu • Kristolojia

Mazingira ya Yesu

Wayahudi • Kiaramu • Bikira Maria • Yosefu (mume wa Maria) • Familia takatifu • Ukoo wa Yesu • Ndugu wa Yesu • Yohane Mbatizaji

Mitazamo juu ya Yesu

Mitazamo katika Agano Jipya · Mitazamo ya Kikristo • Mitazamo ya Kiyahudi • Mitazamo ya Kiislamu • Yesu katika sanaa

Familia takatifu, mchoro wa Raphael.
Mwaka wa liturujia
Magharibi
Mashariki
Polidoro wa Lanciano (1515-1565), Familia takatifu na Malaika, 1540 hivi.

Familia takatifu katika Ukristo ni hasa ile iliyoundwa na Mtoto Yesu, Bikira Maria na mtakatifu Yosefu.

Kwa imani ya Wakristo ni kwamba Mungu alipomtuma Mwanae pekee kujifanya mtu hakutaka azaliwe nje ya familia, kwa kuwa hiyo ndiyo mpango wake asili kwa ajili ya watu tangu alipoumba Adamu na Eva akawabariki wazaliane.

Heshima kwa Familia takatifu katika Kanisa Katoliki ilianzishwa rasmi na Fransisko wa Laval, askofu wa kwanza wa New France (Kanada) katika karne ya 17.

Katika Injili

[hariri | hariri chanzo]

Injili ya Mathayo na ile ya Luka zina habari kadhaa kuhusu maisha ya familia hiyo [1] iliyoanza kwa kufuata taratibu za Wayahudi: mwanamume alitoa mapema posa na mahari, hata hivyo hakuanza kuishi na mke wake hadi baada ya mwaka mmoja.

Ni wakati huo wa katikati kwamba, kadiri ya Injili, Maria alipata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Baada ya Yosefu kujulishwa, ndipo alipomchukua nyumbani asifanye naye tendo la ndoa walau hadi alipomzaa mtoto Yesu.

Baada ya Yesu Kristo kuzaliwa Bethlehemu, Injili hizo zinasimulia matukio ya kutahiriwa kwake siku nane baadaye, kutolewa hekaluni siku arubaini baadaye, kukimbilia Misri, kurudi Nazareti na hija ya pamoja kwenda Yerusalemu[2]. Katika hayo yote Yosefu, Maria na Yesu wako pamoja.

Baada ya tukio hilo la mwisho, ambapo mtoto alikuwa na umri wa miaka 12, Yosefu hatokei tena katika Injili, hivi kwamba wengi wanafikiri alifariki kabla Yesu hajaanza utume wake.

Sikukuu ya Familia takatifu inaadhimishwa na Kanisa la Kilatini mwishoni mwa kila mwaka, kati ya Noeli (25 Desemba) na sherehe ya Mama wa Mungu (1 Januari). Lengo ni kufanya familia hiyo iwe kielelezo cha nyingine zote ziishi kitakatifu[2].

Ilipoanzishwa na Papa Leo XIII mwaka 1893 ilipangwa baada ya Epifania (6 Januari), lakini baadaye ilihamishwa.

Katika sanaa

[hariri | hariri chanzo]
Kadi iliyochorwa Familia takatifu, kwa Kifaransa. University of Dayton Libraries.

Familia takatifu imechorwa mara nyingi na wasanii[3][4][5] kwa jinsi inavyohusiana na mambo ya msingi ya maisha ya binadamu wote.

  1. "Martin, James. "The Holy Family", Catholic Update". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-07-05. Iliwekwa mnamo 2017-10-22.
  2. 2.0 2.1 "Strasser O.S,B., Bernard. With Christ Through the Year". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 2017-10-22. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)
  3. "The Holy Family", New York Metropolitan Museum of Art
  4. "The Holy Family", Art in the Bible
  5. "The Holy Family", The J. Paul Getty Museum

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Familia takatifu kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.