Lilongwe
Lilongwe ni mji mkuu wa Malawi wenye wakazi 597,619 (sensa ya mwaka 2003). Yenyewe iko kusini magharibi mwa nchi, magharibi mwa Mto Malawi karibu na mpaka wa Malawi na Msumbiji na Zambia. Lilongwe mahali pake ni (-13.98333, 33.78333). [1] Ilihifadhiwa 25 Machi 2011 kwenye Wayback Machine.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Mji huo ulianza kama kijiji kwa ufuo wa Mto Malawi na kuwa Kituo cha amri ya wakoloni Waingereza kwa mwanzo wa karne 1900. Yasemekana kwamba, Lilongwe ilisaidia sana kama kituo cha serikali ya wakoloni kwa sababu Lilongwe ilikuwa kwa ruti ya kusini na kaskazini ambayo iliwezesha utawala wa Rhodesia ya kaskazini inayojulikana sasa kama Zambia. Mji wa Lilongwe baadaye ukawa mji wa pili kwa ukubwa Malawi. Mwaka wa 1974, Mji mkuu wa nchi ulihamishwa kutoka Zomba (mji ambao sasa ni wa tatu kwa ukubwa nchini Malawi), hadi kwa mji namba mbili kwa ukubwa, Lilongwe.
Wilaya
[hariri | hariri chanzo]Mji wenyewe una wilaya nyingi ambazo zajulikana kama eneo, mbila kati ya mji kuwa eneo iliopewa namba. Eneo zenyewe hazijapewa namba kulingana vile eneo zimepakana.
Maeneo yaliyojulikana:
- Eneo 1: Mji wa Wakale (Kati)
- Eneo 2: Mji wa Wakale (Kaskazini mwa A1) - Karibu na Mji wakati
- Eneo 3: Mji wa Wakale (Magharibi mwa A1) - Ufuo wa Magharibi, Mto Lilongwe
- Eneo 4: Mji wa Wakale (Mashariki mwa A2) - Ufuo wa Magharibi, Mto Lilongwe
Usafiri
[hariri | hariri chanzo]Kuna mabasi na motokaa za abiria zinazosafirisha watu kwa miji ya kale, katikati ya Mji wenyewe na pia Kiwanja cha denge. Mataksi yapatikana rahisi kutoka kwa na taksi kwa jia inayoitwa Presidential Way, kaskazini mwa maduka za soko zilizokati ya Mji.
Jumla
[hariri | hariri chanzo]Lilongwe inao Wakazi Wakigeni na kwa hivyo waweza kupata chakula za kutoka ng'ambo kwa maduka.
Kuna chuo cha ukulima mjini Lilongwe. Wakati wa mvua hasa ni Oktoba na Aprili. Wakati wa ukame ni kuanzia Aprili hadi Oktoba. Kati ya muda huu wa ukame, Juni na Julai kuna baridi na Agosti kukizidi na upepo na vumbi.
Uchumi
[hariri | hariri chanzo]Viwanda hasa ni kama za tumbako, chai, sukari, utolezi wa vyumo vilivyo siagwa, simiti na vyakula.
Ukulima ni kama wa tumbako, miwa, mipamba, chai, mahindi, viazi, mikota, mihogo, mituta, na pia kwa wanyama ni kama ng'ombe, mbuzi. Mashamba ya ukulima ni kama 34% za nchi.
Vifaa vinavyouzwa kwa nchi za kigeni ni tumbako, chai, sukari, pamba, kahawa, chungu na mbao.
Vifaa vinavyonunuliwa kutoka nchi za kigeni ni vyakula, mafuta, vifaa vilivyoundwa, vifaa vya utumizi na vifaa vya usafirishaji.
Madini na mali ni kama simiti, madini ya yuranimu ambayo hayajachimbwa, makaa ya miamba, madini ya shabu au alumini.
Mambo ya mazingira; ukataji wa miti; mmomonyoko wa udongo; ujanaba wa maji, maji ya siwa (ya choo), takataka za viwanda; samaki kupunguka kwa kuaribu eneo za yai za samaki.