Hannover

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mji wa Hannover


Jiji la Hannover
Jiji la Hannover is located in Ujerumani
Jiji la Hannover
Jiji la Hannover

Mahali pa mji wa Hannover katika Ujerumani

Majiranukta: 52°22′0″N 9°43′0″E / 52.36667°N 9.71667°E / 52.36667; 9.71667
Nchi Ujerumani
Jimbo Saksonia Chini
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 519.000
Tovuti:  www.hannover.de

Hannover ni mji mkuu wa jimbo la Saksonia ya chini nchini Ujerumani. Idadi ya wakazi wake ni takriban 519,000.

Mtangulizi wa mji ilikuwa kijiji kando la mto Leine kwenye nafasi ya kuvuka mto huu kwa miguu; mabaki ya makazi yaligunduliwa yaliyokuwepo tangu zamani za uzaliwa kwa Kristo. Soko la "Hanovere" lilitajwa mara ya kwanza mwaka 1150 likapata haki ya mji mwaka 1241. Mji ulikua haraka ukatajirika na kujenga ukuta wa kinga pamoja na minara mingi. 1533 wananchi wa Hannover waliamua kujiunga na mwendo wa uprotestanti wa Martin Luther. Mwaka 1636 mtawala wa tawi moja la watemi Braunschweig-Lüneburg alifanya mji makao makuu yake na tangu mwaka ule Hannover ilikuwa mji mkuu wa sehemu kubwa za Ujerumani ya kaskazini. 1714 mtemi wa Hannover Georg Ludwig alichaguliwa kuwa mfalme George I wa Uingereza akahamia London; wafalme wa Uingereza walikuwa pia watemi wa Hannover hadi 1837 lakini walikaa Uingereza. Tangu 1837 maungano ya kifalme yalikwisha na mfalme Ernst August I wa Hannover alikaa tena mjini hadi 1866, ambako ufalme wa Hannover ulitekwa na Prussia na mji wa Hannover ilikuwa mji mkuu wa jimbo la Hannover ndani ya Prussia.

Maendeleo ya kisasa yalifika mjini kwa kujengwa kwa taa za gesi kwenye mitaa ya mjini mwaka 1825 ilikuwa mji wa kwanza wa Ulaya uliopata taa za gesi mtaani. Reli ya kwanza iliunganisha Hannover na miji ya jirani mwaka 1843. Kuwa sehemu ya nchi kubwa ya Prussia iliongeza nafasi za kiuchumi za mji na idadi ya wakazi ilikua haraka. Mwaka 1871 walikuweko wakazi 87,000 na mwaka 1912 313,000.

Mji ulikuwa na viwanda vingi; kati ya makampuni makubwa yako hadi leo Volkswagen (motokaa), Continental (matairi), Bahlsen (vyakula), Talanx, VHV na Hannover Re (Bima).

Wakati wa vita kuu ya pili ya dunia sehemu kubwa za mji ziliharibiwa na mabomu. Tangu 1946 ilikuwa Hannover mji mkuu na makao ya serikali ya jimbo la Nidersachsen ikaendelea kukua hadi kupita nusu milioni ya wakazi.

Mji una vyuo mbalimbali pamoja chuo kikuu cha Hannover. Ni makao makuu ya kanisa la Kiluteri la Hannover ambalo ni dayosisi yenye wakristo wengi ya kanisa la Luteri duniani.

Kutokana na mahali pake ni kitovu cha usafiri katika Ujerumani maana njia za reli na barabara kuu kati ya kaskazini na kusini pia kati ya mashariki na magharibi zinakutana hapa pamoja na mfereji wa Mittellandkanal.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Ujerumani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Hannover kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.